Ni aibu kubwa sana kukuta kijana wa kiume au wakike mwenye umri wa miaka 35+ bado anaishi kwao au kwa wazazi

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,403
40,316
Ni aibu kubwa sana kukuta kijana wa kiume au wakike mwenye umri wa miaka 35+ bado anaishi kwao au kwa wazazi.

Hii ni aibu kubwa sana, na ni ishara ya kutokujitambua. Inakuwaje kwa umri huo ungojee chakula cha shikamoo, uchonge ndevu wakati unaishi kwenu au upishane na mzazi huku amefunga taulo kiunoni?

Mwenye umri huo anayeishi kwao abadilike, nyumba za kupanga ziko nyingi tu, hata chumba cha 10,000 kinapatikana.
 
Inategemea na tamaduni zenu kwetu sisi ni jambo la kawaida sana hata uwe na uwezo ikiwa hujaoa au kuolewa utaishi kwenu kwa hiyo mila zinatofautiana
Nakubaliana na wewe,tamaduni zingine si nzuri kwa afya;mfano tamaduni za kutokutairi kwa me hazina mantiki,ni uchafu tu.
 
Back
Top Bottom