Green Thoughts
Member
- Aug 25, 2022
- 42
- 71
Kwenye maisha, sio ngumu sana kugundua kuwa mtu fulani hayupo pamoja nami katika jambo fulani, bali ni ngumu kukubaliana na ile hali kuwa mtu fulani hayupo pamoja nami katika jambo fulani, hasa yule uliyekuwa ukitegemea zaidi kutoka kwake. Hiki ndicho kinachoumiza zaidi.
Muda mwingine ukweli unakuwaga dhahiri na wazi kabisa, lakini changamoto inakuja pale tunapotaka kulazimisha ukweli usiwe kweli.
Hatutaki kuruhusu ule uhalisia ujidhihirishe mbele ya tunachokiona au tunachokishuhudia. Hapo ndipo tunakosea na tunaanza kuumia ama kujiumiza wenyewe.
Tukiamua kuruhusu ukweli uwe dhahiri na kukubaliana nao kama ulivyo, tunaweza kujiweka huru na vitu vingi ambavyo tunakutana navyo katika maisha yetu ya kila siku.
Tusimame na Kweli, kweli itatuweka huru na kutupa amani ya moyo katika vitu ambavyo viko nje ya uwezo wetu kuviweka vile tutakavyo.