joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Mimi ningewashauri wakenya mje Tanzania kujifunza ni jinsi gani Nyerere alivyoweka msingi wa matumizi wa hizi lugha ili ziweze kutumika bila kuleta hathari mbaya ya ukabila.
Watanzania 98% huko vijijini hutumia lugha zao za makabila, kwasababu huko vijijini zaidi ya 99% ya wanaoishi ni kutoka katika kabila moja, uwezekano wa kuweka makundi kwa misingi ya ukabila ni Kama haupo kwasababu wote ni kabila Moja.
Unapokuja katika ofisi za serikali au mijini hali ibabadilika sana, watu wamechanganyika kutoka mikoa na makabila mbalimbali, kila mtu akianza kuzungumza lugha yake inakua ni fujo na watu wanajitenga, hata kupata huduma katika ofisi za serikali kunaanza kuathiriwa.
Typical Example ni Nchi ya Belgium ambayo imegawanyika kutukana na lugha, ukiingia Hotels za Brussels ukizungumza "Flemish" ambayo ni lugha kuu ya Kaskazini mwa Belgium, sio rahisi kupata huduma wanataka uzungumze kifaransa ambayo ni lugha kuu ya kusini mwa Belgium.