Wakuu Kwanza samahanini kwa kuwasumbua, Pili. Lengo la uzi huu ni kuomba ushauri wenu kwa kilichonipata. Nitaenda kuwahadithia kwa kifupi sana
.
Mimi ni kijana wa kiislamu, naishi dar, mwezi mmoja uliopita au mwezi na nusu nilidhulumiwa pesa tsh 2.7M ( million 2 na laki 7 ) sikwambii maumivu nilionayo moyoni, yaan naumia sana halafu alionidhulumu ni mtu wangu wa karibu sana, mtu niliemuamini kwa kila kitu, nimekuwa nikiomba mungu, mungu naomba unilipie, mpe mabalaa na mikosi ya kila aina, huwezi amini hata saiv nnavyoandika uzi huu nimetoka kuomba, lakini naona bado mungu hajanilipia. Je nifanyaje, kuna duah gani ya kumuomba mungu ampe mikosi??? Yaani kiasi kwamba ajute kula jasho langu, mm ndio kwanza mwaka huu nimefungua kibiashara changu nimeanza kutafuta maisha af ananidhulumu. Nifanyaje??? Ndugu zangu naumia mnooo
Sent using
Jamii Forums mobile app