NHIF mnazingua

Saint Changas

Member
Dec 19, 2015
24
32
NHIF itumbuliwe

Tunatambua umuhimu mkubwa wa mfuko huu wa bima ya afya lakini huduma zao haziridhishi.

Shirika hili limekua likichelewesha vitambulisho vya bima y afya kwa wanachama ilhali wanakata fungu lao tangu mshara wa kwanza.

Wachangiaji wa mfuko huo wanalalamika kwa kulazimika kulipia huduma za afya wao na wategemezi wao licha ya kuchangia kila mwezi.

Na asilimia kubwa ya watumishi katika mfuko huu wa bima ya afya hawana majibu ya kuridhisha wanapofuatwa kutoa majibu.

Ikibidi uongozi wa mfuko huu wa bima ya afya utumbuliwe ili wawekwe watu wapya watakaoweza kutoa huduma stahiki kwa wachangiaji.
 
Hivi kwani ni Hiari kujiunga au Lazima?
Maana mie naona mfumo huu bado haujawa rafiki kwa Tanzania.
Ukienda na Pesa unaheshimika,na Kadi unaonekana kama kabwela tu umechoka.
Wakati wenzetu Ulaya,mwenye Kadi akifika sehem anaheshimika balaa,na mwenye pesa ndio anaonekana wa kawaida saana na yupo nje ya wakati

Mie bado sana,kwanza naona nikijiunga nitakuwa kila siku homa haziishi,maana niliwahi kuwa na Kit ile ya first Aid,basi kila siku nikiziona nasikia home,basi nilipoacha tu kuweka homa sipati teeena.
 
Mimi nina mwaka wa nane huu wanachukua tu hela yangu na wale ndugu zao cwt wakati sijawahi kuwaomba kujiunga. Sheria nyingine bhana! zinaleta mashaka mengi ya ufisadi.

Anyway ngoja tu nikawapigie magoti nijisajili kuliko kuendelea kutafuniwa tu hela yangu kila mwezi.
 
NHIF NI JIPU MNO na wanahitaji review unalipa hela nyingi baadhi ya huduma mpaka uende HQ kupata approval.
Miwani hakuna nk wakati viongozi me vx kilimo kwanza.
Shame on you
 
Wanakera mno hospital zote kama Dar haawakubali cars zao ni TMJ ...Kairuki na Recency wengine hawataki
 
Jamaa ni majipu sugu wale, bora huko Dar. Mikoani Huduma Yao ndiyo inatia kichefuchefu. Hospitali za binafsi hazitaki kuziona kabisa kadi zao. Imefikia hata wanufaika tunaona haya kuvionyesha hadharani kwa jinsi vinavyodharaulika.
 
Hawa jamaa nilishaa baada ya kukataliwa huduma ya SINDAMO ya elfu 80 ktk hospitali kubwa hapa ktk ya mji wanadai natakiwa nitoe cash... Nilipouliza KWA nn nitoe cash wakati Nina kadi ya uanachama...Aisee
 
Hawa jamaa nilishaa baada ya kukataliwa huduma ya SINDAMO ya elfu 80 ktk hospitali kubwa hapa ktk ya mji wanadai natakiwa nitoe cash... Nilipouliza KWA nn nitoe cash wakati Nina kadi ya uanachama...Aisee

Hili ni tatizo sugu sana linalo wakabili Wanachama wa Mfuko wa NHIF. Unaenda hosp. Dr. Ana recommend utumie dawa Fulani, ukienda huko pharmacy za ndani ya hosp, unaambiwa dawa hizi Unatakiwa kulipia Cash, huku wakiendelea kusisitizia kuwa hatA Hazina Bei. Sasa kama Hazina Bei!!? Kwa nn nilazimishwe kulipia!?

Ukiomba ile form ambayo inakuruhusu uende nayo kwenye maduka yao wanakuambia pia form hawana au zimewaishia.

Hiii ni kero Kubwa sana. Ambayo inatupata sisi wanachama wao.
 
NHIF wako vizuri sana ni changamoto ndogo ndogo tu ambazo wakizifanyifanyia kazi, trust me, hakuna mfuko mzuri kama huu
 
Back
Top Bottom