Ngorongoro Conservation Area - Home of the brave

Buyaka

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
1,643
1,786




























Eat grass, don't piss!

By Thomas Whetten, Ngorongoro Conservation Area
 
Kitoweo kimekimbia, Sizitaki mbichi hizi.

Simba hapo atakuwa alisema kwanza hujanona mifupa tu, nilikuwa nakutania
 
Mzee mzima chali!! Nifundisho hilo si kila kilicho mbele yako kina lika
 
Kamjeruhi lakini vibaya..Dah atapona mbele bora hajaliwa..



Akaamua Kula pozi hapa.
 
Ndio, mkae mkijua kuwa simba mwindaji ni jike 2! Dume huwa anasubiri kukuta kitoweo kipo tayari. Anayebisha aendelee kufanya uchunguzi..
 
Huyu simba atakuwa anajifunza kuwinda!!! Simba yeyote mzoefu hawezi kumwinda pundamilia kinyumenyume...lazima atakwidwa teke... Tazama picha za wanyama simba yeyote mzoefu akimfukuza pundamilia pale anapomkaribia tu anaanza kumwendea kiubavu-ubavu ili amdake shingoni.

Simba huyu sharobaro sana. LOL
 
Huyu Simba dume inaelekea ametengwa katika kundi au mzee au njaa kali, katika natural state simba dume si mwindaji kawaida huwa ana ambush au anawinda wanyama wadogo kama ngiri,nguruwe n.k au weak spp kama binadamu,mifugo hivyo hii picha ni nzuri sana hayo diyo maajabu ya Ngorongoro.
 

Sina haja naye nyama yake si tamu kama Impalla
 
Simba dume si mwindaji mzuri kama Simba jike.Ukimtazama kwa makini atakuwa ni simba dume mzee kidogo atakuwa kafukuzwa kundini.Simba dume mzee kwanza hana nguvu.pili ana mzingo wa mawazo ya kufukuzwa ndani ya kundi,tatu uwezo wa kula chakula bila kubughuziwa na wanyama wengine kama fisi hata mbwa mwitu unaongezeka.Akitokea mnyama dhaifu ni nafuu yake,hata binadamu ni size yake.
 
Kosa kubwa la huyu simba ni kumtokea pundamilia kwa nyuma. Ilikuwa ni lazima apate kibano cha mateke. Mateke ya kwenye picha ya sita na ya saba ndio yalimaliza kazi hapa. Hili teke la kwenye picha ya saba si ajabu limemng'oa jino huyu simba. Moja ya maonyo tuliyokuwa tukipewa tukiwa wadogo ni kuepuka kumfuata punda kwa nyuma kwani mateke yake ni mabaya sana na yanaweza kukuua yakikupata vilivyo.
 

Na mchunguze pia utakuta hana sharubu. Ukiona hivyo huyo jike na hamkosi. Midume ya simba ina papara sana na sio wawindaji wazuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…