NHC, Tibaijuka na mali za Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NHC, Tibaijuka na mali za Watanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lukansola, Jun 2, 2011.

 1. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Gazeti la NIPASHE la jana jumatano tarehe 1, Juni 2011, lenye kichwa cha habari "Tibaijuka ategwa nyumba za NHC." linatia kichefuchefu, eti wapangaji wa nyumba za shirika hilo zilizopo upanga, wanalazimisha kupitia waziri mwenye thamana wauziwe nyumba hizo. Vigezo na sababu walizozitoa ni dharau, kejeli na ubinafsi ulio kithiri, eti wanasema wao ni wajane, yatima kwa hiyo waonewe huruma. Ni yatima na wajane wangapi wanao ishi kwa umasikini ulio kithiri, ni nani asiyejua kwamba idadi kubwa ya wanaoshi kwenye nyumba hizo ni wale wanojiita wantazania wenye asili ya kiasia? Sio siri kwamba nyumba nyingi sana za mjini zinazomilikiwa na NHC zimepangishwa kwa wahindi, tunafahamu kwamba nhc inazo nyumba nyingi katika maeneo mbalimbali ya nchini, sasa tujiulize ni kwa nini hatuoni wahindi wakipanga Mburahati, Magomeni, nk. Kwa nini wengi wao wapate nyumba mijini? Hivi ni sahihi kuamini kwamba wanaoishi kwenye nyumba za nhc ndio masikini kuliko wanatanzania wengine?

  Hawa jamaa ni wezi, na ni katika kundi lile liliuziana nyumba zetu kwa bei ya kutupa na bila kutushirikisha. Wenye nchi, hivi ni nani anayewapa mamlaka ya kufanya watakavyo? na sisi tuliowaweka pale kutuongoza tutaendelea kuonewa, kunyanyaswa na kuonekana majuha hadi lini?

  WATANZANI imefika wakati wa kusimama na kupinga uonevu huu kwa nguvu zote bila kujali tofauti zetu za kiitikadi. Ni mali nyingi za umma zinawanufaisha wachache kwa misingi ya kibaguzi. Tuamke! wakati umefika wa kusema” sasa basi imetosha.” Wote ni watanzania na tunastahili mgao sawa wa keki ya taifa. Na kwa waziri, ajue kushirikina na walangunzi hao kunamvunjia heshima na kutoa taswira hasi kwa jamii, hao wote watambue kuwa watanzania wote tumelaani dhulma na bado tunaamini siku moja tutapata kiongozi wa Taifa mpenda haki atakaerudisha nyumba hizo kwa wananchi.

  Ningependa kusikia maoni yenu kuhusu suala hili wadau.
   
Loading...