Ni dawa gani niitumie kutibu uvimbe kwenye haja kubwa

profesawaaganojipya

JF-Expert Member
Apr 21, 2015
1,485
3,133
Niende moja kwa moja kwenye mada.

Wakuu ni dawa gani inaweza kutibu viuvimbe na vidonda sehemu ya haja kubwa,na wakati wa kujisaidia damu inamwagika na maumivu makali,

pia vinawasha sana.

Ni dawa gani ninunue dukani inayoweza kunisaidia.
IMG_20240220_225512.jpg
 
Niende moja kwa moja kwenye mada.

Wakuu ni dawa gani inaweza kutibu viuvimbe na vidonda sehemu ya haja kubwa,na wakati wa kujisaidia damu inamwagika na maumivu makali,

pia vinawasha sana.

Ni dawa gani ninunue dukani inayoweza kunisaidia.
View attachment 2910621

UGONJWA WA BAWASIRI (HEMORRHOIDS)​





Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

AINA ZA BAWASIRI
  1. NJE
    Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
  2. NDANI
    Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
    Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
Je bawasiri husababishwa na nini?

BAWASIRI HUSABABISHWA NA NINI?
Bawasiri husababishwa na;
  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
  • Umri mkubwa
DALILI ZA BAWASIRI
  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa

MATATIZO YANAYOWEZA KUTOKEA KUTOKANA NA BAWASIRI
  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids

VIPIMO NA UCHUNGUZI
  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

MATIBABU

Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri
  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
  • Upasuaji;
Hemorrhoidectomy
Stapled hemorrhoidopexy


NJIA ZA KUZUIA BAWASIRI
  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa
TIBA YA MARADHI YA BAWASIRI
TIBA:
Jambo la kwanza kabla ya tiba mgonjwa aweze kutibiwa maradhi ya kutopata choo vizuri ikiwa anayo kwa sababu huzidisha maradhi haya. Pia epuka kula Nyama hasa ya ngombe, Pilipili na vitu vikali. Halkadhalika usinywe maziwa kwa wingi.
Ukitaka dawa ya kuwezakumaliza hayo maradhi yako nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibia maradhi yako upate kupona uguwa pole.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom