Chunda
Senior Member
- Apr 7, 2016
- 182
- 251
Kama ilivyoripotiwa na gazeti la Raia Mwema toleo Na 505 la tarehe 12-04-2017, Uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha uliitangazia Dunia kwamba Chuo hicho kimegundua aina mpya ya Chopa (Helikopta).
Kulingana na uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hiyo ni kwamba kinachodaiwa kuwa ugunduzi ni sawa tu na mchezo wa watoto kuigiliza kutengeneza gari kama wanavyoyaona barabarani. Cha ajabu ni pale ambapo habari hiyo ya ugunduzi wa helikopta Tanzania ilivyosambaa Duniani kama vile ni jambo la kweli lililofanyiwa utafiti na kugundulika.
Tanzania ni sehemu ya Dunia yenye wasomi wanaoaminika na kutambuliwa Duniani. Tungekuwa kisiwa tunakoishi peke yetu tungeweza kujifanyia mambo ya kienyeji kama tunavyotaka. Lakini kwa kuwa sisi ni sehemu ya Dunia inafaa tuende kama Dunia inavyotaka kwa mambo yanayohusu utafiti na ugunduzi.
Inapotokea habari kama hizi za ugunduzi ambao haujafanyiwa utafiti na ambao bado haujathibitishwa na mamlaka za kitaifa zinazotambulika, kurushwa nje ya nchi na hasa pale ambapo habari hizo siyo za uhakika ni kasoro kubwa sana kwa nchi mbele ya uso wa kimataifa. Inakuwa mbaya zaidi pale ambapo taarifa hizo zinapotolewa na Taasisi ya Serikali inayoshughulika na Elimu, Utafiti na Ushauri wa kitaalamu.
Habari za ugunduzi kama hizi zingeandikwa na mafundi wa mtaani ingeweza kuonekana ni jambo la kawaida. Lakini zinapoandikwa na Taasisi ya elimu ya juu inayoaminika kuwa ni ya wasomi ambao huamini katika utafiti ni jambo la ajabu na la kutia aibu, ndani na nje ya nchi.