Nguvu ya sifuri

Zeni2017

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Posts
1,247
Reaction score
534
Milioni tano ukiongeza sifuri ni milioni 50.

Watu milioni tano wakilipa kodi ya mji sh 10 kwa mwezi ni milioni 50.


Je wakilipa mia kwa mwezi? Watafikisha milioni 500.

Milioni mia tano kwa mwezi walimu na manesi watakosa mishahara ya maana? Miji itaacha kusafishwa? Maji ni miradi mingine itasubiri misaada ya nje?

Hivi ndio vitu vya kufikiriwa na wabunge. Lakini wengi wao wamesahau wajibu wao wamejikita kwenye kugombea urais.

 
Nina mfano hai. Tarafa (county)ninayokaa tunalipia kodi za tarafa. Mambo shwari unaweza kusahau kufunga vioo vya gari wiki mbili bila ya gari lako kuguswa na kibaka yeyote.

Inasikitisha viongozi wetu wanachoiga kutoka Marekani ni kuzozana na raisi tu.

Kwa Marekani raisi anatukanwa kwa sababu watu hawamuhitaji wana serikali za mitaa zinamaliza shida zao zote.
 
cha kujiuliza hapo ni hiyo million mia tano inakabidhiwa kwa mtanzania gani asiye dokoa hata buku
 
Tulitegemea watu watokwe mapovu kwenye mambo ya kujenga kama haya,lakini badala yake duh.

Ndio maana huwa nadharau hata usomi wa watu sometimes.

Yaani tukiamua kila kaya yenye makazi itoe shilingi mia mbili kwa mwezi,kuna wastani wa watz 15mil piga hesabu hapo.
 
Hapo ni nguvu ya sifuri kivipi? hapo wamezidisha kwa kumi hizo figure, sio kuongeza sifuri, milioni tano ukiongeza sifuri ni milioni tano hiyohiyo,
na hilo cover uliloweka haliendani na topic yako
 
Hapo ni nguvu ya sifuri kivipi? hapo wamezidisha kwa kumi hizo figure, sio kuongeza sifuri, milioni tano ukiongeza sifuri ni milioni tano hiyohiyo,
na hilo cover uliloweka haliendani na topic yako

Katika ubora wako. Kuna watu wengi wanaoacha maudhui ya topiki na kutafuta cha kuanzia ubishi? By the way umesoma hicho kitabu?
 
Katika ubora wako. Kuna watu wengi wanaoacha maudhui ya topiki na kutafuta cha kuanzia ubishi? By the way umesoma hicho kitabu?
Nimeacha maudhui gani sasa, mbona nimekufafanulia kabisa, hapo unachosema ni kutoza watu ushuru kwa mara 10 zaidi jambo ambalo hawatalichukulia poa hata kidogo
 
Nimeacha maudhui gani sasa, mbona nimekufafanulia kabisa, hapo unachosema ni kutoza watu ushuru kwa mara 10 zaidi jambo ambalo hawatalichukulia poa hata kidogo

Unafikiri sikulijua hilo. Actually nililiacha open kama sucker punch kwa wabishi watakaomisi point wajadili sifuri zimekaaje.
 
Nimeacha maudhui gani sasa, mbona nimekufafanulia kabisa, hapo unachosema ni kutoza watu ushuru kwa mara 10 zaidi jambo ambalo hawatalichukulia poa hata kidogo

Yaani kuna mwananchi Dar atagoma kulipa kodi ya sh 100 kwa mwezi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…