Ni Busara Sana Mh. Edward Lowasa kustaafu siasa.

Mtoto Wabibi

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
451
294
Mh Lowasa ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe sana nchini.Hivyo ni busara na pia tumuombe mzee wetu Lowasa astaafu siasa kutokana na political situation ya sasa kama alivyofanya Dr. Slaa Mwaka Jana kipindi cha uchaguzi.
aternative yake ya kustafu siasa :

Ni vizuri ajisafishe upya kwa kutumia mahakama.Au njia/mbinu yoyote mpya akishirikiana na chama ili kumaliza huu mzizi wa fitina kwa maadui zake kisiasa na kujenga imani zaidi kwa watanzania. Na hapo anaweza kuisimamia nia yake ya kugombea tena 2020 na wananchi wakampa kura.

Ikishindika hiyo alternative basi astafu siasa Kwa sababu zifuatazo.
1: Alifanikiwa sana kujisafisha kisiasa lakini hakutakata vizuri. toka kipindi cha " kujivua gamba" hadi uchaguzi wa 2015 alifanikiwa kwa asilimia kubwa sana.Lakini kutokana na kutojisafisha sawa sawa na kuacha mabaki imegeuka tena kuwa kikwazo zaidi.Kashfa hizi zinaonekana kuathiri upande wa upinzani sana na hata kukosa imani kwa wananchi.

2:Kwa umri wake na uwezo wake ametumikia vya kutosha sana watanzania hivyo itakuwa busara kuwaachia vijana wapambane kwani imeonekana kufifisha upinzani kwa kashfa zake.

Vinginevyo upinzani unaelekea kushindwa au kupotea kabisa nchi.
Hatima ya upinzani ipo mikononi mwa Lowasa ( kuuimarisha au kuua) na sio mtu mwingine.

Nawasilisha
 
Aliyekwambia kwamba unaweza staafu siasa ni Nani? Siasa is all about life, kwa hiyo unamaanisha akisha staafu siasa halafu akaona mfn.sukari imepanda bei asiongee? Maana akiongea lazima aguse siasa, siasa ina determine maisha yatu ya kila Siku ndy maana hakuna anayeweza kujitenga na siasa hata Mapadre na mashehe wameshindwa hilo.
 
Back
Top Bottom