NHC ni chanzo cha foleni Dar es salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NHC ni chanzo cha foleni Dar es salaam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dear, Jan 28, 2011.

 1. D

  Dear Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kama wiki hivi imepita niliona kwenye vyombo vya habari,Shirika la Nyumba linampango wake wa kubomoa nyumba za historia za Upanga na Kariakoo ili kujenga maghorofa kwa ajili ya kutoa tatizo la makazi jijini Dar es salaam.Mimi nilijua kuwa huu uongozi mpya uliowekwa na Chiligati ni ungekuja kuleta mabadiliko kwa kuzuia kubomoa jumba za zamani ambazo ni za kihistoria kujua Dar imetoka wapi na kwa kweli ni imara kuliko hata zile zinazojengwa sasa hivi.

  Na huu ujenzi wa maghorofa marefu hadi ghorofa 11 kwa Upanga ni kusabasha foleni na kukosekana kwa parking,na kuleta msongamano mkubwa mjini pasipo na maana yoyote.

  Na nahisi kuna mikataba ya walakini ya hawa wahindi wanaonunua hizi nyumba za chini za NHC na kujenga maghorofa marefu. Cha kushangaza zaidi wanasema wanapunguza matatizo ya makazi,mimi sifikiri kama ni kweli maana hizi nyumba zikiisha hawakai tena waswahili,ni wahindi kuanzia chini hadi juu,na kuna tetesi kuwa mswahili akienda kuomba upangaji kwenye hizi nyumba mpya zinazojengwa wanatajiwa bei kubwa sana kiasi anajiona hawezi kuafford kabisa, lakini kwa hawa wahindi wenzao wakienda wanaambia bei za chini ili waweze kupanga.

  Kwa taifa jamani hii ni fedheha sana na sijui wanaonaje kwenye kujenga huko mbali kuendeleza mji badala ya kung'ang'ania sehemu moja hapa mjini.

  NHC na wizara ya mama Tibaijuka liangalieni hili,kuongeza makazi ya watu sio kung'an'gania mjini tu hata huko mbali ya mjini maghorofa yanaweza yakajengwa.
  Embu fikiria sasa hivi hadi miundo mbinu ya maji taka haifai tena, pale Agha Khan baharini ni hapafai kabisa harufu kinyesi unakiona juu kabisa,na watoto wetu wa kiswahili wanatoka huko magomeni na kariakoo nao wanakuja kuogelea kwenye mazingira machafu,hii ni yote ni kwa sababu ya NHC kung'ang'ania mjini.

  TUMECHOKA KUCHAKACHULIWA JAMANI
   
Loading...