NHC na NSSF zifutwe na kuundwe taasisi mpya zenye ufanisi na tija kwa umma

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Endapo raisi atasikiliza ushauri wangu, naamini kabisa mashirika haya makubwa yatafutwa na kuunda taasisi imara sana na zenye nguvu ya kiuchumi, lkn yenye tija kwa maendeleo ya nchi! Issues za cost effectiveness lazima zizingatiwe!
Ushauri wangu ni kuwa baadhi ya Taasisi ziunganishwe ili kupunguza mzigo wa huendeshaji lkn pia kuongeza tija ktk utendaji! Labda tuangalie maeneo kadhaa yanayofaa kwa marekebisho!
  1. Kupunguza idadi ya mashirika ya umma yanayofanya kazi moja na hivyo kuongeza mzigo kwa serikali!
    1. Mfano wa hili ni mifuko ya hifadhi za jamii ambayo yote inalengo moja, na yote ipo chini ya Jamhuri! Matokeo yake tumeunda ofisi nyingine SSRA ambayo inaisimamia mifuko hiyo! Ikumbukwe wakurugenzi ndio watu wenye mishahara mikubwa kuliko mtumishi mwingine wa umma including Mkuu wa nchi! Sasa kama tume-merge wizara au kufuta vitengo ili tubane matumizi nadhani wakati sasa umefika wa kuiunganisha hii mifuko! Idadi ya wafanyakazi isipunguzwe kuongeza ufanisi, Ila wakuu wake wapunguzwe kutoka karibu 6 kwa sasa hadi 1! Watakaobaki, watakuwa wakiongoza kurugenzi mbalimbali za mfuko huo mmoja! Hii itasaidia kufanya harmonisation ya funds na utendaji! Pia malipo tofauti kwa beneficiries wa ngazi moja ya mshahara na makato isingeweza kutokea kama ilivyo sasa! Pia SSRA ingekuwa natural death hivyo kuokoa pesa nyingi!
    2. NDC na NHC nadhani wanafanya kazi zote za maendeleo, so ujenzi wa nyumba na Nyanja nyingine za maendeleo vingeunganishwa!
    3. Sanjari na kuziunga NDC, NHC na ule wa muunganiko wa mifuko ya hifadhi, hilo shirika jipya na nyumba na maendeleo ya miji, lingefanya kazi na hii mifuko kupitia bank yao ya umoja! Badala ya shughuli za maendeleo na ujenzi kuwa chini ya shirika moja moja, huku NHC, huku PSPF, NSSF, PPF etc, then wote hawa pesa zao zipite ktk bank yao na NDC/NHC (shirika jipya) likopeshwe kusimamia mipango ya uendelezaji miji, makazi, Viwanda vya kati na shughuli nyingine za maendeleo!
    4. Katika sekta ya Bima, tuunge NHIF na NIC, kwa kuwa zote ni Bima Ila ni just branches tofauti! NIC inakaribia kufa, inawatumishi wengi ambao NHIF ingewatumia bila ya shida!
Msingi wa kuunganisha idara au taasisi sio tu utapunguza gharama kwa kupunguza wakurugenzi wakuu, bali pia utaruhusu utilisation ya resources ambazo nyingine zinatumika kidogo huku wengine wakiwa na upungufu na wengine wakiwa na plenty!
Kwa ilivyo sasa baadhi ya ofisi kama TRA inafanya ktk sekta tofauti bila ya kubadilishwa au kuzaliwa taasisi nyingine! Vinabaki kuwa vitengo tu ndani ya mfumo mmoja, kama wanaosimamia ushuru wa forodha bandarini na airports, biashara ndogondogo, nyumba/majengo, leseni za udereva etc! Hizi ofisi tunazoomba viunganishwe zinaweza kufanya review ya model ya TRA na jinsi inavyofanya kazi kwa ufanisi! Kukua kwa taaluma ya IT na uwepo wa harmonisation ya taarifa za kibank, mishahara, vitambulisho vya taifa, tin number kwa watanzania na mpango wa universal Bima ya afya vyote vinazua ushawishi wa kumerge taasisi, ili monitoring na issues za accountability/transparency ziimarike zaidi!
Toa maoni yako kusaidia kujenga mifumo bora zaidi ya kuimarisha uchumi!
 
Ufanisi ni jambo muhimu sana. Lazima upembuzi yakinifu ufanyike katika kuunganisha hizi taasisi .
Kuunganisha kuwa taasisi moja isije ikawa ni chanzo cha huduma mbovu.

Na pia inangaliwe hizi taasisi kama zinajiendesha zenyewe kwa faida sio haja ya Kuunganisha.
 
Kwa nchi hizi zinazoendelea zipo sababu za ki usalama na kiuchumi,ambazo zinazuia uwezekano wa kuwa na mashirika yenye nguvu sana kifedha kuizidi serikali yenyewe.Kwa kuzingatia hayo hamna uwezekano wa kuyaunganisha.
 
Na hasa ukizingatia serikali yenyewe imekopa na inamadeni makubwa kwenye hizi taasisi.
 
Tuanze na wizara kwanza marekani na ukubwa wote wana wizara 15 tu amabzo wao huziita departments ,sisi huku tuna wizara kibao na makatibu wa wizara mpaka watatu kwenye wizara moja angalia wenzetu wa marekani wizara zao the Secretaries of Agriculture, Commerce, Defense, Education, Energy, Health and Human Services, Homeland Security, Housing and Urban Development, Interior, Labor, State, Transportation, Treasury, and Veterans Affairs, as well as the Attorney General.
 
Hakuna sababu ya msingi ya kuyaunganisha... Yaachwe yashindane.
Ni ushindani usio na tija!
Mbona TRA inafanya vema ikiwa ni moja ya Taasisi pana sana nchini!
Mimi siuoni ushindani wa pspf, PPF, GEPF na NSSF ktk mafao, naona mashirika ambayo moja linachuma pesa na kuwekeza ktk rasilimali na mengine yakipewa pesa na baadhi kutoa mafao makubwa kwa watumishi wa serikali kuu, bila ya vigezo vya msingi!
Hebu tazameni upya kweli PPF na NSSF wanashindana ktk lipi?
Vipi kuhusu NHIF na NIC?
Zinashindania wapi?
Tuache hofu, tuanze kujipanga upya na kutazama uwezekano wa kuboresha mifumo yetu ya uchumi, ni kazi kubwa sana kusimamia hii mifumo yote na watendaji wote!
 
Bichwa lako la habari na utumbo wako wa habari ni vitu tofauti.

Utakuwa ni kanjanja wa magazeti ya udaku.
 
Ufanisi wa mashirika haya uko duni sana ingawa wameanza kuamka hivi karibuni. Yaunganishwe tu
 
Bichwa lako la habari na utumbo wako wa habari ni vitu tofauti.

Utakuwa ni kanjanja wa magazeti ya udaku.
FaizaFoxy angalau siku moja na wewe uache kupenda ugomvi!
Hebu pumzika na mzee saa nyingine utunze familia kama huna cha kuchangia!
 
Kwa nchi hizi zinazoendelea zipo sababu za ki usalama na kiuchumi,ambazo zinazuia uwezekano wa kuwa na mashirika yenye nguvu sana kifedha kuizidi serikali yenyewe.Kwa kuzingatia hayo hamna uwezekano wa kuyaunganisha.
Hebu elezea vema!
Yaani nchi iogope mashirika yake kuwa na uchumi mkubwa?
Bado lkn zipo taasisi nyingi tu nchini ambazo zipo super rich ukilinganisha na idara za umma! MF. Mengi na IPP, Azam, Mo etc! Kama wakishindwa kufanya mashirika ya umma yawe na uchumi imara, basi ipo saa mashirika binafsi yattasumbua nchi!
 
Soma bichwa lako la habari, kama si uongo huo ni nini?
Ok!
Vichwa lilisema hivi: NHC na NSSF kufutwa
Haya huo Utumbo wako ulianza hivi:
" Endapo raisi atasikiliza ushauri wangu, naamini mashirika haya makubwa yatafutwa...."

Hapo Faiza ina maanisha yatafutwa tu, endapo raisi atasikiliza ushauri wangu, kama hatonisikiliza basi hayatafutwa! Hapo kitu gani hakiendani! Umechoka Faiza, ukimalliza kubeba box lala kwanza halafu ndio uje JF, shida yako ukipata uchochoro tu wa kuzogoa unawahi huku!
Haya pole kwa kazi za mchana kutwa!
 
Jibichwa lako la habari limeshafutwa na kurekebishwa.

Kwa hiyo wacha porojo za kutetea uongo. Sasa ulivyoandika bichwa lako la ku mislead watu kama ulikuwa si uongo kwanini lirekebishwe?
 
Dada fox faisal usitukane leta point,Mtoa hoja yuko wazi kuchangia mada,na point zake ziko sawa hata kama zinaonekana kupotezea wengine ajira,uzalendo mhimu sana ndio tutasonga mbele.Mashirika haya yamegawanyika na yote yanfanya kazi moja. Kuyaunganisha ni sahihi kabisa.Mfano angalia NHC ina wafanyakazi wangapi na wanazalisha nini je wanazalisha mpaka ziada? PPF ,NSSF,na mengineyo yako chini ya SSRA nashauli hayo yote yangekuwa ni shirika moja. Nadhani mtoa mada amengalia kwenye aspect ya financial and economic development aspect. NIC &NHIF wanafanya kazi gani zenye utofauti?kwa ni nini isiwe shirika moja lenye nguvu.Tanzania Kurugenzi ni nyingi sana zinazofanya kazi ya aina moja kwenye mashirika yanayofanana.Okay its employment nature but also reforms as well kwa pale ambapo hapana umuhimu. Cost serving ni muhimu sana.Nakupongeza mtoa mada ongeza bidii
 
Jibichwa lako la habari limeshafutwa na kurekebishwa.

Kwa hiyo wacha porojo za kutetea uongo. Sasa ulivyoandika bichwa lako la ku mislead watu kama ulikuwa si uongo kwanini lirekebishwe?
Shida yako unadhani vitu hubadilishwa kwa kuwa ni vibovu! La hasha kuna wakati tunabadili vitu ili kuboresha zaidi! Mods wameiweka sawa zaidi na Mimi nawashukuru kwa kazi yao!
The same thread niliiweka na decent heading kwa 5 hours haikuwa na uchangiaji, nimeitwist heading kidogo kuwaleta watu wachangie!
Pole kama in any way nilichofanya kilikuletea taharuki! Sikupanga kukunyima raha!
Ok! Now unasemaje, jibichwa limebadilishwa, je tuzivunje hizi kurugenzi zinazofanana tuunde kurugenzi moja yenye nguvu au vipi?
 
Tatizo ni uongo na mods wameliona hilo.

Zingine ni porojo za kujitetea tu, huna jipya wala la maana.
 
Back
Top Bottom