Viongozi wote wa juu BAWACHA ''Wamenunuliwa'' au ni tatizo ndani ya CHADEMA?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Kama tukikubaliana na hoja ya ''kununuliwa'' ambapo viongozi wote wa Juu wa Balaza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) wanaweza ''kununuliwa'' basi kuna tatizo kubwa nala msingi ndani ya chama ambacho kwa sasa kingekuwa ni chama kilichokabidhiwa mali za Taifa zima wazilinde na kuziendeleza kama chama tawala!

Hawa sio viongozi ambao wameanza uongozi mwaka huu bali kuna wengine wamekuwa wabunge na Mawaziri vivuli katika Wizara mbali mbali kwa zaidi ya miaka 10. Kwa lugha nyingine kwa sasa wangekuwa ni Mawaziri katika serikali ya CHADEMA.

Kwa vyovyote vile utakavyoweka lakini huwezi kupuuza ukweli kuwa hawa viongozi ni wajumbe wa kikao muhimu na cha juu cha CHADEMA(Kamati Kuu) ambacho kinapanga mikakati ya kisiasa lakini pia ni viongozi waliokuwa wanaaminiwa sana ndani na nje ya chama mpaka wengine wakaitwa ''Iron Lady'' kutokana na misimamo yao ''isiyoyumba''.

Zamani tulikuwa tunaona kiongozi mmoja au wawili ndani ya CHADEMA wakituhumiwa ''kununuliwa/kusaliti'' lakini hili la uongozi wote wa jumuiya ''kununuliwa/kusaliti'' limevunja rekodi. Hii inatupa ujumbe kuwa kila kiongozi ndani ya CHADEMA ana bei na ukitaka ''kumnunua'' unamnunua!

Hili tukio limetoa maswali mengi kuhusu uaminifu wa viongozi wa CHADEMA sio ndani ya chadema peke yake bali kwa taifa.

Kama tukikubali hoja ya kuwa ''hawajanunuliwa'' bali wamefanya tu kinyume na maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu. Hili nalo pia lina uweka uongozi wa juu wa CHADEMA katika maswali mengi kuhusu suala zima la uongozi ndani ya chama.

Huwezi kuwa na wajumbe wa Kamati Kuu wazoefu zaidi ya watano wanafanya maamuzi makubwa kama haya bila ''ruhusa'' ya Kamati Kuu.

Hawa sio kwamba wameibuka tu siku moja na kumaliza kila kitu. Ni lazima Kamati Kuu yote ilikuwa inajua kinachoendelea lakini inawezekana baadhi ya wajumbe hawakujua kilichokuwa kinaendelea kwa undani zaidi.

Hoja za msingi;
Je, Mwenyekiti wa Taifa alijua kinachoendelea na kama alijua alichukua hatua gani kabla ya tukio halijafikia lilipofikia?
Je, ofisi ya Mtendaji Mkuu wa chama(Katibu Mkuu) ilijua kinachoendelea na kama ilijua ilichukua uamuzi gani?

Kama ofisi za Mwenyekiti wa Taifa na Katibu wa Taifa hawakujua kinachoendelea basi viongozi wake watakuwa hawajui kazi zao kitu ambacho naamini sivyo kutokana na uzoefu wao kisiasa nchini.

Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa uongozi wote wa Juu wa Balaza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA) ndio ulioapishwa kuwa wabunge wa viti maalum ''bila ridhaa'' ya vikao vya CHADEMA.

Viongozi wa BAWACHA kitaifa wanaotuhumiwa ambao wameapishwa kuwa wabunge wa viti maalum ni hawa:-

1) Mwenyekiti wa BAWACHA - Halima Mdee.
2) Makamu Mwenyekiti wa BAWACHA - Hawa Subira Mwaifunga
3) Katibu Mkuu wa BAWACHA - Grace Tendega
4) Naibu Katibu Mkuu BAWACHA (Bara) - Jesca Kishoa
5) Naibu Katibu Mkuu BAWACHA (Zanzibar) - Asia Mwadin Mohamed.
6) Katibu Mwenezi BAWACHA - Agnesta Lambat Kaiza

Hata Balaza la vijana (BAVICHA) nalo halikukosa kiongozi katika kundi hilo, Katibu wake Mkuu wa BAVICHA, Nusrat Hanje pia aliapishwa.

Hawa ni wajumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA wanaoingia kwenye vikao kwa sababu ya vyeo vyao.

Wamo pia wengine katika kundi hilo la Ujumbe wa Kamati Kuu ambao waliapishwa;
1) Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Serengeti na Mjumbe wa Kamati Kuu - Esther Matiko
2) Ester Bulaya

Wamo pia viongozi wa mikoa ikiwamo:-
1) Mwenyekiti wa Chadema Mkoani Mtwara - Tunza Malapo.
 
CDM ikishika dola,unadhani ni nani atakuwa mgumu huko CCM kununuliwa?Inaweza kununuliwa kamati kuu nzima ya CCM!

*Unaanza mbinyo kwa CCM,yaani wanapitishwa kwenye tanuru la moto!Wanakuwa watu wa mahakamani kila siku,na kesi zao za kuwabambikizia zinapigwa pini dhamana!Wakishateseka kama miaka 3 hivi.

*Unawapa ulaji baadhi yao,wakiangalia mateso na kile kilichoko mezani hakuna wa kuchomoa!

Tusiende mbali,CCM waliofisadi nchi hii kwa miaka nenda rudi,wamelitokea Chadema?
 
CDM ikishika dola,unadhani ni nani atakuwa mgumu huko CCM kununuliwa?Inaweza kununuliwa kamati kuu nzima ya CCM!
*Unaanza mbinyo kwa CCM,yaani wanapitishwa kwenye tanuru la moto!Wanakuwa watu wa mahakamani kila siku,na kesi zao za kuwabambikizia zinapigwa pini dhamana!Wakishateseka kama miaka 3 hivi-
*Unawapa ulaji baadhi yao,wakiangalia mateso na kile kilichoko mezani hakuna wa kuchomoa!

Tusiende mbali,CCM waliofisadi nchi hii kwa miaka nenda rudi,wamelitokea Chadema?
Kwa mtu mwenye fikra pana unajua unasema kuwa CHADEMA wananunuliwa kwa sababu hata CCM wangekuwa wapinzani wangenunuliwa!

Hili la kusema ''hata CCM wangekuwa wapinzani wangenunuliwa'' haliwezi kuwa ndio uhalali wa viongozi wa juu wa CHADEMA kununuliwa!

CHADEMA wanatakiwa wawe tofauti na CCM lakini kama wanajilinganisha na CCM wakati sio CCM inatoa picha kuwa uongozi wa CHADEMA una tatizo kubwa sana! tena Kubwa sana!

Fikiria vizuri!
 
Naunga mkono hoja yako Mkuu MsemajiUkweli kwa hoja zako.

Katika bandiko zinazohusu mgogoro wa uteuzi wa wabunge wa viti maalumu, nimeandika, na narejea tena kuwa tatizo siyo yaliyoandikwa kwenye Katiba ya CHADEMA ila ni uongozi wa juu wa chama kutokumkemea na kumchukulia hatua Mbowe, M/kiti wa chama. Lawama na madai ya viongozi wenzake dhidi yake, sina uhakika kama huongelewa kwenye vikao vya ndani. Hayo tunayasikia nje ya chama kutoka kwa viongozi wanaokihama chama.

Najiuliza, je, huko ndani ya chama kuna viongozi jasiri wa kumhoji Mbowe, M/kiti, kwa jinsi ile ile wanavyomhoji na kumkebehi Rais wa JMT, ambaye pia ni M/kiti wa CCM, chama tawala?

Tusubiri matokeo ya kikao cha Kamati ya Maadili ya Kamati Kuu ya Chama ambayo inakaa leo kujadili sakata hilo.
 
Lissu yeye amenunuliwa na mabeberu ametulia Ubelgiji swaaaafi halafu anataka wenzie wafe njaa huku 😂...
Lissu akianza kupitisha pesa za wafadhili kwenye chama ndio watakuwa na maelewano na Mbowe, kwa sasa kila mtu apambaniye tumbo lake.
 
Kwa mtu mwenye fikra pana unajua unasema kuwa CHADEMA wananunuliwa kwa sababu hata CCM wangekuwa wapinzani wangenunuliwa!

Hili la kusema ''hata CCM wangekuwa wapinzani wangenunuliwa'' haliwezi kuwa ndio uhalali wa viongozi wa juu wa CHADEMA kununuliwa!

CHADEMA wanatakiwa wawe tofauti na CCM lakini kama wanajilinganisha na CCM wakati sio CCM inatoa picha kuwa uongozi wa CHADEMA una tatizo kubwa sana! tena Kubwa sana!

Fikiria vizuri!
Ndio maana tumetoa ushauri kuwa waliosaliti chama wafukuzwe japo tunaweza kuelewa angle yao ya kukubali kwenda kuapa!Mtu kamaNusrat Hanje,amekaa gerezani zaidi ya miezi minne,mara pap deal mezani hilo hapo,uachiwe na ukubali kwenda kuwa mbunge!Kwa hali ya kibinadamu lazima ukubali!

Hao wote nashauri wafukuzwe,ila Nusrat apeww adhabu ndogo maana mazingira yake ni magumu,jela sio mchezo!

Nilichosema hapo juu ni kuwa ukandamizaji wa haki ndio umepelekea kugawanyika na makundi ndani ya upinzani!Kila binadamu ana kipimo chake cha uvumilivu,wengine wameona isiwe taabu,wameteseka sana wacha wamalizie miaka mitano kwa pesa nono.

Either way,serikali na bunge vimejidhalilisha sana kushiriki kuvunja katiba ya nchi na sheria kwa kuingilia maamuzi ya ndani ya chama na kuamua mambo ya chama kwa niaba ya chama!Huu ni uhuni mkubwa ambao hatujawahi kuuona toka vyama vingi vianze mchini!
 
Tatizo ndani ya Chadema ndio lisababishe Ndugai awe mtetezi wao?

Hao viongozi uliowataja (Mwenyekiti na Katibu) umewageuza malaika wajue mipango miovu iliyokuwa inapangwa kwenye korido za Lumumba? au kwa njia ya simu?

Inavyoonekana hapo huwezi kuwatoa CCM kwenye huo mchezo, hasa suala la Nusrat Hanje kutolewa gerezani usiku na kuwahishwa Dodoma.

Kama kuna viongozi wa Chadema waliohusika, watakuwa viongozi wa pembeni wasio na mamlaka na hilo suala (hapa inatajwa ofisi ya Salum Mwalim) kwamba yeye ndie ameratibu huo mpango muovu akishirikiana na Kigaila( ambao wote wawili inasemekana wana mahusiano ya kimapenzi) na baadhi ya hao waliokwenda kuapishwa). Japo hili sina hakika nalo 100%

Hivyo kinachoonekana hapa, kuna viongozi wa CCM waliohusika kuwashawishi hao viongozi wa Chadema wakiwemo wabunge waliokwenda kuapishwa bungeni, hili halina shaka ndio maana Ndugai ameshaanza kutoa kauli za kujichanganya.

Vyema Chadema kama chama Kamati Kuu itapoketi, wafukue vizuri chanzo cha hilo tatizo na kuwaadhibu wote waliohusika, hata kama kwasasa hatuwasikii wakitajwa.
 
Wafukuzwe wote tuone mwanasheria mkuu wa serikali atafanya nini...watu wazima usiwatishie nyau
 
Back
Top Bottom