Ngumi Jiwe!

Jaguar

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2011
Posts
3,440
Reaction score
1,029
Jamaa mmoja mrefu alikuwa akipigana na mshikaji mmoja mfupi sana mida ya saa 2 usiku. Watu walipoingilia kati kutaka kuwatenganisha, yule jamaa mrefu akasema, "hebu niacheni nimfundishe adabu huyu pimbi".

Baada ya kama dakika mbili,yule jamaa alipigwa kichwa na yule jamaa mfupi, akaanguka chini, akaanza kulia,' mamaa nakufaa, nichukulieni namba za gari iliyonigonga!.

[WATU]:Hakuna gari iliyopita hapa, ni yule pimbi kakupiga.
[JAMAA MREFU]:Basi naombeni nyundo aliyonipigia!.
[WATU]:Hakuwa na nyundo.
[JAMAA MUREFU]:Basi nipelekeni kivulini!.
[WATU]:Mida hii ni usiku, hakuna jua!
 
teh teh madharau sio ishu,unamwona mtu ana umbo ndogo ila amekomaa
 
Jamaa kaona jua usiku?? Kweli pimbi mtata
 
Naomba nipelekeni hosptali! Amenipiga na ki2 kama spiringi yani kapigwa kofi moja mpk chini!
 
Watu wengine wamekandwa na wazi wanavunjia kichwani mwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…