Ng'ombe wa milioni 400/- wapotea NARCO

Ng'ombe wa milioni 400/- wapotea NARCO

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

Deo%20Filikunjomb-October28-2014.jpg

Mwenyekiti wa PAC,Deo Filikunjombe

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imesema Shirika la Ranchi za Taifa (Narco), halistahili kupewa Sh. bilioni 17 walizoomba serikalini kutokana na kushindwa kusimamia uendeshaji na upotevu wa ng'ombe 376 katika Ranchi ya Ruvu mkoani Pwani.

Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe, jana alitoa maelekezo ya kamati kwa viongozi wa Narco na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, baada ya kuwahoji juu ya taarifa ya ukaguzi maalum iliyofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Alisema ukaguzi huo ulibaini kuwa ngombe 376 wamepotea kwa kipindi cha miezi mitatu, makato ya mifuko ya hifadhi ya jamii ya wanachama haipelekwi, kushindwa kuendelea kwa ujenzi wa machinjio licha ya serikali kutoa fedha na kuendelea kudidimia kwa Shirika hilo siku hadi siku.

Ng'ombe hao wana thamani ya Sh. 413,600,000 ikiwa kama kila ng'ombe atakuwa na kilo 220 na kuuzwa kwa Sh. 5,000 kwa kilo moja.

"Kamati tumeona hamstahili kupewa fedha hizi kutokana na kushindwa kwa menejimenti, fedha nyingi imepotea na mifugo pia imepotea, hatupendekezi mpewe fedha hadi mbadilike," aliagiza Filikunjombe.

Mwenyekiti wa Bodi ya NARCO, Salum Shamte, aliieleza kuwa shirika linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa mtaji wa kujiendesha, miundombinu duni jambo ambalo ni gumu kutengeneza faida.

Alisema Narco ilichukua mkopo katika benki ya CRDB ambako riba ni kati ya asilimia 16 na 18 na kwmba kwa mkopo wa Sh. milioni 400 walilipa Sh. milioni 700 na kwmaba mkopo wa benki ya TIB ni wa kununua ng'ombe na kunenepesha ambao hauwezi kulivusha shirika hilo.

Shamte alisema ujenzi wa machinjio ulisitisha baada ya kuingia mkataba na Suma JKT ambao walijenga chini ya kiwango na kuvunja mkataba nao na kwamba ujenzi utaendelea siku za karibuni na unatarajiwa kukamilika mwakani.

Baada ya maelezo hayo, kamati hiyo iliagiza Msajili wa Hazina kupitia taarifa ya uchunguzi ya CAG akishirikiana na Wizara na kuchukua hatua kwa kipindi cha wiki tatu.

Pia, Bodi ya NARCO ijitathmini iwapo menejimenti ya Narco Taifa na Ruvu, zinastahili kuendelea kuwepo na umri wa kustaafu ni miaka 60, lakini Mkurugenzi Mkuu ana miaka 61. Mwenyekiti wa Bodi pia ametakiwa kujitathimini kama anastahili kuendelea kuwepo.


CHANZO: NIPASHE
 
hizi porojo ndio Mzanaki (Nyerere) alizikemea kwa nguvu zake zote - mnasema mnajiendesha kwa hasara bila ufafanuzi halafu ranchi hizo hizo wakipewana sio kuuziwa watu binafsi zinajiendesha kwa faida - kuwepo kwenu kuna faida gani kama sio kuwa mzigo kwa taifa.

Halafu hizi bodi ni watu vibogoyo waliochaguana kwa kuelewana na sio Weledi. mwenyekiti Shamte ni mzuri lakini anaponzwa na uswahili wake - maneno mengi matamu.
 
Tupa kule kama hawawezi! !!!
Wamekopa 400 wamelipa mia 700 faida ilikuwa ngapi!!??
 
Tatizo la NARCO ni meneja mkuu aliyepo. aliingia kampuni ikiwa na zaidi ya ng,ombe 35,000 kwa sasa kampuni ina ng'ombe 14,000. Karibia ng'ombe 20,000 wamepungua chini ya uongozi wake. Dawa yake ni kumg'oa huyu meneja mkuu na kuteua mamaeja wa ranchi wa ndani ya kampuni ambao wanajua vizuri hali ya kampuni.
 
hili shirika linapendwa sana na wafanyakazi wa serikali hawajiendeshi kifaida kabisa typical mfano wa shirika la umaa amblo hamna anayejali fika bucha la nyama lao pale clock tower unaweza panga folen masaa 2 hupati nyama tena unataka kununua kwa cash hapo ni mfululizo wa magari ya serikali ya wizara na ofisi mbali mbali wanakuja chukua nyama za mabosi wao ambao wanapewa kwa mkopo wa ofisi na hizo ofisi nyingi i am sure hazilipi mwisho wa cku ilo deni?

kipindi cha sikukuu huwez pata nyama kabisa kwa sie wateja wa kawaida ambao infact tunataka nunua kwa cash, nyama zote ni zinakwenda wizara na ofisi za serikali tu ni kama mfugaji anayechinja wanyama kwa matumizi ya familia yake hamna dalili yoyote ya kujiendesha kifaida, ktk mashirika yaliyotakiwa kubinafsishwa kwanza kwanza hili ni mojawapo ila linatumika sana kula ela ndo mana watu wanabakisha ulaji!!!
 
Back
Top Bottom