Jamani, hii gemu ya Serengeti boys dhidi ya Niger imekwisha, tumefungwa 2-1, Mimi nilijua tutafungwa hasa baada ya kumsikiliza kocha Mkuu Bakari Shime mipango yake juu ya hii mechi. Alisema kwamba Niger watashambulia sana kwa sababu wanahitaji lazima washinde ili waingie nusu fainali, sisi tulihitaji sare tu ili tusonge nusu fainali na kisha tupate tiketi ya kushiriki kombe la dunia la vijana kule India.
Kichekesho ni kwamba kocha mkuu Shime akasema watacheza kwa kujihami zaidi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza, hilo tayari lilukuwa kosa kubwa sana kwa sababu njia nzuri ya kujilinda siku zote ni kushambulia na si kujilinda.
Tatizo kubwa lilikuwa kipindi cha kwanza, Serengeti boys hawakucheza mpira wowote zaidi ya kujilinda na kufanya mashambulizi machache sana, hii ilisababisha Niger kutushambulia na kupata bao la kujifunga wenyewe.
Funzo, waangalie Mali, tulikuwa tunalingana kwa pointi lakini wao hawakwenda kujihami kama sisi na wamepata matokeo mazuri kwa kuishinda Angola bao 4-0, sisi tulihamka kipindi cha pili, hata hivyo tulishachelewa kwani wale wachezaji wazuri Kama Nkomola walikuwa bench, sijui kwa nini? Lazima tujirekebishe, huwezi kubadilisha fomesheni na kuwaacha wachezaji wazuri bench wakati bado hujafuzu.