Ni biashara huru au kuingiliana kwa majukumu?

mayowela

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
2,125
Reaction score
1,757
Ni biashara huru au kuingiliana kwa majukumu? Hiki kitu nimekiona muda na huwa najiuliza kama ni soko huru kila mtu anafanya awezavyo ilimradi kodi iende kwa wahusika.

Kumekuwa na muingiliano wa kibiashara kwa makampuni makubwa, mwanzo kulikuwa na malalamiko ila Regulators hawakutaka kuyakumbatia na wakatoa go-ahead, bwana kama mwenzio anafanya hivi na wewe fanya, kilichotokea ndiyo hiki tunakiona sasa hivi.

TELECOM COMPANIES
Hawa biashara yao kubwa ni Data na Sauti, ila baadae wakaona sio kesi mbona kuna hili Bank hawalioni, wakaanzisha Mobile financial service, kila kona kukawa na Wakala wa huduma za pesa kwa njia ya simu, na biashara ikashamiri, haya makampuni leseni yalitoa wapi kuanza huduma za fedha? Benki kuu ndio ilitoa na kusimamia, baadae Ma bank wakalalama kuwa wanaibiwa wateja, msimamizi mkuu akaona kama hawa mbona hawana uwezo wa kufikiri, akawatimulia mbali (hapa tunaona Mtandao wa simu unafanya kazi ya Bank)

FINANCIAL INSTITUTION
Bank baada ya kuona kama wamepigwa TKO wakaona sio issue, wakaja na wao na huduma ya Wakala, kila Bank ikaja na huduma hio kama kusogeza huduma karibu na mteja, wakaenda mbali wakaona ili biashara hii ishamili, wakaanza kuajiri wafanyakazi kutoka kwenye makampuni ya simu ambao wanaijua biashara hiyo na baadhi yao wanafanya vizuri.

Hawa hawa waliokenda kulalama kuwa wanaingiliwa majukumu, wakaanzisha huduma ya Bima, karibu bank nne nazifahamu zinatoa huduma ya bima, na msimamizi wa Bima akatoa leseni na biashara inaendelea na wanachukua wafanyakazi kutoka kampuni z Bima, Swali ni Je, kampuni za Bima nazo zimelalama kuwa wanaingiliwa kwenye uwanja wao?

INSURANCE COMPANIES
Hawa nao, waliona hapana tusitegemee wateja wa mtaani tu, wakapanua fikra, wakaenda TCRA kuomba kibali ili watumie wateja ambao tayari ni base ya mtandao fulani wa simu na likafanikiwa

NB: Pia kuna makampuni ya huduma za fedha/ mikopo yanatumia wateja ambao ni wa makampuni ya simu kutoa mikopo, Je kwa sasa hii ni Biashara huru?
 
Kwa dunia ya sasa sio mpaka mtu au kampuni fulani itoe huduma ile tu zama zimebadilika na kila kitu kinatakiwa kumfikia mteja mlangoni kwake. Sioni kosa waangalie ni jinsi gani mteja atanufaika na sio nani kaibiwa biashara yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwahiyo hii ni sawa, na sio kwa baadhi ya makampuni kulalama, inatakiwa wajue na wao wanaingiaje kwenye biashara ambayo imevamiwa na kampuni zingine
 
Back
Top Bottom