Ni ACCA au CPA?

kamwendo

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Posts
908
Reaction score
1,939
Habari Wakuu,

Nakalibia kumaliza usajili wa kusomea ACCA ile ya worldwide ambayo makao makuu yake yako London, Ila kwa hapa nchini wana branch yao pale posta.

Swali langu kwenu Je, kuna yeyote aliyesomea ACCA kwa distance learning na akafanikiwa kuhitimu kwa wakati?

Je, kipi kina faida zaidi Kati ya ACCA na CPA (T)?

Hawa jamaa kwa mujibu wa maelezo yao wanasema unapohitimu ACCA unakuwa Qualified moja kwa moja kuchukua Master's ya Accounting and Finance Chuo Kikuu cha London U.K

Naomba kwa mwenye kufahamu kuhusu hili atuweke wazi hapa kwa faida ya wote.
Mie ni muajiriwa na nipo mkoani kanda ya nyanda za juu, Nimekuwa interested na hii kitu kwa muda sasa.

Natanguliza shukrani.
 
ACCA, waweza fanya kazi nchi yoyote Duniani, ina kila kitu mle, kuanzia Managerial, Finance, IT, Chain Supply to Logistics education..kila la heri..
 
ACCA, waweza fanya kazi nchi yoyote Duniani, ina kila mtu mle, kuanzia Managerial, Finance, IT, Chain Supply to Logistics education..kila la heri..
Asante Sana Mkuu, Barikiwa
 
kama una uwezo kifedha fanya ACCA,najua gharama ni kubwa sana ukilinganisha na CPA, ila ukimaliza pia unaweza pata cpa ya bongo kwa kufanya masomo matatu business law,taxation 1 and taxation 2,hapo utakuwa umeua ndege wawili kwa jiwe moja,wengi ikiwemo mimi nilishindwa kufanya ACCA kwa sababu ya gharama nikaopt kufanya cpa tnakaribia kumaliza
 
Naunga mkono hoja, fanya ACCA halafu ukimaliza unafanya CPA unakua exempted unafanya masomo mawili kama sijakosea ambayo ni Taxation lingine sikumbuki ili uwe CPA qualified. Tuji-position kimataifa ni vizuri zaidi ili upanue wigo wa ujuzi na kuajiriwa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…