Ni aibu kwa Jeshi la Polisi kutoa sababu za uwongo wa kiwango hiki katika kuvunja mkutano wa ACT Wazalendo!

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,486
30,166
Hivi Jeshi la Polisi linawafanya watanzania wote ni wapumbavu na malofa wanaoweza kuwadanganya wapendavyo??

Tumesikia taarifa waliyotoa jana katika kuuvunja mkutano wa ACT wazalendo kuwa eti wameuvunja mkutano huo kwa madai kuwa wamehofia kutokea kuvunjika amani kutokana na taarifa za kiintelejensia walizo nazo kuwa kikundi cha CUF cha Lipumba kina mpango wa kuwafanyia fujo chama hiko cha ACT wazalendo!

Sababu zilizotolewa ni za uwongo wa hali ya juu ambazo hakuna mtanzania yeyote anayeweza ziamini

Kwanza, nini wajibu wa Jeshi letu la Polisi nchini??

Inajulikana wazi kuwa Jeshi la Polisi nchini wajibu wake mkubwa kabisa, ni kuwalinda raia na Mali zao.

Sasa inakuwaje tena hao raia wanaopaswa kulindwa na Jeshi la Polisi, Jeshi hilo hilo lenye silaha za kivita, liwaogope raia ambao hawana hata visu, kuwa eti wana mpango wa kuwafanyia vurugu hao ACT wazalendo katika mikutano wao??

Hivi ni mkutano gani ungeweza kuwa wa hatari zaidi, ni ule wa Profesa Lipumba wa majuzi wakati wakimuidhinisha Profesa Lipumba katika uenyekiti wake wa "magumashi" au ni huu mkutano wa Maalim Seif wa kuwaeleza sera wanachama wao wa ACT wazalendo??

Ilikuwaje hili Jeshi la Polisi likatoa ulinzi mwanzo hadi mwisho katika mkutano wa Profesa Lipumba na wakati huo huo mkutano wa ACT wazakendo wakidai kuwa "wanawaogopa" hao wafuasi wa Lipumba, hadi kuwalazimisha kuuvunja mkutano huo??

Kama alivyonukuliwa Rais Magufuli mwanzoni mwa mwezi huu, wakati akiliongelea suala la utekwaji kwa mfanyibiashara maarufu nchini kuwa Jeshi la Polisi lisiwafanye watanzania wajinga, kwa kuwaongopea kuhusu "movie" yao waliyocheza ya kutekwa kwa Mo, ambapo hadi Leo hajakamatwa mtuhumiwa yeyote na Kamanda Mambosasa alionekana kunywa nao chai akina Mo!

Hatuna budi watanzania kwa ujumla wetu tukatae kufanywa wajinga na Jeshi hili la Polisi, kwa kutoa visingizio vyao visivyo na kichwa wala miguu, ili mradi wahalalishe katika kutumika kwao na chama tawala cha CCM
 
Labda ndo style mpya mkuu!
Hata wakipata taarifa za kiintelejensia kuwa kuna majambazi yatavamia mtaa flani inabidi wawahamishe wananchi ili majambazi yakija yakute holaaaaah!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ama kweli kama hiyo ndiyo staili mpya ya kutupiga "fix" kwa hao maaskari wetu

Basi tuna Maaskari badala ya kulinda raia na mali zao, wao ni kufanya usanii tu
 
Kimya cha CUF kina maana gani? Je, wanakubali kwamba walitaka kutia fujo kwenye huo mkutano wa ACT? Kama ni kweli kwanini Msajili asiwaandikie barua ya kuwafuta kwasababu ni chama cha fujo? Mambo ni mengi muda ni mchache
Umehoji kitu cha msingi sana

Kama ni kweli chama cha CUF kilitaka kufanya fujo kwenye mkutano wa ACT wazalendo, ni kwanini msajili wa vyama, Jaji Mutungi hajakifuta chama hicho, kutokana na kuwa chama hicho kina mlengo wa vurugu badala ya kuwa chama cha siasa??

Maswali ni mengi yanayokosa majibu
 
Inavyoelekea huko tuendako mikutano ya CCM itakuja kuvunjwa kwa kuwa kuna tishio la CUF kuvamia mkutano huo.

Sitashangaa siku mechi ya Simba na Yanga ikazuiwa na Polisi kwa kuwa kuna taarifa za kiintelegensia kuwa CUF watavamia Uwanja wa Taifa!

Mbaya zaidi kuna siku panya road wataachwa wakabe na kupora mtaa hadi mtaa kwa kuwa watakuwa wamevaa fulana zenye nembo ya CUF na Polisi wetu wanawaogopa CUF kama EBOLA!
 
Kwakweli ni aibu kwa jeshi hili, maana kutokana na tukio hili angalau polisi imewafungua macho watanzania kwamba uaminifu kwa jeshi tunalopaswa kuliamini ni mdogo.
Mpaka sasa sijajua kwamba wanachama hao wa CUF wana jeshi lenye mizinga au makomandoo wa hali ya juu kiasi gani mpaka waogopwe na polisi wetu.
Na jambo baya mpaka sasa hawajamkamata mtu hata mmoja miongoni mwa wale waliokusudia kwenda kumwaga damu ya viongozi wa ACT Wazalendo.
Ushauri.
Polisi Tanzania kuendelea kutumika na wanasiasa, wataleta mpasuko kwenye umoja wetu na kulivunjia heshima jeshi la polisi tunaloliamini
 
Hivi Jeshi la Polisi linawafanya watanzania wote ni wapumbavu na malofa wanaoweza kuwadanganya wapendavyo??

Tumesikia taarifa waliyotoa jana katika kuuvunja mkutano wa ACT wazalendo kuwa eti wameuvunja mkutano huo kwa madai kuwa wamehofia kutokea kuvunjika amani kutokana na taarifa za kiintelejensia walizo nazo kuwa kikundi cha CUF cha Lipumba kina mpango wa kuwafanyia fujo chama hiko cha ACT wazalendo!

Sababu zilizotolewa ni za uwongo wa hali ya juu ambazo hakuna mtanzania yeyote anayeweza ziamini

Kwanza, nini wajibu wa Jeshi letu la Polisi nchini??

Inajulikana wazi kuwa Jeshi la Polisi nchini wajibu wake na, moja ni kuwalinda raia na Mali zao.

Sasa inakuwaje tena hao raia wanaopaswa kulindwa na Jeshi la Polisi, Jeshi hilo hilo lenye silaha za kivita, liwaogope raia ambao hawana hata visu, kuwa eti wana mpango wa kuwafanyia vurugu hao ACT wazalendo katika mikutano wao?

Hivi ni mkutano gani ungeweza kuwa wa hatari zaidi, ni ule wa Profesa Lipumba wa majuzi wakati wakmuidhinisha Profesa Lipumba katika uenyekiti wake wa magumashi au ni huu mikutano wa Maalim Seif wa kuwaeleza sera wanachama wao wa ACT wazalendo??

Ilikuwaje hili Jeshi la Polisi likatoa ulinzi mwanzo hadi mwisho, wakati hiuu mkutano wa ACT wazakendo wakidai kuwa "wanawaogopa" hao wafuasi wa Lipumba, hadi kuwalazimisha kuuvunja mkutano huo??

Kama alivyonukuliwa Rais Magufuli mwanzoni mwa mwezi huu, wakati akiliongelea suala la utekwaji kwa mfanyibiashara maarufu nchini kuwa Jeshi la Polisi lisiwafanye watanzania wajinga, kwa kuwaongopea kuhusu "movie" yao waliyocheza ya kutekwa kwa Mo, ambapo hadi Leo hajakamatwa mtuhumiwa yeyote na Kamanda Mambosasa alionekana kunywa nao chai akina Mo!

Hatuna budi watanzania kwa ujumla wetu tukatae kufanywa wajinga na Jeshi hili la Polisi, kwa kutoa visingizio vyao visivyo na kichwa wala miguu, ili mradi wahalalishe katika kutumika kwao na chama tawala cha CCM
- KumbukiziMTAFUTANO.jpg
 
Kwakweli ni aibu kwa jeshi hili, maana kutokana na tukio hili angalau polisi imewafungua macho watanzania kwamba uaminifu kwa jeshi tunalopaswa kuliamini ni mdogo.
Mpaka sasa sijajua kwamba wanachama hao wa CUF wana jeshi lenye mizinga au makomandoo wa hali ya juu kiasi gani mpaka waogopwe na polisi wetu.
Na jambo baya mpaka sasa hawajamkamata mtu hata mmoja miongoni mwa wale waliokusudia kwenda kumwaga damu ya viongozi wa ACT Wazalendo.
Ushauri.
Polisi Tanzania kuendelea kutumika na wanasiasa, wataleta mpasuko kwenye umoja wetu na kulivunjia heshima jeshi la polisi tunaloliamini
Baada ya CCM kung'olewa rasmi 2020 kama dunia nzima inavyotarajia , jeshi la polisi litavunjwa na baadhi ya viongozi wake akiwemo Mambosasa watakamatwa
 
Jeshi la police linaiogopa CUF?hao CUF wamekuwa ni magaidi kiasi kwamba police inawahofia?
Msajili wa vyama anafanya nini/chukua hatua gani kwa hicho chama cha ugaidi CUF?
asipokiwajibisha hicho kikundi,mbeleni atakuja kujuta maana kesi huwa haiozi
 
Jaji Mutungi basi waandikie kabarua CUF angalau uwape onyo au wakueleze ni kwanini usikifute chama chao kutokana na shtuma zilizotolewa na jeshi la polisi ana wao bado wapo kimya.
Kweli kabisa tena tuhuma zimetolewa na vyombo vya usalama hakika CUF wafutiwe usajiri
 
Waliweza kulinda mkutano wa propesa ili achaguliwe na maalim atemwe lakini wameshindwa kulinda mkutano wa zzk na maalim ahutubie. Wanamhitaji Yesu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni ajabu na kweli kuona Jeshi la Polisi linaulimda mkutano wa kuchaguliwa kimangu mashi Profesa Lipumba, lakini Jeshi hilo hilo linashibdwa kuulinda mkutano wa chama cha ACT wazalendo, wa kueleza seta zao!
 
Kama ni hivyo maombi ni muhimu wapendwa
Hakika kwa utendaji kazi wa Polisi wa awamu hii, inabidi tuliombee Jeshi hilo ili litende kazi bila kupendelea upande wowote wa chama, kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi
 
Back
Top Bottom