Ngúgí Wa Thiong'o awahutubia Wahispania kwa lugha ya Gíkúyú baada ya Rais wa Cataluña kumtunuku tuzo la Premi Internacional Catalunya

kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,076
2,000
Kitu chochote kinacholeta matatizo katika jamii au kuwafanya watu watengane, wachukiane na kupigana ni kitu kibaya bila kujali nani amekileta.

Ukabila ni chimbuko letu waafrika, lakini katika nchi nyingi, ukabila umekua ndio chanzo cha mifarakano na mapigano, dini zimeletwa na wageni, lakini kuna baadhi ya nchi dini zimekua chanzo cha mifarakono na mapigano.

Pale ambapo makabila hayana athari mbaya kama Tanzania, sio vibaya kuendekeza na kutanguliza makabila, lakini kwa nchi kama Rwanda na Kenya, ni hatari sana kuachia ukabila kuzagaa mitaani kwasababu ni sawa na kumwaga Petrol katika nyasi kavu, lazima yatalipuka.
Sio kweli, Somalia ni jamii moja na lugha yao moja lakini wanapigana.

Huwezi kumwambia mtu akatae asili yake ili awe mtumwa wa identity bandia ya mzungu.

Lazima tukubali kuwa sisi ni watu tofauti na historia zetu ni tofauti. Huwezi kulazimisha watu tofauti waishi pamoja kwa kupuuza tofauti zao.

Kwa nini hatupambani kuondoa dini za kigeni kwa sababu ni msingi wa matatizo mengi Afrika?
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
19,439

Mbona inaonekana unasoma post ili kujibu badala ya kusoma ili kuelewa?, wacha papara soma kwa makini. Nimesema kitu chochote kinachosababisha mifarakano ktk jamii bila kujali kama chimbuko Lake ni African au nje ya Africa, basi hicho kitu ni kibaya, nikatoa mifano miwili ya Ukabila na udini ambavyo vyote huwa vinasababisha malumbano, ninakushangaa unaponiuliza kuhusu dini wakati nimeshaitaja, tulia wacha papers.

Somalia wanapigana kwasababu ya koo mbalimbali, hiyo ni sehemu ya ukabila, siwezi kutaja mifano yote hapa, muhimu tulia usome kwa utulivu
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,456
2,000
Wewe utakuwa ni mjinga wa kwanza. Mtu kuzungumza lugha yake ya asili ni jambo la kujitambua. Hayo unayoita makabila ndiyo utambulisho wetu wa asili na sote tunaojitambua hatuwezi kuyatupa.

Hizo nchi za Afrika zilitengenezwa na Wazungu na hamna ufahari wowote kujiita mzalendo wa nchi iliyoundwa na Mzungu.

Wewe kama hupendi kabila lako baki na ujinga wako.
Wewe ni shoga taahira
 
kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,076
2,000
Mbona inaonekana unasoma post ili kujibu badala ya kusoma ili kuelewa?, wacha papara soma kwa makini. Nimesema kitu chochote kinachosababisha mifarakano ktk jamii bila kujali kama chimbuko Lake ni African au nje ya Africa, basi hicho kitu ni kibaya, nikatoa mifano miwili ya Ukabila na udini ambavyo vyote huwa vinasababisha malumbano, ninakushangaa unaponiuliza kuhusu dini wakati nimeshaitaja, tulia wacha papers.

Somalia wanapigana kwasababu ya koo mbalimbali, hiyo ni sehemu ya ukabila, siwezi kutaja mifano yote hapa, muhimu tulia usome kwa utulivu

Kwa hiyo wewe ukiwa 'Mtanzania' maana yake ndiyo ufarakane na 'Mkenya' kwa kuwa ni watu tofauti?

Kama unajichukia wewe na identity yako waache wanaojitambua kujivunia asili yao.
Sisi tunaojitambua hatuwezi kuua lugha zetu kwa sababu ya vinchi feki vilivyotengenezwa na Mzungu.
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
19,439
2,000
Kwa hiyo wewe ukiwa 'Mtanzania' maana yake ndiyo ufarakane na 'Mkenya' kwa kuwa ni watu tofauti?

Kama unajichukia wewe na identity yako waache wanaojitambua kujivunia asili yao.
Sisi tunaojitambua hatuwezi kuua lugha zetu kwa sababu ya vinchi feki vilivyotengenezwa na Mzungu.
Mwenye kujitambua hawezi kumchinja jirani yake kwasababu tu sio kabila lake. Kenya na Tanzania ni mikwaruzano ya ndani ya familia moja, hata wewe na jirani wake au hata ndugu wa damu moja huwa mnakwaruzana mara kwa mara lakini sio kawaida kufikia hatua ya kuchinjana kama ilivyotokea hapo Kenya na Rwanda.
 
kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,076
2,000
Mwenye kujitambua hawezi kumchinja jirani yake kwasababu tu sio kabila lake. Kenya na Tanzania ni mikwaruzano ya ndani ya familia moja, hata wewe na jirani wake au hata ndugu wa damu moja huwa mnakwaruzana mara kwa mara lakini sio kawaida kufikia hatua ya kuchinjana kama ilivyotokea hapo Kenya na Rwanda.
Mtu kujivunia kabila lake hakumfanyi achukie wengine. Watu wasipoongea lugha zao maana yake hizo lugha zitakufa.

Lugha yako ikifa ni kwamba identity yako imekufa. Wengine historia zetu hazikuanzia Berlin 1884 na hatuwezi kutoa sadaka historia.
 
Chamoto

JF-Expert Member
Dec 7, 2007
6,624
2,000
Tukumbuke kuwa hata Kiswahili ni matokeo ya biashara ya utumwa na hamna ufahari wowote katika lugha hiyo.
Utaelezeaje mikoa ambayo utumwa haukuwepo wenyeji wakikijua kiswahili, naongelea karne ya 19.
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
19,439
2,000
Mtu kujivunia kabila lake hakumfanyi achukie wengine. Watu wasipoongea lugha zao maana yake hizo lugha zitakufa.

Lugha yako ikifa ni kwamba identity yako imekufa. Wengine historia zetu hazikuanzia Berlin 1884 na hatuwezi kutoa sadaka historia.
Huwezi kutoa sadaka Historia na identity lakini mpo tayari kutoa sadaka uhai na maisha ya watu kwa ajili ya kulinda lugha za makabila yenu, hizo akili ni made in Kenya
 
kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,076
2,000
Utaelezeaje mikoa ambayo utumwa haukuwepo wenyeji wakikijua kiswahili, naongelea karne ya 19.

Kiswahili asili yake ni Pwani ya Afrika Mashariki, huko kwingine lugha hiyo ilienea tu. Hata jina lenyewe la lugha hiyo ni la Kiarabu.

Lugha ya Mhaya ni Kihaya, lugha ya Msukuma ni Kisukuma, lugha ya Mmaasai ni Kimaasai n.k. Ni jambo la ajabu kumshangaa mtu anayeongea lugha yake.
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
19,439
2,000
Kiswahili asili yake ni Pwani ya Afrika Mashariki, huko kwingine lugha hiyo ilienea tu. Hata jina lenyewe la lugha hiyo ni la Kiarabu.

Lugha ya Mhaya ni Kihaya, lugha ya Msukuma ni Kisukuma, lugha ya Mmaasai ni Kimaasai n.k. Ni jambo la ajabu kumshangaa mtu anayeongea lugha yake.
Kiswahili ni mkusanyika wa lugha nyingi za Africa na baadhi ya lugha za nje kwasababu wote walikua wanakutana pwani na kubadilishana bidhaa. Kiswahili kinaunganisha makabila mengi tofauti tofauti, kuna sababu gani ya kuzungumza lugha ya kabila moja wakati ipo lugha inayounganisha makabila yote kama sio kutaka kujitenga?
 
kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,076
2,000
Huwezi kutoa sadaka Historia na identity lakini mpo tayari kutoa sadaka uhai na maisha ya watu kwa ajili ya kulinda lugha za makabila yenu, hizo akili ni made in Kenya

Waangalie Wamarekani Weusi halafu uje na tathmini. Hawaongei lugha zao na wala hawana majina yao ya asili, je wanaishi vizuri na wazungu sababu wanaongea lugha moja?
Hamna uhusiano wa watu kuongea lugha tofauti na kupigana. Wasukuma wanaongea lugha moja na kila siku wanauwana.
 
Chamoto

JF-Expert Member
Dec 7, 2007
6,624
2,000
Kiswahili asili yake ni Pwani ya Afrika Mashariki, huko kwingine lugha hiyo ilienea tu. Hata jina lenyewe la lugha hiyo ni la Kiarabu.
Siyo kweli, muundo wa lugha ya kiswahili ni wa kibantu (kiafrika), kama umewahi kuwa karibu na waarabu watakuambia kuwa hawaelewi muundo wa lugha yetu. Ila mzulu au mshona ataelewa kiasi kwa kuwa kuna mfanano wa kimuundo baina ya lugha za kibantu.
 
kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,076
2,000
Kiswahili ni mkusanyika wa lugha nyingi za Africa na baadhi ya lugha za nje kwasababu wote walikua wanakutana pwani na kubadilishana bidhaa. Kiswahili kinaunganisha makabila mengi tofauti tofauti, kuna sababu gani ya kuzungumza lugha ya kabila moja wakati ipo lugha inayounganisha makabila yote kama sio kutaka kujitenga?
Kiswahili ni mchanganyiko wa lugha ya mabwana (waarabu) na watumwa (Wabantu). Kiarabu ni zaidi ya 35% ya Kiswahili.

Sasa mtu tofauti na wewe akijitenga wewe shida yako ni nini? Kitendo cha kuwa na lugha tofauti maana yake nyie ni watu tofauti.

Tufunge makanisa na misikiti kama tunalenga kutengeneza identity moja.
 
kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,076
2,000
Siyo kweli, muundo wa lugha ya kiswahili ni wa kibantu (kiafrika), kama umewahi kuwa karibu na waarabu watakuambia kuwa hawaelewi kwa nini muundo uko hivyo ila mzulu au mshona ataelewa vizuri kwa kuwa kuna mfanano.

Kiswahili ni mchanganyiko wa lugha ya mabwana (waarabu) na watumwa (Wabantu). Kiarabu ni zaidi ya 35% ya Kiswahili.

Muundo wa kibantu (hasa Chishona na Chichewa) lakini zaidi ya 35% ya misamiati ni Kiarabu. Neno Kiswahili lenyewe ni Kiarabu.

Hamna ufahari kwenye lugha ya kitumwa hiyo.
 
kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,076
2,000
Siyo kweli, muundo wa lugha ya kiswahili ni wa kibantu (kiafrika), kama umewahi kuwa karibu na waarabu watakuambia kuwa hawaelewi muundo wa lugha yetu. Ila mzulu au mshona ataelewa kiasi kwa kuwa kuna mfanano wa kimuundo baina ya lugha za kibantu.

Kiarabu: Sita Mia, Kiswahili : Mia sita
Kiarabu : Wali samaki, Kiswahili : Wali samaki
Kiarabu : Saba dakika, Kiswahili : Dakika saba

Ukiongea Kiswahili, Muarabu anaelewa maneno mengi unayoongea.
 
Chamoto

JF-Expert Member
Dec 7, 2007
6,624
2,000
Kiarabu: Sita Mia, Kiswahili : Mia sita
Kiarabu : Wali samaki, Kiswahili : Wali samaki
Kiarabu : Saba dakika, Kiswahili : Dakika saba

Ukiongea Kiswahili, Muarabu anaelewa maneno mengi unayoongea.
Tangu lini muundo wa sentensi ukakosa kitenzi?
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
19,439
2,000
Waangalie Wamarekani Weusi halafu uje na tathmini. Hawaongei lugha zao na wala hawana majina yao ya asili, je wanaishi vizuri na wazungu sababu wanaongea lugha moja?
Hamna uhusiano wa watu kuongea lugha tofauti na kupigana. Wasukuma wanaongea lugha moja na kila siku wanauwana.
Tatizo lako ni ufinyu wa uwelewa na mawazo mafupi, kila mafarakano yana sababu tofauti tofauti, Marekani sababu kubwa ya kuuana ni shootings kutokana na kuzagaa kwa silaha za mikononi, sababu nyingine ni ubaguzi wa rangi.

Afrika kusini sababu kubwa ya mifarakano ni crime inayotokana na tofauti ya kipato kati ya wazungu na watu weusi, pia ni kutokana na kuzagaa kwa silaha mitaani tangu enzi za Vita vya ukombozi.

Somalia sababu ni Alshabab na mabishano Kati ya koo za wasomali. Kenya sababu kubwa za mizozo ni mauaji ni Ugaidi, ukabila na dhuluma katika kumiliki ardhi, kuzagaa kwa silaha haramu pia kunachangia. Nimeshanga kusikia wasukuma wanauana, hao ni wasukuma wa nchi gani?.

Usisahau kwamba Tanzania ni nchi ya 52 duniani kwa amani wakati Kenya ni nchi ya 125, Tanzania ni watu wastaarabu hatuwezi kuuana hovyo kama wanyama.
 
MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
22,045
2,000
Kiswahili ni mchanganyiko wa lugha ya mabwana (waarabu) na watumwa (Wabantu). Kiarabu ni zaidi ya 35% ya Kiswahili.

Muundo wa kibantu (hasa Chishona na Chichewa) lakini zaidi ya 35% ya misamiati ni Kiarabu. Neno Kiswahili lenyewe ni Kiarabu.

Hamna ufahari kwenye lugha ya kitumwa hiyo.

Huwa napishana na wewe kwenye hoja zingine lakini kwa hili la kuenzi lugha zetu za asili naungana nawe kwa dhati, hainingii akilini niende kuwasabahi wazee wetu kijijini kule Ukikuyuni halafu niongee nao kwa Kiswahili, huo ndio utumwa haswa. Kwangu mimi japo nakipenda Kiswahili ila huwa nimekiweka kwenye kiwango kimoja na Kingereza, maana kwamba sio lugha yangu ya asili, kinaniwezesha kuwasiliana na wasio wa asili yangu hapa EAC, kama ilivyo kwa Kingereza, hunisaidia pale nahitaji kuwasiliana na Wachina, Warusi, Waghana, Wamarekani n.k.

Muhimu sana kuhakikisha hata watoto tunaozaa na kulea wanazungumza lugha zetu za asili, la sivyo tutaendelea kufutwa na kumezwa wote. Unakuta mzee mzima mjini hajui hata salamu kwa lugha yake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom