NHIF wana mkataba na watoa huduma na sehemu ya mkataba unaainisha bei za dawa na vipimo pamoja na consultation. Hakuna mahali mtoa huduma anaweza kujiandikia tu bei ya dawa.Kumekuwa na taarifa zikiripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari ya kwamba mfuko wa bima ya afya kukumbwa na changamoto mbalimbali za ukwasi, na hii inadhihirishwa na NHIF wenyewe walivyokuja na mwongozo kwa wanufaika wa idadi ya siku za kwenda kupata matibabu kwa mwezi na baada ya siku chache wakasitisha.
Wanachama wengi wa NHIF wamekuwa wakilalamika na hata kugombana na baadhi ya wahudumu wa hospitali hususani za private kwenye kipengele kidogo cha kujaza gharama za matibabu. Wahudumu wengi wanajaza baada ya mgonjwa kuondoka na haijulikani wanajaza kiasi gani hii hali inapelekea NHIF kuyumba kipesa.
Nchi yetu ina watalamu wengi sana wa mifumo, ningeshauri zile sms wanazotuma mara baada ya mnufaika kupata huduma basi ziambatane na bei husika iliyotumika, hii angalau inaweze ikasaidia kunusuru NHIF kufirisika.
Hili jambo nadhani linahitajika kujadiliwa kwa ukweli na nia njema bila ya kuleta chembe chembe za ushabiki bila ya kulijua jambo. NHIF kuharibika kwake kunatokana na usimamizi hafifu na mbovu na wala si michango ya wanachama.NHIF wana mkataba na watoa huduma na sehemu ya mkataba unaainisha bei za dawa na vipimo pamoja na consultation. Hakuna mahali mtoa huduma anaweza kujiandikia tu bei ya dawa.
Hii ndio point kubwa, serikali inachangia sana kufilisi hii mifuko ya uchangiaji halafu wanarudi kwa Gia ingineWe need to go into the primary aim of NHIF ilianzishwa kwa lengo gani kipato chao kilikuwaje? matumizi yao? na Fedha zilizokopwa na serikali zilisha rudishwa? usikute Serikali kuu inahusika na kufilisika huko mnataka kuhamisha tatizo hili kwa wachangiaji.
Same as mifuko mingine ya jamii shida ni hiyo hiyo, awamu iliyopita walimerge hii mifuko shida ni hiyo hiyo kufilisika na uwekezaji usiona mashiko bila kuangalia return na demand za wenye mifuko husika.
Kwenye nchi zenye discipline ya fedha nifuko kama NHIF inapesa nyingi sana hata kufikia kununua hati fungani za kiserikali na sio kujiingiza kwenye miradi ya real estate kama hapa au serikali kuchukua fedha bila ahadi maalum za urejeshaji.
Na sasa serikali inaingilia jinsi ya kubadili sheria na kumbana mchangiaji ambae kimsingi ndio owner wa mifuko hii. Hii ni very bad.
Serikali irejeshe pesa yote ya mifuko hii ya jamii in full na kuachana na uwekezaji kwenye maendeleo bila kumjali wananchi wake. Primary issue kwa serikali ni watu wake sio vitu au madaraja tu.
Je mtu akipimwa malaria baade ile form ikaongezwa amepimwa na typhoid nk nk nk? wapi inaonesha kuwa ile form sasa imefungwa/haiwezi kuongezwa chochote, baada ya mgonjwa kusaini. Najua wapo watoa huduma waaminifu sana ila kuna mianya mingi kila mahala ya kupiga dili. sasa badala ya kuthibiti mianya kwanza wanapambana na wenye mfukoNHIF wana mkataba na watoa huduma na sehemu ya mkataba unaainisha bei za dawa na vipimo pamoja na consultation. Hakuna mahali mtoa huduma anaweza kujiandikia tu bei ya dawa.