Nguvu ya mitandao: Wangekuwa CHADEMA ndio wanaandaa karibu viongozi wote leo wangekuwa mahabusu

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
FB_IMG_1520766334400.jpg

Wanachekaaaaa wanavyoona serikali inapelekwa puta na Mange.

Serikali iko kwenye dilemma haijui ivamie ofisi ipi imuhoji nani kuhusu maandamano imebaki kutisha yeyote anayejitokeza na kufoka kijumla jumla tu hasira zinaishia kwa wananchi wanaofungua karatasi katikati ya hotuba hakuna specific group ambalo wanali target, hawajui waandamanaji watapitia njia zipi ili wawapange FFU, wala watu watakusanyika wapi.

Wangekuwa Chadema ndio wameandaa nafikiri leo kama sio Kamati Kuu yote ya Chadema kuwa lockup basi viongozi wengi wangekuwa ICU wanapumulia mashine.

Hii ndiyo inaitwa "nguvu ya mitandao" + "nguvu ya umma" watu wamesambaa dunia nzima wanajadili na kupanga tukio moja, inawezekana wapangaji wako ulaya au humu humu nchini, hata ukiwajua wako wapi ni vigumu sana kuwakuta pamoja na kuwakamata tofauti na chama cha siasa ambacho ofisi zao na viongozi wao wanajulikana.

Waliko wanatamani waizime kitu ambacho ni ngumu sana kwa wakati huu wa utandawazi.
 
Back
Top Bottom