Nguvu ya Biashara ya Forex, Ujasusi na yaliyo nyuma ya pazia

:D:DYana nikishamuona mtu anayemsifia mtu na kuweka neno IQ namuona limbukeni sana
Maana yake wewe huamini habari ya IQ au nini. Hebu dadavua maana kwa IQ level ya Francis da don huwezi kumfananisha na magenious wengine. Yeye yuko juu sana
 
Ni kweli mkuu, unabusara sana!

Hata wakulima wanapolima wakisubiri mvua ambayo inaweza kunyesha au isinyeshe pia wanacheza kamari.

Na hawa wanaotengeneza bidhaa mbali mbali ambazo hawana uhakika kama zitanunuliwa au hazitanunuliwa pia wanacheza kamari.

Bila kusahau maombi tunayoomba kanisani na misikitini bila kujua Mungu amepanga nini pia ni kamari.

You are very smart!

 
...ukinunua nyumba na kuuza kwa bei ya juu hapo umecheza kamari mkuu hakuna uzalishaji mali mkuu...uzalishaji mali labda ujenge kiwanda cha kutengeneza juisi hapo ndio kuna kitu kimezalisha....lakini biashara za kununua na kuuza hakuna uzalishaji wowote hapo
Ndio maana tunasema uzalishaji 'Mali' au 'Huduma', sio mali peke yake. Akinunua nyumba na kuiuza baadae ni ametoa 'Huduma'ya 'Real estate agency'.
 
Achana naye huyo hajui kitu. Kama hajaelewa, usitumie nguvu kubwa kumwelimisha. Atakuja kushtuka baadae wakati tulioanza tuko mbali. Mfano TMT session ya kwanza ya dsm, huwezi linganisha ki mafanikio na TMT ya last session ya Mwanza. Tuko tofauti.

Siku akigundua ukweli, atabadili gia angani na kusema alikuwa anabisha ili hoja zitolewe aelewe.

Mtake aingie darasani huyo, sessions zimeanza.

Tangu saa tisa usiku wa leo, nomepandisha akaunt yangu kwa faida hii hapa, na bado naangalia fursa zaidi.

Eti dola 19 kwa pesa ya kibongo ni shiling ngapi?

be1cf76d4e5125fc2228e71e6700265f.jpg
Nakuonea huruma, shuhuda kama za wale foreverliving hizi
 
mkuu sorry jana tulitofautiana kimtazamo juu ya hii insu,hapo hapo baada ya jibu lako nikaikumbuka kauli ya Mwl wangu chuoni alipokuwa antufundisha mambo ya monetary economics kuwa hakuna bishara duniani ambayo unaweza kuifanya bila kudhurumu mtu ila ni forex pekee ndipo leo nilipokuwa ofisini niliamua kwenda chimbo kidogo kuhusiana na hii kitu kwa kweli nikiri forex sio kamali ila ukitazama kwa juu juu pasipo kuwa na knowledge na concepts za kiuchumi unaweza kusema ni kamari but ni vitu viwili tofauti
Lete hoja ya kwanini si kamari
 
BLACK WEDNESDAY: NGUVU YA BIASHARA YA FOREX, UJASUSI NA YALIYO NYUMA YA PAZIA

de483a8db03b3e42aa7355d44dbe9ac3.gif


SEHEMU YA TANO


"…uwekezaji unahitaji subira. Ni kama vile kupaka rangi nyumba na kusubiri ikauke. Au kupanda mmea na kuusubiri ukue. Kama wewe ni mtu mwenye kupenda furaha ya haraka haraka chukua elfu kumi yako nenda 'coco beach'.!"


- The Bold, 2018



'Dili' ya Karne

Katika sehemu iliyopita nilieleza namna ambavyo George Soros alianza kutengeneza position yenye thamani ya zaidi ya bilioni 10 za Marekani. Lakini pia tuliangalia kwa mapana maana ya 'short sell' katika soko la hisa na soko la fedha duniani.

Katika sehemu hii ya tano twende taratibu hatua kwa hatua tuone namna amnavyo George Soros alishort Paundi ya Uingereza na kuifilisi benki Kuu.

Karibu…

Usiku wa kuamkia tarehe 16 Septemba 1992 wakati ambao ulimwengu mzima umelala George Soros kupitia Quatumn Fund alikuwa anaazima na kuuza Paundi ya Uingereza kuzidi katika kiwango kikubwa na cha kutisha. Alikuwa anaazima kutoka kwa kila benki na mashirika makubwa ambayo yalikuwa tayari kumpatia.
Naamini mpaka sasa wote tunaelewa kwa upana maana ya short sell na hivyo tunaelewa kwa nini Soros alikuwa anaazima na kuiuza Paundi.

Katika ulimwengu wa masoko ya fedha duniani, wafanyabiashara wa fedha wana tabia kama mbwa mwitu. 'Hawalali' muda wote wakiwinda fursa za kuuza au kununua sarafu fulani.
Kwa hiyo kitendo hiki cha George Soros kuuza kwa kasi Paundi na kwa kiwango kikubwa mawimbi yake yaliwafikia pia Hedge Funfmds nyingine na wafanyabiashara wengine wa soko la fedha. Japokuwa kama nilivyoeleza huko awali kwamba katika kipindi hiki Soros bado hakuwa Bilionea maarufu kama tumjuavyo sasa lakini wafanyabiashara wengi wa soko la fedha walikiwa wanamfahamu yeye na kampuni yake na walifahamu na kuheshimu umahiri wake hasa hasa kwenye uchambuzi wa masoko ya Ulaya.

Hivyo basi baada ya kusikia kuwa George Soros alikuwa akiazima Paundi kwa kiwango kikubwa na kuziuza, karibia soko lote la fedha duniani likaanza kuuza Paundi ya Uingereza.

Mpaka kufikia muda ambao London Market inafunguliwa mida ya asubuhi, maafisa wa serikali waliianza siku kwa kushuhudia mabilioni ya Paundi yakiwa yameuzwa tayari. Kama ambavyo nilieleza kuwa sarafu fulani ikiwa inauzwa sana thamani yake kwenye soko inashuka. Ikinunuliwa sana, thamani yake inapanda.
Kwa hiyo kitendo cha Paundi kuwa inauzwa sana kilisababisha kuwe na presha ya kuitaka thamani yake ishuke. Kilichokuwa kinasaidia pekee ni ile hali ya serikali kuzingatia sharti kwamba Paundi isiuzwe chini ya 2.78 DM.

Lakini kitendo cha serikali kung'ang'ana kwamba thamani ya Paundi ibaki pale pale kilikuwa kinaumiza zaidi sarafu yao. Hakuna mfanyabiashara wa fedha ambaye alikuwa tayari kuinunua kwa thamani hiyo huku akijua fika kwamba kuna mabilioni kwa mabilioni ya Paundi yanauzwa na hii ikiashiria kwamba thamani ya Paundi inaelekea kuporomoka kwa kasi ya radi.

Kwa hiyo kulikuwa na njia mbili za kuhakikisha kwamba thamani ya Paundi inabaki juu. Njia ya kwanza ilikuwa ni kuhakikisha inaanza tena kununuliwa kwa kiwango kikubwa. Na njia ya Pili ilikuwa ni kuanza kucheza na Interest Rates.
Njia zote mbili hizi zilikuwa na changamoto zake.
Njia ya kwanza ya kuhakikisha inaanza tena kununuliwa ilikuwa haiwezekani kwa maana ya kwamba wafanyabiashara wakubwa wote walikuwa wanafuata kile ambacho Soros alikuwa anakifanya. Walikuwa wanauza kila Paundi waliyonayo na ile ambayo waliweza kuazima.
Njia ya Pili ya kuongeza Interest Rates ilikuwa ni hatari zaidi kwa kuwa nchi ilikuwa imetoka kwenye mdororo wa kiuchumi, kwa hiyo walihitaji kuhakikisha kuna spending kubwa kwa wananchi ili uchumi uendelee kuchangamka.


Ndio hapa inaturejesha tena kwenye kikao cha Waziri Mkuu John Mayor na wasaidizi wake nyumbani kwake Whitehall siku hiyo hiyo ya Septemba 16, 1992.


Nyumbani kwa Waziri Mkuu

Hali ya kikao ilikuwa tete kweli kweli. Wanasema siku ya kufa nyami miti yote inateleza. Ndicho ambacho kilikuwa kinawakuta serikali ya Uingereza. Kila suluhisho ambalo walikuwa wanalijadili na kulipendekeza lilikuwa haliwezekani kiutekelezaji.
Ndipo hapa wakafikia uamuzi ambao walikuja kuujutia baadae.

Kwa kuwa hakukuwa na mfanyabiashara mkubwa au shirika lolote la fedha au mabenki ambao walikuwa tayari kununua Paundi ya Uingereza (kila mtu alikuwa anauza) serikali ya Uingereza ikafikia uamuzi kwamba wao wenyewe kama serikali waanze kuinunua Paundi.
Kitu ambacho nataka ukumbuke ni kwamba, unaponunua sarafu fulani maana yake ni kwamba unatoa/unauza sarafu nyingine. Yaani kwa mfano ukisema unataka kununua sarafu ya kitanzania yenye thamani ya bilioni moja. Maana yake unatakiwa utumia mfano dola kama laki nne na nusu hivi kuinunua bilioni moja ya kitanzania. Ndio hapa tinasema unakuwa umenunua shilingi na umeuza dola.

Kwa hiyo kitendo cha serikali ya Uingereza kufikia uamuzi wa kutaka kuanza kuinunua Paundi maana yake ni kwamba walikuwa wanatumia akiba yao ya fedha za kigeni (Foreign Reserve) kuinusuru Paundi. Kama ikitokea George Soros akashinda vita hii maana yale ni kwamba watapata hasara mara mbili, sarafu yao kushuka thamani na watakuwa wamepoteza kiwango kikubwa cha akiba ya fedha za kigeni.

Mida ya saa 8:40 AM serikali ya walijibu mapigo ya Soros kwa kununua Paundi Bilioni moja!

Ajabu ni kwamba hakukuwa na muitikio wowote ule chanya katika soko. Bado watu waliendelea kuuza Paundi kwa kasi ya radi.

Ndipo hapa ambapo serikali ya Uingereza ikaanza mchezo mchafu wa propaganda.
Waziri wa Fedha wa Uingereza Bw. Norman Lamont akafanya kikao na waandishi wa habari na kueleza kwamba kuna mfanyabiashara (George Soros) ambaye alikuwa amedhamiria kuubomoa uchumi wa Uingereza. Waziri Lamont akajiapiza kwamba watatumia misuli yao yote kupambana na 'dhalimu' huyo ili kutetea uchumi wa Uingereza na akaweka hadharani mpango wa Serikali kutumia dola bilioni 15 kuitetea Paundi.

Kwa wale ambao wanafanya biashara ya Forex nadhani wanajua ni kwa kiasi gani ambavyo 'News' zinaathiri soko la fedha. Leo hii Trump hata akitweet tu tayari kwenye soko utaona athari zake. Ukisikia Mario Draghi, Rais wa Benki ya Ulaya anaongea na kama unahold 'pair' fulani yenye Euro ndani yake basi presha inakupanda. Ukisikia mwanamama Janet Yellen, Mwenyekiti wa Federal Reserve ya Marekani ana mkutano na waandishi wa habari alafu wewe unaifanyia biashara pair yenye USD ndani yake unaweza kuzimia. Ni kwa sababu hicho kitakachoongelewa eidha kitakupa faida ambayo itakufanya utabasamu mpaka koromeo lidondoke au habari hiyo itakupa kilio cha uchungu kufanana na msiba.
Binafsi naweza kusema katiba biashara ya fedha (forex) News ndio factor kubwa zaidi inayoamua uelekeo wa thamani ya sarafu. Na factor ya pili ni kubwa ni 'market markers' (hawa tutawaongelea huko mbele saikolojia yao na namna wanavyocheza na masoko ya fedha).

Kwa hiyo mkutano huu na vyombo vya habari ulilenga mambo mawili. Moja ni kutaka kuingiza hali ya uzalendo kwa mabenki ya Uingereza kuitetea Paundi ili kupambana na 'dhalimu' wa kimarekani ambaye anataka kuuzamisha uchumi wa Uingereza, na pili ni kujaribu kuiokoa Paundi kwa factor ya 'positive news' (nadhiri ya kutumia dola bilioni 15 kuitetea Paundi) maana yake thamani ya Paundi iende juu.

cd0ced9f8c8bb59fad15983e74e6777b.jpg

George Soros na Girlfriend wake Adrianna Ferreyr mcheza sinema kutoka Brazil


George Soros anajulikana kwa namna ambavyo yuko 'notorious' kwenye kutake risk za kibiashara.
Baada ya kusikia kuwa serikali ya Uingereza wanatumia dola bilioni 15 ya akiba yao ya fedha ya kigeni kuitetea Paundi, naye akaongeza position yake kutoka dola bilioni 10 mpaka dola bilioni 15.

Kwa hiyo kile kikao cha Waziri Lamont na waandishi wa habari pamoja na nadhiri ya kutumia dola bilioni 15 kuitetea dola haikuwa na matokeo yoyote chanya kwenye soko. Paundi iliendelea kuuzwa kwa kasi na kwa kiwango kikubwa katika soko la fedha la dunia.

Serikali ya Uingereza hawakuishia hapo tu. Japo walitangaza kutumia dola bilioni 15 kuitetea Paundi lakini walijikuta wanatumia fedha za kigeni zenye thamani ya Puandi bilioni 27 kuinunua Paundi.

Lakini misuli ya Soros ilionekana ngangari zaidi yao. Ulimwengu ulikuwa na imani zaidi na Soros kuzidi serikali ya Uingereza. Soros aliendelea kuhold position yake dhidi ya Puandi na ulimwengu mzima wa soko la fedha ulikuwa nyuma yake kwa kuendelea kuiuza Puandi kwa mabilioni na mabilioni.

Serikali ya Uingereza ilishikwa na kiwewe zaidi.

Kila mti ulikuwa unateleza.

Mbele yao walikiwa na silaha moja ya mwisho… Interest Rates.

Saa 9:00 AM Waziri wa fedha wa Uingereza wa kipindi hicho, Norman Lamont akampigia simu Waziri Mkuu John Mayor akiwa na pendekezo la mwisho la kuinusuru Puandi. Kwamba waongeze Interest Rates.
Naamini tunakumbuka nilivyofafanua namna gani ukiongeza interest rates thamani ya sarafu yako inapanda kwa kuwa wafanyabiashara na mabenki watainunua ili waiuze kwa faida hiyo ya juu.
Lakini kwa mazingira ambayo Uingereza walikuwa wanapitia ilikuwa ni wendawazimu kuongeza Interest Rates. Nilieleza kwamba nchi ikiwa kwenye mdororo wa kiuchumi unapaswa kushusha interest rates ili kuchochea spending na mzunguko wa fedha. Na ikumbukwe kwamba ukiongeza interest rates watakaonufaika moja kwa moja ni wafanyabiashara ya fedha na mabenki na sio mwananchi wa kawaida. Lakini pia kama wangelifanya hivi kulikuwa na tishio la kuurejesha uchumi wa Uingereza kwenye mdororo ambao wametoka mwaka mmoja tu uliopita.

Kwa hiyo pendekexo hili la Waziri Lamont ilikuwa ni wendawazimu katika viwango vyote.
Lakini uwendawazimu huu ndio ilikuwa silaha yao pekee ambayo ilikuwa imebakia.

Mara hii ya kwanza saa tatu asubuhi Waziri Mkuu John Mayor alikataa katakata kuongeza Interest Rates.

Kwenye soko la dunia Paundi ilikuwa inauzwa kwa kasi zaidi.

Saa 10:00 AM Waziri wa Fedha Norman Lamont alipiga tena simu kwa Waziri Mkuu akimuomba akubali ombi lake la kuongeza Interest Rates. Waziri Mkuu John Mayor akakataa kwa mara nyingine.

Paundi ikaendelea kuuzwa zaidi kwenye soko la Dunia.

Saa 11:00 AM Lamont akapiga tena simu kwa Waziri Mkuu. Safari hii akimtaka Waziri Mkuu amwambie wafanye nini? Waziri Mkuu hakuwa na jawabu… wala hakuna mtu yeyote kwenye serikali ya Uingereza ambaye alikuwa na jawabu. Silaha pekee ambayo walibakiwa nayo ilikuwa ni Interest Rates.
Hivyo basi saa 11:30 AM Waziri Mkuu John Mayor alikubali ombi la Waziri wa Fedha kuongeza Interest Rates.

Kwa hiyo majira ya saa sita kasoro mchana, serikali ya Uingereza ilitangaza kuongeza Interest Rates kwa basis points 200… yaani kutoka 10% mpaka 12%.

Ilikuwa ni 'dili' nono ambayo ingewatoa mate wafanyabiashara wote wa fedha duniani. Lakini watu katika ulimwengu wa fedha walikuwa wanamuangalia Soros atafanya nini.
"Don't bite!" Ndilo jibu pekee ambalo Soros aliwajibu wafanyabiashara wenzake na mabenki ambao mate yaliaanza kuwatoka kutokana na kuongezwa kwa interest rates. Aliwaonya kwamba 'meli' inaelekea kuzama. Wasijitumbukize wakazama nayo.

6c9b5a857e54582c7393a3b054a884cc.jpg

Waziri Norman Lamont akiwa na mentee wake, David Cameroon kipindi akiwa kijana


Bundi aliendelea kulia mlangoni kwa serikali ya Uingereza… ulimwengu uliendelea kuuza Paundi kwa kasi. Licha ya kuongeza interest rates bado watu walikuwa na imani na kile ambacho Soros alikuwa anakiona akilini mwake. Anguko la Paundi la Kihistoria.

Ndipo hapa ambapo serikali ya Uingereza ikafanya jambo lingine la uwendawazimu zaidi.
Majira ya saa 04:00 PM Waziri Lamont alielekea nyumbani kwa Waziri Mkuu John Mayor maeneo ya Whitehall kuungana na wengine walioko huko kufanya mjadala nini zaidi kifanyike kuinusuru Paundi.
Baada ya majadiliano ya masaa kadhaa wakatoka na moja ya uamuzi wa ajabu zaidi kiuchumi kuwahi kufanyika.

Serikali ya Uingereza ikatangaza tena kuongeza Interesf Rates kutoka ile 12% waliyoongeza awali mpaka 15%..!!!

Ilikuwa ni ajabu kweli kweli hasa ukizingatia hali tete ya kiuchumi ambayo Uingereza walikuwa nayo kipindi hicho.
Naomba ieleweke kwamba mfano sasa hivi, serikali nyingi ulimwenguni huwa wanatangaza viwango vipya vya interest rates maro moja kwa mwezi. Kwa hiyo kitendo cha serikali ya Uingereza kutangaza interest rates na kuzipandisha mara mbili ndani ya siku moja kilikuwa ni kitu cha ajabu kuzidi maelezo ninayoweza kuyatoa.

Mabenki na wafanyabiashara wengi mate yalianza kuwatoka. Lakini macho yao yalikuwa kwa Soros. Atafanya nini?
Soros alikuwa na jibu moja tu… kwamba serikali ya Uingereza ilikuwa 'desperate'! Wanachokifanya si jambo la kawaida kiuchumi, na hii inaonyesha ni kiasi gani ambavyo walikuwa desperate na hawana mbinu yoyote waliyobakiwa nayo kuinusuru Paundi. Hii maana yake ni kwamba walikuwa wanaelekea kusalimu amri na kupiga magoti. Walikuwa wanapaparika kama kuku anayekata roho. Hawakuwa na ujanja. Walikuwa wamewashika 'sehemu nyeti' na muda si mwingi watasalimu amri.

Kwa hiyo Soros akawahamasisha wenzake… "sell it!! Sell it as much as you can get!! Sell the GBP! Sell it against any other currency… Sell it against the US Dollar, Sell it against AUD, sell CAD, sell it against chinese Yen, sell it against Korean Won… just sell it as much as you can and by the time we go to sleep today we will have a fortune.."

Paundi iliuzwa kama njugu kwenye soko la fedha la dunia. Kwa mabilioni na mabilioni zaidi. Na kwa kasi ambayo haijawahi kutokea.

Serikali ya Uingereza hawakuwa na ujanja tena. Hawakuwa na silaha nyingine yoyote ile. Mafuriko ambayo walikuwa wameyazuia kwa mikono kwa siku nzima yalikuwa yamewazidi nguvu. Ulikuwa ni muda wa kupiga magoti, kuelekea kibla na kuchinjwa.

Muda wowote ulimwengu ulikuwa unatarajia serikali ya Uingereza kutangaza kushusha thamani ya Paundi na kujitoa kwenye mpango wa ERM.

Wanasema kwamba kama unaweza kuona 'aura' ya binadamu unaweza kujua kabla kifo akija mpata. Kwamba ukiangalia mfano picha ya mwisho ya marehemu Tupac, machoni mwake unaweza kukiona kifo kabisa. Unaweza kuona woga ambao anao. Unaweza kuona hofu ndani ya nafsi yake. Unaweza kuona kabisa kifo kikiwa kinamnyemelea.

Ndivyo ambavyo aura ya Waziri Norman Lamont ilivyokuwa alipoingia kwenye ukumbi wa mkutano na waandishi wa habari mida ya saa 07:30 PM.
Chumba chote kilikuwa kimya. Kelele cha kamera tu ambazo zilikuwa zinafotoa picha ndizo ambazo zilikuwa zinasikika. Waziri Lamont aliingia akiwa ameongozana na wasaidizi wake kadhaa pamoja na watu wa benki kuu na hazina. Wananchi wa Uingereza ambao walikuwa wanafuatilia mubashara mkutano huu wa Waziri na waandishi wa habari hofu ilikuwa imewajaa mioyoni mwao. Ni mwaka mmoja tu wametoka kwenye mdororo wa kiuchumi na leo hii kitakachotamkwa na Waziri kinaweza kuirudisha Uingereza kwenye mdororo kama ule au zaidi.

Lakini kwa upande wa Soros hii ulikuwa ni wakati ambao amekuwa anausubiri kwa zaidi ya miezi miwili tangu aanze kujenga position yake ya mabilioni dhidi ya Paundi. Na wakati huo ndio ulikuwa umewadia.
Yeye pamoja na vijana wake walikuwa wamejikusanya mbele ya runinga ofisini kwao New York wakifuatilia mubashara kabisa mkutano huu wa Waziri Lamont na wanahabari.

Wakati wa kujua mbivu na mbichi ulikuwa umewadia.



Stay here… narudi!


The Bold - 0718 096 811 (WhatsApp Only)
To Infinity and Beyond

Pls: Follow, subscribe and nifuate WhatsApp
 
Back
Top Bottom