Nguvu za usalama katika siasa na teuzi

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
11,136
19,871
Natumai wana jf mu wazima wa afya hata kwa wale wenye shida kiafya M/Mungu awapeni wepesi,
Ndugu wana jf nimeleta uzi huu ili kuweza kuwafungua macho ndugu wengi humu walio na mitazamo hafifu juu ya viongozi wa nchi na mafungamano ya kiusalama, hapa nazungumzia hapa nchini kwetu Tanzania, Fahamu haya:-

1. Kuwa waziri mkuu lazima uwe mwana usalama yaani TISS
Hili wengi hawajui undani wake na inaweza kushangaza sana, waziri mkuu ni coordinating person ambaye majukum yake ni makubwa sana kwani ni ngazi ya pili tu kutoka urais,
bila kificho mawaziri wakuu wengi wa hivi karibuni wanatoka kwenye hii taasisi ya usalama, EDWARD LOWASSA ni mwana usalama mpaka kufa kwake, licha ya kuwa mwanasiasa kamwe hatodiriki kuanika hadharani baadhi ya masuala ya serikali tofauti na wanasiasa kama akina Mbowe.

2. Kuwa waziri wa mambo ya nje lazima uwe mwanadiplomasia kutoka usalama wa taifa,
hili lipo wazi waziri wa hiyo wizara mpaka sasa ni mwanausalama,

3. Kuwa jaji mkuu lazima uwe unatoka kwenye taasisi ya usalama wa taifa, hili halipingiki kwani nguvu na ufuatiliaji anaopaswa kuwa nao jaji lazima ujikite katika uweledi wa kiusalama na upelelezi yaani intelijensia.

4. Ili uwe rais lazima uidhinishwe na usalama wa taifa,
Hili litapingwa na wengi sana wasio na mwanga juu ya nguvu ya usalama wa taifa, wanasiasa wanapofikia hatua ya kuwania kiti hiki hawaachwi peke yao kufanya watakavyo katika mapendekezo na teuzi zao, ni hii taasisi hujipenyeza na kushauri yupi ni mtu/watu wafaao kuwania nafasi hii, kiukweli ni wazi hapa Tanzania chama tawala ndio kiko chini ya udhibiti wa taasisi hii kwani imekuwa kama desturi kwa chama kupitisha mgombea na kushinda chaguzi,
pia wagombea waliopitishwa na taasisi hii huanza kupewa ulinzi wa usalama wa taifa moja kwa moja, rejea kampeni za 2015.
tiss na magu.JPG

kwa wale wanaofahamu moja ya walinzi wa rais, huyo jamaa mwenye shati la draft na kofia ya CCM ni wa usalama na tayari alikuwa anamlinda mgombea wa urais kabla hata ya kushinda, kwanini? kwa sababu tayari alikuwa ameidhinishwa na TISS.
nguvu ya usalama wa taifa ni pana na ina maamuzi zaidi ya mienendo ya kisiasa na mihimili mingine.
Nb. NILIYOELEZA YACHUKULIWE KAMA SEHEMU YA KUJIFUNZA NA SI VINGINEVYO.
 
Hili linajulikana mbona? Na lipo wazi kabisa.

Ila nnachoshangaa kwa hao wana usalama, inamana hawaoni mambo yanayoendekea Tanzania?

Wanafurahia kwa sababu wao wanakula na kulala bure?

Rais anatoa hotuba za hovyohovyo na wao wapo kimya tu..
 
Hili linajulikana mbona? Na lipo wazi kabisa.

Ila nnachoshangaa kwa hao wana usalama, inamana hawaoni mambo yanayoendekea Tanzania?

Wanafurahia kwa sababu wao wanakula na kulala bure?

Rais anatoa hotuba za hovyohovyo na wao wapo kimya tu..
Kuna wazee hawapendi kupokea ushauri wa watoto wao, wanaamini wao ni wao!
 
Hili linajulikana mbona? Na lipo wazi kabisa.

Ila nnachoshangaa kwa hao wana usalama, inamana hawaoni mambo yanayoendekea Tanzania?

Wanafurahia kwa sababu wao wanakula na kulala bure?

Rais anatoa hotuba za hovyohovyo na wao wapo kimya tu..
mkuu rais hawezi kudhibitiwa na idara hii japo ndio idara inayomuweka kitini
 
Back
Top Bottom