Ngurumo: Ni kaburi la CCM au CHADEMA?

Ngurumo: Ni kaburi la CCM au CHADEMA?

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
13,104
Reaction score
5,665
NATAKA kusema neno moja. Ni hivi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitakufa. Lakini hakifi leo, wala hakitakufa kwa sababu ya kumvua vyeo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na wenzake.

Kitakufa siku moja kama vyama vingine vyote vitakavyokufa, kwa sababu kila kilichoanza kina mwisho wake.

Kitakufa wakati wake utakapowadia. Si sasa. Si leo. Na hakitakufa kabla Watanzania hawajashuhudia kifo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM). Niamini.

Zaidi ya hayo, hakitakufa kwa sababu ya makundi ya wana CCM wanaojipanga nchi nzima kuzomea, kuchochea mgororo, kutisha viongozi wa CHADEMA na kubeza uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho.

Badala yake, kwa kufanya uamuzi mgumu, kwa kugusa baadhi ya wanachama na viongozi wanaodhaniwa kuwa hawagusiki; kwa kufanya kile ambacho CCM wamekuwa wanashindwa kufanya, CHADEMA kimejiweka katika mazingira mapya ya kukua na kukomaa.

Kinaonyesha kuwa sasa kimekuwa taasisi. Walio tayari kufanya kazi kitaasisi wataendelea kufanya kazi. Waliojiunga na chama kufuata watu, wataondoka na watu hao. Waliofuata sera watabaki. Chama kitapona.

CCM ilipokuwa bado imara iliwahi kufanya uamuzi mgumu. Katika kutetea kile ambacho uongozi wa chama uliona ni msimamo wao kuhusu Muungano, chama kilimfukuza Makamu wa Rais, Aboud Jumbe na Waziri Kiongozi, Seif Shariff Hamad.
Uzito na ukweli wa hoja zao ni jambo moja; na msimamo wa chama ni jambo jingine. Chama kilitetea msimamo wake. Viongozi wakubwa wa ngazi hizo wakaanguka, chama kikapona.

CCM legelege ya sasa haiwezi kufukuza hata wale inaowatuhumu kwa makosa makubwa na kuwashambulia hadharani. Inawaogopa.

Ndiyo maana kelele za kuvua magamba zilipopamba moto, Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, alikejeli harakati za wenzake akisema, "gamba limekwama kiunoni. Mwenye uwezo wa kulivua aje na shoka."

Mwaka umepita sasa, gamba la Chenge limewashinda Rais Jakaya Kikwete, Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, na mashabiki wao.

Kwa hiyo haishangazi kwamba CHADEMA inapochukua hatua ndogo tu ya kubadilisha watu vyeo kwa sababu ya kukosa imani nao, wanaokerwa zaidi na hatua hiyo ni wana CCM.

Ndio wanaohaha nchi nzima wakitangaza kila kona "CHADEMA kinakufa, CHADEMA kinakufa." Kisa, eti Kamati Kuu imemvua Zitto vyeo. Kwani yeye alivipataje? Si wale wale waliompatia vyeo ndio wameamua kumwondolea vyeo hivyo?
Na tangu lini CCM wakawa na huruma kwa CHADEMA? Iweje leo ‘CHADEMA inakufa' halafu wanaoumia ni wana CCM?

Kwanini CCM wanasikitishwa na ‘kifo' cha CHADEMA? Kuna jambo. Wenye akili wameshaligundua.

Iweje wanaoandaa magenge ya kuzomea viongozi wa CHADEMA na kubeza uamuzi wa Kamati Kuu ni baadhi ya wanachama wa zamani wa CHADEMA waliokimbilia CCM?

Wanatuma ujumbe gani kwa Watanzania? Zaidi ya hayo, mbona hawa wamenyang'anywa vyeo tu, tayari propaganda za udini na ukabila ndo zinaibuka tena?

Ni dini gani inayoagiza kwamba cheo ni haki ya kuzaliwa ambayo mtu akishapewa hapaswi kunyang'anywa, hata ikithibitika kwamba wenzake hawana imani naye?

CCM na makapi yao sasa wanahaha nchi nzima kuhubiri udini na ukabila. Huu nimeuita ujinga. Ni ugonjwa wa akili. Ni kichaa kama vingine.

Hivi CHADEMA ilipovunja uongozi wa chama Mkoa wa Mwanza ilikuwa inatetea dini na makabila?

Ilipofukuza madiwani wanne Arusha ilikuwa inapambana na Uislamu? Ilipomvua cheo Samson Mwigamba na Dk. Kitila Mkumbo ilikuwa inajadili dini na makabila yao?

Ni lini tumeanza kuficha udhaifu wetu katika makabila yetu na imani zetu za kidini? Kwa faida ya nani?

Ndiyo! Ipo siku CHADEMA itakufa. Lakini kwa mbinu hizi za CCM ya sasa, CHADEMA itazidi kushamiri. Jipeni muda, mtaelewa maneno yangu.

Wanaotaka kutumia mwanya huu kudhoofisha chama hiki wanapoteza muda. Hawataweza. Chama kimeshawazidi nguvu. Kimewazidi kimo.

Nakumbuka miaka kama 15 iliyopita, wana CCM walikuwa wanamwaga sifa kwa CHADEMA, wakisema ni chama cha watu wastaarabu, hakina fujo wala migogoro. Walikiona ni chama cha wastaafu na mabepari wenye pesa ambao hawana papara.

Leo wanakiona ni chama chenye fujo. Wamefikia hatua ya kukizushia tuhuma za ugaidi. Sababu ni moja. Wakati ule, CHADEMA hakikuwa tishio kwa chama tawala.

Kilipewa sifa hizo kwa kuwa kilikuwa kinaonekana ni mateka wa mfumo unaotawala.
Kilikuwa chama kwa sababu tu kina usajili.

Lakini hakikuwa kinaonyesha dalili zozote za kutaka au kukaribia kushika dola. Ustaarabu wa CHADEMA wa enzi zile ilikuwa silaha ya nyongeza ya CCM.

Leo CHADEMA ndicho chama pekee kinachokua kwa kasi hapa nchini. Ndicho kinachotetemesha wakubwa katika mijadala bungeni.

Ndicho kinachoongoza mapambano ya wanyonge dhidi ya watawala. Ndilo tishio kuu la serikali ya sasa.

Kwa hali ya sasa ya kisiasa, katika kutapatapa kukubalika na kubaki madarakani, CCM inajua kuwa haitapata kuungwa mkono na watu kwa mikutano ya hadhara au sarakasi zozote za kisiasa.

Inajua kuwa wananchi wamechoka, wanataka mabadiliko. Njia ya mabadiliko inayotazamwa sasa ni CHADEMA.
Watawala wamebaki na mambo mawili ya kufanya. Ya kwanza ni kupenyeza ‘virusi' ndani ya CHADEMA. Ya pili ni kupenyeza rupia ndani ya CHADEMA katika ngazi mbalimbali.

Kinachowakera watawala ni kwamba tayari CHADEMA imeshaanza kugundua baadhi ya hatua zinazochukuliwa na CCM.

Kinachokera zaidi ni kwamba CHADEMA inaweza kuthubutu kuchukua hatua, na kupambana na matokeo. Hili nalo ni chukizo kwa CCM.

Kimsingi, CCM inatamani kuua CHADEMA, lakini haijajipanga vema. Haijui jinsi ya kuiua. Ijipange upya.
Watanzania wanajua kipi kinaelekea kaburini kati ya CCM na CHADEMA. Waachwe waamue.
 
Waandishi wa namna hii ni disaster kweli kweli, Hivi hajui Chama na mwanachama ni zaidi ya kuku na Yai, Chama kinachoshindwa kumtendea haki mwanachama, wala hakiwezi kufika mbali.
Chama kinachowapikia jungu wananchama wake eti kisa wasigombee uenyekiti, ni chama kinachojichinja chenyewe.
Mwandishi ameonyesha ushabiki wa hali ya juu huku akijitwika joho la falsafa, "eti kitakufa kwa sababu kila chenye mwanzo kina mwisho". SO WHAT IF MWANZO NI 1992 NA MWANZO WA MWISHO NI 2013?.
Bahati mbaya sana mwandishi hajaeleza ni kwa namna gani chama hushamiri, na ni kwa namna gani chama hufa. LABDA NIMKUMBUSHE TU KWAMBA, HAKI KWA KILA MWANANCHAMA NDIYO MSINGI WA UHAI WA CHAMA. NA WAJIBU WA KILA MWANACHAMA NDIYO HUKIFANYA CHAMA KISHAMIRI ZAIDI.
kwa kuwatungia tuhuma za kizushi, Viongozi wa juu, halafu ukawahukumu viongozi hao, HALAFU UKAANZA KUTAMBA KAMA ZUZU ETI CHAMA KIMEFANYA MAAMUZI MAGUMU NI UJUHA WA HALI YA JUU.
 
Akhsanta KAMANDA kwa uchambuzi makini,magambalism wanagwayagwaya kifo chao kimetimia na hakiepukiki hata kwa dua za mkesha.BYBY CCM IACHENI TANZANIA IJENGWE NA WAZALENDO WENYE MOYO.,mmetutesa sana,mmetudhalilisha sana "KAMA TAIFA TWASEMA SASA BASI,YATOSHA".
 
Huyu Ngurumo ni mwandishi wa habari(profession) au ni mwandishi wa mawakala tu kama ambavyo hata mimi naweza kuandika makala?!!
 
Kamanda umeeleweka, tatizo CCM wanaacha mambo ya msingi ambayo yangesababisha wakae madarakani wanaanza kushughulika na kutoa rushwa kwa watu ili kuharibu mifumo na demokrasia ya vyama! Wange invest kwenye huduma kwa jamii tungewaelewa rather than playing dirty politics!
 
Chama amekiua mbowe na slaa kwa kuongoza chama kilaghai kana kwamba wao ni wadogo zake na yesu kumbe wakawaida tu hata kwa mungu wameasi.
 
Msema kweli ni mpenzi wa MUNGU.Atakayekupinga ndugu mwandishi basi ni mchawi wa karne hii.
 
Huyu Ngurumo ni mwandishi wa habari(profession) au ni mwandishi wa mawakala tu kama ambavyo hata mimi naweza kuandika makala?!!

Ngurumo ni mwandishi professional na yeye zaidi huandika makala za siasa na si vuguvugu kama wengine bali amechagua upande wa kusimama na hiyo inaruhusiwa.Elimu yake inaeleweka na ameamua kuwa adui wa CCM bila kupepesa macho.
 
Mkuu mwenye kukuelewa amekuelewa, lakini asiekuelewa ana hofu na uliyoandika.
 
Waandishi wa namna hii ni disaster kweli kweli, Hivi hajui Chama na mwanachama ni zaidi ya kuku na Yai, Chama kinachoshindwa kumtendea haki mwanachama, wala hakiwezi kufika mbali.
Chama kinachowapikia jungu wananchama wake eti kisa wasigombee uenyekiti, ni chama kinachojichinja chenyewe.
Mwandishi ameonyesha ushabiki wa hali ya juu huku akijitwika joho la falsafa, "eti kitakufa kwa sababu kila chenye mwanzo kina mwisho". SO WHAT IF MWANZO NI 1992 NA MWANZO WA MWISHO NI 2013?.
Bahati mbaya sana mwandishi hajaeleza ni kwa namna gani chama hushamiri, na ni kwa namna gani chama hufa. LABDA NIMKUMBUSHE TU KWAMBA, HAKI KWA KILA MWANANCHAMA NDIYO MSINGI WA UHAI WA CHAMA. NA WAJIBU WA KILA MWANACHAMA NDIYO HUKIFANYA CHAMA KISHAMIRI ZAIDI.
kwa kuwatungia tuhuma za kizushi, Viongozi wa juu, halafu ukawahukumu viongozi hao, HALAFU UKAANZA KUTAMBA KAMA ZUZU ETI CHAMA KIMEFANYA MAAMUZI MAGUMU NI UJUHA WA HALI YA JUU.

Tuondoleee bangi zako hapa!!!! Hivi kuna haki bila wajibu? Unatimiza wajibu ndipo haki hufuata..... Mfano wa Jumbe na Seif uko sahihi kabisa kwa sababu walishindwa kutimiza wajibu kwa chama ndiyo maana chama kikawatimua japo walikuwa na haki ya kutoa maoni yao....kitu ambacho CCM ya sasa imeshndwa kuwachukulia hatua mafisadi ndani ya chama.... Au ndo kulinda haki zao ndani ya chama kwa sababu mafisadi ndo msingi wa CCM?? Hivi watoto na wajukuu zako wakisoma huu uharo wako si watajiuliza sana uwezo wako wa kupambanua mambo
 
Chama amekiua mbowe na slaa kwa kuongoza chama kilaghai kana kwamba wao ni wadogo zake na yesu kumbe wakawaida tu hata kwa mungu wameasi.

!
!
ukome tena ukome na iwe mwanzo na mwisho kuandika 'yesu'....nyambafu wewe,andika Yesu au YESU, kama huwezi acha. una akili sana wewe,Mwalimu mkuu mama yako nini?
 
Tuondoleee bangi zako hapa!!!! Hivi kuna haki bila wajibu? Unatimiza wajibu ndipo haki hufuata..... Mfano wa Jumbe na Seif uko sahihi kabisa kwa sababu walishindwa kutimiza wajibu kwa chama ndiyo maana chama kikawatimua japo walikuwa na haki ya kutoa maoni yao....kitu ambacho CCM ya sasa imeshndwa kuwachukulia hatua mafisadi ndani ya chama.... Au ndo kulinda haki zao ndani ya chama kwa sababu mafisadi ndo msingi wa CCM?? Hivi watoto na wajukuu zako wakisoma huu uharo wako si watajiuliza sana uwezo wako wa kupambanua mambo

sasa wewe umejibu nini hapo. Si bora ungekaa kimya tu
 
Weka picha kama ni kweli:

Zitto.jpg
 
“Sasa unaachaje kumsikiliza huyu na ukamsikiliza zaidi mtu ambaye hana sifa za kimageuzi katika ngazi ya kitaifa? Wanaozua tuhuma dhidi ya wenzao hawana hata miaka mitano ndani ya chama?
“Labda nikupe mfano mzuri. Hivi unategemea leo, CCM kwa mfano, eti akina Richard Tambwe Hizza, waanzishe mkakati wa kumng’oa kwenye chama mtu kama Kingunge Ngombale Mwiru kwa madai ni msaliti? Haya mambo yako CHADEMA tu,” alisema mwanasiasa huyo
 
@ Gamba la Nyoka, Haki ipi apatiwe mwanachama anayevunja katiba ya chama? Mbona CCM walimfanyia mizengwe ya chini chini JMS kutangaza adhma ya kupambana na JMK ktk kuteuliwa na chama kuwania uraisi ktk muda na wakati sahihi kwa mujibu wa katiba ya chama hata akaamua kujitoa mwenyewe.Hiyo ndio haki kwa mwanachama?
CDM haitakufa,mpaka CCM itakapokufa!
 
Rudi tena shule ukajifunze namna ya kusoma habari na kuchambua maudhui yake.
 
Waandishi wa namna hii ni disaster kweli kweli, Hivi hajui Chama na mwanachama ni zaidi ya kuku na Yai, Chama kinachoshindwa kumtendea haki mwanachama, wala hakiwezi kufika mbali.
Chama kinachowapikia jungu wananchama wake eti kisa wasigombee uenyekiti, ni chama kinachojichinja chenyewe.
Mwandishi ameonyesha ushabiki wa hali ya juu huku akijitwika joho la falsafa, "eti kitakufa kwa sababu kila chenye mwanzo kina mwisho". SO WHAT IF MWANZO NI 1992 NA MWANZO WA MWISHO NI 2013?.
Bahati mbaya sana mwandishi hajaeleza ni kwa namna gani chama hushamiri, na ni kwa namna gani chama hufa. LABDA NIMKUMBUSHE TU KWAMBA, HAKI KWA KILA MWANANCHAMA NDIYO MSINGI WA UHAI WA CHAMA. NA WAJIBU WA KILA MWANACHAMA NDIYO HUKIFANYA CHAMA KISHAMIRI ZAIDI.
kwa kuwatungia tuhuma za kizushi, Viongozi wa juu, halafu ukawahukumu viongozi hao, HALAFU UKAANZA KUTAMBA KAMA ZUZU ETI CHAMA KIMEFANYA MAAMUZI MAGUMU NI UJUHA WA HALI YA JUU.

Ooh kumbe maneno meengi halafu Id name ni Gamba la Nyoka. Sina haja ya kuongeza neno kwaheri Gamba
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom