Nguzo kuu za kweli CHADEMA ni zipi?

Nguzo kuu za kweli CHADEMA ni zipi?

safisha

New Member
Joined
May 5, 2013
Posts
3
Reaction score
0
Mara nyingi yamekua yakisemwa mengi,pengine ni kutokana na msukumo wa kimakundi kutokana na ukuaji wa chama ama vinginevyo.Watanzania wamekua wakiendelea kushuhudia mengi toka kwa wabunge wetu wa CHADEMA.

Swali la msingi ni kua,wapi wanaobeba sura ya uzalendo,ubinafsi wa umaarufu wao kwa malengo yao na mengineyo?

GT,tujaribu kuchambua kwa kina pasipo matusi,kuwasaidia watanzania angalau kupata dondoo toka kwetu.

Idadi ya wafatiliaji wa mtandao huu inazidi kuongezeka hivyo tutumie hoja kwenye uchambuzi wetu.
 
nguzo kuu ya chadema ni "NGUVU YA UMMA"
Full stop.
 
tuanzena za ccm.
mi nafikiri vyama vimeshaachana na nguzo,imani na sera vingine vimetekwa na mafisadi,majangili na wahujumu uchumi wakati vingine vikiangalia nyakati na mahitaji ya umma ya sasa .
 
Kama alivyosema mdau hapo juu; hakuna kitu kinachoitwa "Nguzo Kuu ZA ..." bali "Nguzo Kuu YA ..." nayo sio nyingine bali "The PEOPLE - UMMA". Na juu ya nguzo hii zimejengwa KATIBA, FALSAFA, ITIKADI, n.k. Na kwamba madaraka na mamlaka ya Chama yana/yatatokana na mhimili huu - the PEOPLE. Na kwamba "The PEOPLE" ukiamua madaraka ya Chama yakome, yatakoma mara moja bila kukawia.
 
Wakati Nguzo Kuu ya Chadema ni "The PEOPE"; nguzo za CCM na CUF ni zipi? Si vibaya pia kuzifahamu tukajadili and then tuka - compare and contrast.
 
nguzo ya ccm na cuf ni serikali ya umoja wa kitaifa e.g zanzibar....
 
nguzo ya ccm na cuf ni serikali ya umoja wa kitaifa e.g zanzibar....

Issues tatu kwa haraka haraka:-

1. Serikali ya umoja iko kule Zanzibar pekee; kwa hoja yako unamaanisha kwa upande wa bara CCM na/au CUF hawana nguzo yoyote?

2. Kwa kuwa nguzo ya CCM na CUF ni moja (kwa hoja yako); itakuwa sahihi kusema vyama hivyo viwili ni kitu kimoja? Yaani CUF sio chama cha upinzani kama kinavyotaka kujinasibisha mbele ya jamii?

3. Kwa kuwa kimojawapo kati ya hivyo viwili kimeonekana sana kushabikia makundi ya kidini ya siasa kali hususan kule Zanzibar, na kwa kuwa vinasimamia nguzo moja na kwa maana hiyo ni vimoja; je ni sahihi kusema kwamba vyote vinashabikia siasa kali zinazoelekea kujipenyeza nchini?
 
Ama kwa hakika huu mtiririko una mashiko na unaweza aminisha watanzania/wafatiliaji wa mtandao huu wa kijamii,kua ni kweli hii ni nyumba/mtandao wa GT..
Inapendeza tukiwa na mwenendo kama huu kwa faida ya Taifa letu.
Mungu ibariki Tanzania..
Tuendelee GT.
 
nguzo kuu ya chadema ni UMMA. Yaani watu na ndiyo maana mara nyingi kinashirikisha watu katika kutoa maamuzi
 
Back
Top Bottom