Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,875
Na
Jesca Lutego
Mwenyekiti wa Ngome ya vijana ACT Wazalendo Taifa Abdul Nondo, akiongea na vijana katika mkutano wa Naibu katibu Mkuu Ndug. Joram Bashange
Aidha Abdul Nondo , ameelezea changamoto ya vijana na wakazi wa Jimbo la Kigoma Mjini kuhusu changamoto ya shughuli za kiuchumi, mzunguko wa fedha na ukosefu wa ajira akisema Kigoma ni fukara , Kigoma hakuna mzunguko wa fedha na shughuli za kiuchumi zimedorora, vijana hawana ajira na sababu kubwa ni serikali kwa makusudi kuanzia mwaka 2015 kuzuia miradi ya kiuchumi na kimaendeleo Kigoma ambayo ilitafutwa na aliyekuwa Mbunge Zitto Zuberi Kabwe na Manispaa.
Amesema kuwa mradi wa maboresho ya Bandari ya Kigoma Mjini, ambapo Shirika la JICA la JAPAN lilitoa fedha za msaaada Tsh. Bilion 100 ili kuboresha Bandari ya Kigoma Mjini ila serikali ya awamu ya tano ilizizuia anamuomba Mh. Rais Samia , anamuomba Makamu wa Rais Mh. Mpango na Mh. Mwigulu Nchemba kuziachia fedha hizo ili kusaidia maboresho ya Bandari Kigoma ili kufaidika na fursa za kiuchumi kupitia nchi jirani za Congo na Burundi.Nondo amekumbushia tena suala la matengenezo ya meli hata umuhimu wa kuletwa meli mpya ili wakazi wa Kigoma mjini wanufaike na shughuli za kiuchumi kuongezeka.
Pia, Mwenyekiti Nondo amesema Bandari ikiboreshwa,Reli ya kati ya Standard Gauge pia inapaswa kuunganishwa haraka, bila kusubiri ya kutokea Tabora kwenda Mwanza kuisha kwani inawezekana kabisa serikali kutafuta Mkandarasi ambaye ataanzia Tabora hadi Kigoma ili Kigoma kunufaika kiuchumi.