JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
Salamu wanabodi!
Kwa muda sasa nimekuwa nafuatilia maoni ya wananchi kuhusu utawala wa Magufuli , nimebaini jambo moja bays sana kwa mstakabali wa Nchi yetu.
Kuna kundi kubwa sana hasa miongoni mwa wasio soma na wasio na kitu' the have nots' kuona kwamba sababu ya wao kuwa masikini ni watumishi wa umma. Ndio maana ikitokea Rais amemtumbua mtu yeyote wao hufurahi bila kipimo bila kujali haki imetendeka au laa!
Juzijuzi nilikuwa Mtwara sehemu Fulani, mara akaja Kijana anaendesha Gari ndogo nzuri, vijana waliokuwa wamekaa pale wakasema 'fedha zetu hizo' ! Mmoja akasema' wanatuibia sana'. Hapa kuna tatizo tena kubwa.
Bahati mbaya ni kwamba hata mwelekeo wa serikali hii Ni sawa na wao. Haiwezekani Rais aseme kuwa madai ya walimu Ni hewa wakati anajua sehemu kubwa ya deni hilo amelisababisha yeye! Vijana masikini wanaona kila Mwenye uwezo maana yake ni mwizi!
Ni hatari kupandikiza chuki kwa wananchi, Rais ni lazima apime Maneno take.