watu wengi huwa wanadharau biashara fulani kwa kujiona wana elimu ya darasani!!
Kuna mama mmoja alikuwa anahojiwa anasema katika biashara yake ya kukaanga mihogo anapata faida ya elf 10. Anaanza kazi sa moja hadi sa sita mihogo ishaisha.
Ukipiga mahesabu kwa mwezi utaona faida yake.
Nina uhakika kuna watu wapo kwenye ofisi za watu zenye majina makubwa ila mishahara yao hata laki haifiki na wanatumika asbuh hadi jioni.
Inawezekana vielimu walivyonavyo wanaona kuna baadhi ya biashara hawastahili kuzifanya. Inawezekana wewe ni mmojawapo.
Biashara ni ngumu sana, inataka usimamizi wa hali ya juu, usipokuwa makini utabaki kusimulia kuwa nilikuwa na 5m/= juzi juzi zimekwisha, ukiweza weka kwenye fixed deposit, kama bado ipo, then tulia tuli.

duuuh kweli kuitafuta pesa ndipo uanze kuwaza uifanyie nini its hard game KIKUBWA CHA KUKUSHAURI WAONE CONSULTANCY wapo wengi au jiangalie kipi unakipenda ukitaka ufanye biashara kisa pesa utaumia maana utakosa passion na nidhamu ya fedha waone wakushauri kwanza au vipi mtafute mfanyabiashara aliyefanikiwa eneo lakp akushauri