Ni busara kumpokea Rais Zuma kipindi hiki ambacho nchi yake haimtambui kama Rais?

NTEGEYE Jr

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
322
286
Naomba kuuliza, Je ni busara kumpokea Mh. Jacoub Zuma kipindi hiki ambacho Taifa lake halimtambui kama Raisi wao?
 
Anapokelewa na nani?, hebu wataje kwanza wanaompokea ili tuwajadili kwanza hao wanaompokea maana hao ndiyo wanaweza kuwa tatizo
 
Kuuliza ni ujinga coz ujinga ni kukosa akili au taarifa wikipedia defn. Lakini kwa kifupi waweza jiuliza tu hilo taifa halimtambui kwa namna gani huku alichaguliwa na bado ni rais hadi sasa!! kama hawamtambui informally hiyo ni kimpango wao but officially bado anatambulika na dunia kuwa ni Rais wa SA.
 
Naomba kuuliza, Je ni busara kumpokea Mh. Jacoub Zuma kipindi hiki ambacho Taifa lake halimtambui kama Raisi wao?
hata mwenyeji wake Pamoja na pacha wake hatambuliwi na ukawa, wacha watapetape siku zinaenda
 
Huyo ni Rais na bado ANC haijasema Mtukufu Rais Zuma hawamtambui wewe huku unashakia nini wakati kibanzi kilichopo machoni mwako hujakiondoa??? Mbona huko wako safi na wanaendelea kujenga uchumi wao hadi wanamtuma Rais wao aje kuona fursa za uwekezeji mnaacha kuzitumia....tuache kushabikia tufanye kazi uchumi upo tunawaachia wengine kumbuka Net Group Solution , ATC NBC.........
 
maana ya Busara ni nini? we unataka kujivisha usouth Afrika kutokana na ushabiki wa kijinga, he's a Republic of South Africa's president, fujo za wasauzi haziondoi itifaki za kimataifa.
 
Umeuliza swali ukasema kwenye headline yako Rais Zuma,,chini ukasema muheshimiwa dah akili zile zile
 
Ni nafuu kwa NCHI kumpokea ZUMA angalau ujio wake unaweza kuleta matokeo katika siku za mbeleni.

Safari ya bwana ZUMA ni ziara RASMI kabisa iliyo ratibiwa na NCHI yake kwa kodi za wana SA..

Hakuna asie jua...ni idadi ya watu wangapi anafuatana nao katika ZIARA hii ambayo wengi katika msafara ni WAFANYA BIASHARA..

Pamoja na misukosuko ya KISIASA anayo kumbana
nayo kutoka kwa WANASIASA pamoja na RAIA wake...mazingira haya hayawezi kubadili MAHUSIANO na USHIRIKIANO mwema tulio nao kati yetu Watanzania na jirani zetu kutoka katika nchi ya MADIBA....

Kama nchi tutazame FURSA za kibiashara anazo kuja nazo bwana ZUMA..

Matatizo yao KISIASA tuwaachie wenyewe...

Ni BORA tungehoji USHIRIKA wa mkuu wa nchi JPM na mkuu wa chama cha upinzani nchini KENYA bwana RAILA...

Tujitathimini TUNAJENGA ama TUNABOMOA.....!!!?
 
hawamtambui kivipi? unaweza elezea namna ambavyo unaona hawamtambui? katiba yao inasemaje na amevunja kifungu gan cha katiba


Naomba kuuliza, Je ni busara kumpokea Mh. Jacoub Zuma kipindi hiki ambacho Taifa lake halimtambui kama Raisi wao?
 
Back
Top Bottom