Ni hakika kabisa unaweza kufanya biashara kariakoo hata kwa mtaji kidogo tu

Ni hakika kabisa unaweza kufanya biashara kariakoo hata kwa mtaji kidogo tu

fact only

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2024
Posts
975
Reaction score
1,356
Habari wakuu.

Unaweza ukawa una wazo(idea)+mtaji(capital) lakini hauelewi uanzie wapi au haujui ni biashara gani ufanye ikupe matokeo mazuri pia (place)location gani nzuri au kuna wengine wanatamani kuja kariakoo na hawajui waanzie wapi maana wanasikia kuwa kariakoo fremu bei juu, wanasikia kariakoo ili upate fremu ni lazima ulipie kilemba n.k

Sasa nataka nikwambie hapa kariakoo zipo fremu za bei chee tu unapata bila hata ya kulipia kilemba hivyo hata wewe mwenye mtaji mdogo unaweza ukaanza biashara yako taratibu na taratibu taratibu ukakuza mtaji wako. Fremu zipo kuanzia 150,000..........800,000.

Kwa maana hiyo basi wale wote wanao hitaji fremu za kuuzia nguo, viatu, urembo, vyombo, huduma za kifedha kama M-PESA , MIXX BY YAS zamani TIGO PESA, AIRTEL MONEY, HALO PESA, CRDB wakala, NMB wakala, NBC wakala n.k, kuuza simu, kuuza underwear(boxer,chupi,soksi,taiti n.k), kuuza vinywaji kama soda, maji, juisi n.k, kuuza vifaa vya simu, kuuza vyakula, kuuza mifuko kwa jumla, kuuza t shirt, kuuza vifaa vya ujenzi, fremu za pharmacy, stoo za mizigo, kuuza vifaa vya saloon, kuuza computer, kuuza nguo za michezo, stationary n.k karibuni vigoli na fremu zipo nyingi sana.
 
Back
Top Bottom