Ni furaha tupu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni furaha tupu!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Dec 12, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mwezi huu ni mwezi wa furaha kwani siku chache zijazo tutaanza kusikia kila kona ya miji mbalimbali duniani kote ikitawaliwa na nyimbo na mapambo ya X-Mas na mwaka mpya. Hii inaonyesha ni jinsi gani siku hiyo ilivyo ya furaha.

  Tengeneza furaha katika moyo wako, anza kujijenga kisaikolojia mapema, hata kama huna pesa, usijisike vibaya, tumia kidogo ulicho nacho na mwenza wako kwa hakika mtalidhika na mlichonacho.

  Kubwa zaidi katika mwezi huu unapaswa kuepuka kujifananisha na fulani, usitake kufanya jambo fulani kwa kuwa fulani kafanya jambo fulani, epuka madeni ili usherehekee sikukuu za mwezi huu vizuri. Kikubwa ni wewe kuwa na furaha katika moyo wako. Kama mnajiweza msisite kujumuika na familia nzima katika moja ya sikukuu, kwaajili ya chakula cha mchana.

  Ni mwezi wa kutembelea marafiki na kujuliana hali, lakini pia ni mwezi wa kutafakari mafanikio mliyoyapata katika maisha yako na maisha yenu ya kimapenzi. Tafuta kitu kizuri cha kumfanyia mpenzi wako ili mfunge mwaka kwa furaha kwa kumfanya asahau mabaya yote uliyomtendea ndani ya mwaka huu.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Haya, wengine ni wazee mno kujifananisha na wengine.

  asante - sred ya Lizzy
   
 3. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #3
  Dec 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  teh!teh! unanifurahisha sana kwani wazee huwa hawana furaha!tena utakuta kama ni babu/bibi akiwa na furaha utaona meno ishirin nje maana sio tena thelathin na mbili megine yameshang'oka ni mapengo!

  [​IMG]
   
Loading...