Ngúgí Wa Thiong'o awahutubia Wahispania kwa lugha ya Gíkúyú baada ya Rais wa Cataluña kumtunuku tuzo la Premi Internacional Catalunya

joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
19,443
2,000
Wewe you just mental redemption,if u have ever attended a psychology class it just shows you are a person mwenye umelelewa Kwa chuki such that you cannot appreciate the success of other people
Umeshindwa kujenga hoja badala yake umeamua kukimbilia katka Personal attacks sio?
 
MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
22,047
2,000
Hiii kisukuma inasound kiluhyia/kikisii but wanazungumza haraka kama kikisii

Yeah Wasukuma wanaendana sana na Waluhya hata kwenye aina ya vyakula kama ugali, ila Wanyambo na Wahaya ndio wana undugu kabisa na Waluhya, kama unafahamu Kiluhya ni vigumu sana Mnyambo wa Tanzania akuseme kwa kilugha bila wewe kumshtukia, utaelewa kama 60% ya kila anachokisema, nilishangaa sana hii maana mimi nakifahamu Kiluhya haswa Kinyole, sasa kuna Wanyambo walikua wakianza kuongea kilugha najikuta nikiwaelewa vizuri sana.
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,447
2,000
Sio Mkenya kweli huyo Ngugi? upuuzi wa kubaguana na kuchinjana kwao wanahamishia kwa wengine hovyo sana Kenya
Kwahivyo mhispania akizungumza kwa kihispania huwa anaendeleza ubaguzi? Hizi akili bana ni kama za sokwe.
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
19,443
2,000
Kwahivyo mhispania akizungumza kwa kihispania huwa anaendeleza ubaguzi? Hizi akili bana ni kama za sokwe.
Tulia dawa ikuingie, lazima mikutano ya hadhara ya kitaifa itumike lugha ya Taifa husika inayoeleweka kwa watu wengi, Hispania lugha yao ya Taifa ni Kihispania, utasemaje wanaendeleza ukabila?, wacha kutapatapa, lazima mkubali kwamba Kenya kuna tatizo la ukabila na matumizi ya lugha zenu katika mikutano ya hadhara na katika vyombo vya habari vinachangia sana kuendeleza ukabila
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,447
2,000
Miafrika bana.Pambaneni na umasikini. Kuzungumza mijilugha yenu hautawboreshea maisha wala kufuta colonial legacy.Focus kwenye mambo ya msingi
Huu ni utumwa, ulitegemea Ngúgí ahutubie wahispania kwa kiingereza, kwenye hafla ambayo ilikuwa ya kumtunukia tuzo kwa kuzienzi tamaduni na lugha za kiafrika?
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
19,443
2,000
Huu ni utumwa, ulitegemea Ngúgí ahutubie wahispania kwa kiingereza, kwenye hafla ambayo ilikuwa ya kumtunukia tuzo kwa kuzienzi tamaduni na lugha za kiafrika?
Zaidi ya Kikuyu ameshaandika kwa kutumia lugha zipi za hapo Kenya?, lazima mkubali kwamba katika hilo wakenya mnakosea sana na mnapaswa kujifunza toka Tanzania, sio kwamba hatuna makabila au hatujui kuzungumza lugha zetu za asili, lakini tunajua kwa kufanya hivyo tutaanza kujitenga katika makundi ya kikabila.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,457
2,000
Huu ni utumwa, ulitegemea Ngúgí ahutubie wahispania kwa kiingereza, kwenye hafla ambayo ilikuwa ya kumtunukia tuzo kwa kuzienzi tamaduni na lugha za kiafrika?
Aanze kabisa na kuvaa ngozi ili aepuke utumwa kabisa
 
BlietzKrieg

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
2,233
2,000
Yeah Wasukuma wanaendana sana na Waluhya hata kwenye aina ya vyakula kama ugali, ila Wanyambo na Wahaya ndio wana undugu kabisa na Waluhya, kama unafahamu Kiluhya ni vigumu sana Mnyambo wa Tanzania akuseme kwa kilugha bila wewe kumshtukia, utaelewa kama 60% ya kila anachokisema, nilishangaa sana hii maana mimi nakifahamu Kiluhya haswa Kinyole, sasa kuna Wanyambo walikua wakianza kuongea kilugha najikuta nikiwaelewa vizuri sana.
great lake Bantus,
Jamii ya Loogoli ni wakisii,wakuria,wazanaki(Nyerere tribe),wamaragoli,waNyore,Tiriki,Simbiti,Ikoma,
Hawa lugha zao ni 80% same especially kisii-kuria-maragoli
 
Tony254

JF-Expert Member
May 11, 2017
12,130
2,000
Tuzo la Premi Intercional Catalunya(kwa kicatalan) au El Premio Intercional Cataluña(kwa kihispania) ni tuzo ambalo serikali ya Catalonia, nchini Uhispania, imekuwa ikiwatunukia watu tofauti tangia mwaka wa 1989.

Tuzo hilo huwa linatunukiwa watu ambao wamebobea kwenye nyanja tofauti kote duniani na wakaigusa dunia kwa njia moja au nyingine. Waafrika wawili tu ndio wamepokea tuzo hilo, mmoja wao akiwa ni Desmond Tutu wa S.A.

Mwaka huu mwandishi mashuhuri kutoka Kenya, Ngúgí Wa Thiong'o, ndiye aliyetunukiwa tuzo hilo. Rais wa Catalonia kwenye hafla iliyopeperushwa live alisema kwamba Ngúgi Wa Thiong'o alitunukiwa tuzo hilo kwasababu ya juhudi zake. Kwenye kuhifadhi na kuendeleza mila, desturi, utamaduni na lugha za kiafrika.

Ngúgí alitoa hotuba ya kupokea tuzo hilo kwa lugha ya Gíkúyú, huku tafsiri ikitolewa kwa lugha ya kihispania. Ní thígio múno Ngúgi, njamba ya Kírínyaga, na Ngai arokúrathima múno.(Shukran kwake Ngúgí) *Hotuba ya Ngúgí inaanza @ 46:50.

Asante kwa habari hii. Tupende lugha zetu.
 
Tony254

JF-Expert Member
May 11, 2017
12,130
2,000
Lakini huyu huyu ndiye aliyeandika Kitabu cha "This time tomorrow " kuhusu siasa mbovu za ubepari za Kanya, mkamfukuza na kumfunga na kumuita msaliti hadi leo mnafurahia ubepari wakati yeye unaupinga kwa nguvu zote.

Kumbuka kwamba ukabila Kenya ulisababishwa na viongozi na wasomi wakubwa hapo Kenya Kama Jommo Kenyatta, Moi, Jaramogi, Tom Mboya na Ngugi wa Thiong, kwa kutukuza makabila yao politically, intellectually or otherwise.
Tutaendelea kutukuza kabila zetu. Wewe endelea kulia.
 
ntamaholo

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
12,613
2,000
Sitegemei kajamba kama wewe ambaye huwa hasomi amjue au amuelewe Ngúgí Wa Thiong'o. Muacha mila ni mtumwa. Ngúgí ametunukiwa na anafahamika kote duniani kwasababu ya kazi yake nzuri ya kuendeleza na kuhifadhi mila, utamaduni na lugha za kiafrika.

Vitabu vyake huwa anaviandika kwa lugha ya kikuyu na vimesomwa na vikashinda tuzo nyingi kote duniani. Vitabu vyake vimetafsiriwa kwa lugha zaidi ya 90! Baadhi ya vitabu vyake; Weep Not, Child, A Grain Of Wheat, Dreams in a Time of War, Petals of Blood, The Trial of Dedan Kimathi, Devil on the Cross(Shetani Msalabani), The River Between, The Black Hermit, I Will Marry When I Want, In the House of the Interpreter, Wizard of the Crow n.k, n.k.
Niandikie I will marry when I want kwa kikuyu tagadhali
 
pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
11,447
2,000
Niandikie I will marry when I want kwa kikuyu tagadhali
Ngahika(I Will Marry) Ndeenda(When I Want). Alafu kitabu hicho sio cha riwaya ni tamthilia moja kali sana. Cover ya version ya kwanza ya kitabu hicho. kwa kikikuyu, ndio hii hapa.
ngaahikaNdeenda.jpg
 
kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,076
2,000
Miafrika bana.

Pambaneni na umasikini. Kuzungumza mijilugha yenu hautawboreshea maisha wala kufuta colonial legacy.

Focus kwenye mambo ya msingi

Wewe utakuwa ni mjinga wa kwanza. Mtu kuzungumza lugha yake ya asili ni jambo la kujitambua. Hayo unayoita makabila ndiyo utambulisho wetu wa asili na sote tunaojitambua hatuwezi kuyatupa.

Hizo nchi za Afrika zilitengenezwa na Wazungu na hamna ufahari wowote kujiita mzalendo wa nchi iliyoundwa na Mzungu.

Wewe kama hupendi kabila lako baki na ujinga wako.
 
kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,076
2,000
Tribalism shall never end in Kenyaland.
Hamna shida ya Mkikuyu kuongea lugha yake. Angeongea lugha nyingine angeonesha kuwa yeye ni mtumwa.

Nchi kama Tanzania na Kenya ni matokeo ya ukoloni na hamna mtu anayejitambua atayetupa kabila lake kwa identity ya mzungu.

Tukumbuke kuwa hata Kiswahili ni matokeo ya biashara ya utumwa na hamna ufahari wowote katika lugha hiyo.
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
19,443
2,000
Hamna shida ya Mkikuyu kuongea lugha yake. Angeongea lugha nyingine angeonesha kuwa yeye ni mtumwa.

Nchi kama Tanzania na Kenya ni matokeo ya ukoloni na hamna mtu anayejitambua atayetupa kabila lake kwa identity ya mzungu.

Tukumbuke kuwa hata Kiswahili ni matokeo ya biashara ya utumwa na hamna ufahari wowote katika lugha hiyo.
Kitu chochote kinacholeta matatizo katika jamii au kuwafanya watu watengane, wachukiane na kupigana ni kitu kibaya bila kujali nani amekileta.

Ukabila ni chimbuko letu waafrika, lakini katika nchi nyingi, ukabila umekua ndio chanzo cha mifarakano na mapigano, dini zimeletwa na wageni, lakini kuna baadhi ya nchi dini zimekua chanzo cha mifarakono na mapigano.

Pale ambapo makabila hayana athari mbaya kama Tanzania, sio vibaya kuendekeza na kutanguliza makabila, lakini kwa nchi kama Rwanda na Kenya, ni hatari sana kuachia ukabila kuzagaa mitaani kwasababu ni sawa na kumwaga Petrol katika nyasi kavu, lazima yatalipuka.
 
joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
19,443
2,000
Ngahika(I Will Marry) Ndeenda(When I Want). Alafu kitabu hicho sio cha riwaya ni tamthilia moja kali sana. Cover ya version ya kwanza ya kitabu hicho. kwa kikikuyu, ndio hii hapa.
ngaahikaNdeenda.jpg
Endeleeni kuendekeza huu ujinga matokeo yake ni haya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom