Ni aibu sana mke, mume na watoto familia moja wote kuwa facebook

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Turudi kwenye mambo ya ndoa sasa, unakuta mume akipost kitu fb, mke ana-like au kucomment kiroho safi tu. Au wakati mwingine vice versa is true.

Kweli umeoa /umeoa na unamwona mwenzio Facebook na bado tu unajisikia amani??Duh.

Bora mmoja awe fb, mwingine asiwepo kabisa. Ni heri awe anadeal na JF tu kuliko kukutana na mke/mume wako fb. Watoto nao wako fb.Kazi mtindo mmoja.

Tubadilike jamani,fb siyo nzuri sana.
 
huwa najiuliza kama mke na mume na watoto mna mawasiliano ya karibu kuna haja gani kurushiana post na ku-reply na ku-like na ku-share?
kama kuna mjadala si mufanye ana kwa ana tu? kuna kuiga kwingine kwa kijinga sana. sasa mzazi ukiona post za picha za utupu za marafiki wa watoto wako utamlaumu nani?
 
Da watu tuna mitazamo tofauti kwa kwa kweli !sijui face book watu mnaichukulia kama ibada au dubwan la ajabu sana eh?
Ngoja nikusogeze karibu kwa kizazi cha sasa ni kawaida mkaoana na kila mtu akaendelea ku keep rafiki zake na wengi wapo face book right?
Then marafiki wako baadhi wanakuwa marafiki wa mwenzawako kupitia fb.
Baadae mnakuwa na friendly chat btn the two of u au yeyote yule na wote mki engage katka mazungumzo yenu ya kistaarab nini tatizo?
Ila kwa nyie wenye marafiki wa ajabu ajabu ambao kwenu ni fahari unapokuwa na "rafiki"kama 1000++ ambao asilimia 99 huwajui in person well mna reason za ku ogopa kuwa in FB na wenzi wenu sis wengine asilimia 99 rafiki zetu ni real sio virtual ni watu tunaowajua natunatembeleana majumbani kwetu
 
Eeh bwana bora hio ya familia.. Juzi kati nikapata friend request toka kwa house girl wetu wa kitambo kile, sijakaa sawa namuona mwalimu wangu wa madrassa,.. Hadi Fundi baiskeli kijijini kwetu yuko Fb... Sawa TECNO werevaaa wamerahisisha maisha, lakiniiii... Daaah
 
Turudi kwenye mambo ya ndoa sasa, unakuta mume akipost kitu fb, mke ana-like au kucomment kiroho safi tu. Au wakati mwingine vice versa is true.

Kweli umeoa /umeoa na unamwona mwenzio Facebook na bado tu unajisikia amani??Duh.

Bora mmoja awe fb, mwingine asiwepo kabisa. Ni heri awe anadeal na JF tu kuliko kukutana na mke/mume wako fb. Watoto nao wako fb.Kazi mtindo mmoja.

Tubadilike jamani,fb siyo nzuri sana.
Sio nzuri kivip? dadavua ueleweke maana hata kisu ni kizuri unakatia kitimoto unakula lakini kinaweza pia kugeuka silaha na kusababisha mauti
 
sio ustaarabu kwa kweli... yaan wengine marafik zetu post zao hazipaswi kabisa kuonwa na wazazi... hapa kweli ni tatizo!
 
FB ni nzuri kama tu una marafiki wanaijielewa,unaweza kuitumia kuwasiliana na pia kutangaza biashara yako,lakini ukiwa na marafiki na wengi wao huwafahamu,tegemea tu kulikuta picha la ngono na mipicha ya uchi..
 
Mmmmh, mie wa miaka ile hata Mamangu hajui data ni kitu gani.!! Hii yawahusu watoto wa digitali
 
Mimi Mwanaume ukishakua unamiliki akaunti facebook...instagram na unatupia vipicha vyako vya selfie nakuona huna tofauti na kinaJamesDelicious
 
Sikumbuki ata applctn ya fb ipoje vile maana nlishaitoa kabisa in my phone japo naishi kibachela
 
Kila mtu ana uhuru wa kupata taarifa inategemea mnatumiaje mitandao. Kwangu si jambo baya.
 
Sina account ya FB wala Insta ila nina account WordPress.

Unakuta msomi ana picha 1000 insta na FB ila hana makala hata moja mtandaoni!

Call me J
 
FB ni nzuri kama tu una marafiki wanaijielewa,unaweza kuitumia kuwasiliana na pia kutangaza biashara yako,lakini ukiwa na marafiki na wengi wao huwafahamu,tegemea tu kulikuta picha la ngono na mipicha ya uchi..

Nilijifunza kutobeba ovyo sijui friend of a friend, sijui nani FB. Mambo ya mipicha michafu wanayotundika inabore mpaka basi, na usiombe yakukute kwenye computer ya kazini.
 
Back
Top Bottom