Ni biashara gani ndugu zangu inaweza kuniingizia elfu saba kwa siku?

Nimepiga mahesabu yangu ya maisha, kwa kuanza nahitaji walau elfu 9 Mpaka 10 kwa kila siku niiweke.

Biashara gani itanipatia wastani wa Elfu 9-10 kwa kila siku?
Nataka nijiajiri.

Hapa nina mtaji wa laki mbili cash. Naweza kuongeza hata ikafika laki tatu, ila niwe na uhakika wa kupata elfu kumi kwa kila siku kama faida.

Naweza kwenda kuishi Mkoa wowote Tanzania, ila hela hiyo uhakika wa kuipata uwepo.
Nisaidieni...

Mtaji; Laki mbili
Hela ninayotaka kuingiza; Wastani wa elfu kumi kwa siku.
Cheza single betting. Weka under 5 mara nyingi hula kwa hiyo laki 2 hukosi 10 kwa siku
 
1. kama upo dar es saalam, anza kutengeneza kahawa na kasheti; tafuta vijana waamifu 5 waanze kukutembezea
2. Tafuta meza ya matunda Eneo lolote la chuo ama sehemu nzuri ile ya watu waliostaarabika wanaojali afya na kujua umuhimu wa kula wa matunda.
3. Fungua genge la chakula sehemu zilizochangamka tafuta wadada wasafi na mvuto kiasi wakuzunguka vijiweni na maofisini kukuuzia na kukutafutia masoko. Chakula kitamu na bei iwe inaendana na hali za watanzania.usitake faida kubwa
4. Wengine wataendelea zipo nyingi tu naamini
 
niko dar sasa hivi, Ila fursa hata ikiwa mkoani nitaifata.
Katika hiyo hela...toa hapo 50,000 tu....damka saa 9 usiku Anza safari ya kwenda karume..natumaini mpk kufikia saa 11 Alfajiri utakuwa umeshafika Karume nenda ka point viatu vya mtumba vya kike...maana itakuwa rahisi kuvijua vizuri ni vipi...anza kupitisha mtaani...hautojuta hiyo hela unayoitaja ni faida ya pair moja tu ya kiatu...Muhimu ujue kuchagua. Niliwahi kufanya hiyo biashara ina faida Sana ingawa watu wanawadharau Machinga ila Kuna Siri kubwa wasiyo ifahamu. Kupata faida ya Tsh 40,000 kwa siku ni Jambo la kawaida, muhimu uwe pointer mzuri.
 
1. kama upo dar es saalam, anza kutengeneza kahawa na kasheti; tafuta vijana waamifu 5 waanze kukutembezea
2. Tafuta meza ya matunda Eneo lolote la chuo ama sehemu nzuri ile ya watu waliostaarabika wanaojali afya na kujua umuhimu wa kula wa matunda.
3. Fungua genge la chakula sehemu zilizochangamka tafuta wadada wasafi na mvuto kiasi wakuzunguka vijiweni na maofisini kukuuzia na kukutafutia masoko. Chakula kitamu na bei iwe inaendana na hali za watanzania.usitake faida kubwa
4. Wengine wataendelea zipo nyingi tu naamini
Namba 2 akizingatia atapata faida hata zaidi ya hiyo anayotaka ila no 3 kwa mtaji wake ni ngumu kidogo
 
Katika hiyo hela...toa hapo 50,000 tu....damka saa 9 usiku Anza safari ya kwenda karume..natumaini mpk kufikia saa 11 Alfajiri utakuwa umeshafika Karume nenda ka point viatu vya mtumba vya kike...maana itakuwa rahisi kuvijua vizuri ni vipi...anza kupitisha mtaani...hautojuta hiyo hela unayoitaja ni faida ya pair moja tu ya kiatu...Muhimu ujue kuchagua. Niliwahi kufanya hiyo biashara ina faida Sana ingawa watu wanawadharau Machinga ila Kuna Siri kubwa wasiyo ifahamu. Kupata faida ya Tsh 40,000 kwa siku ni Jambo la kawaida, muhimu uwe pointer mzuri.
Hii biashara iko vizuri best yangu anafanya hii anasifia inalipa kiasi
 
1. kama upo dar es saalam, anza kutengeneza kahawa na kasheti; tafuta vijana waamifu 5 waanze kukutembezea
2. Tafuta meza ya matunda Eneo lolote la chuo ama sehemu nzuri ile ya watu waliostaarabika wanaojali afya na kujua umuhimu wa kula wa matunda.
3. Fungua genge la chakula sehemu zilizochangamka tafuta wadada wasafi na mvuto kiasi wakuzunguka vijiweni na maofisini kukuuzia na kukutafutia masoko. Chakula kitamu na bei iwe inaendana na hali za watanzania.usitake faida kubwa
4. Wengine wataendelea zipo nyingi tu naamini
Ushauri mzuri
 
Back
Top Bottom