Ngoma za siasa zisizojulikana... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngoma za siasa zisizojulikana...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanamageuko, Jan 5, 2011.

 1. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Watanzania!

  1992 watu walitoka UT na kuanzisha vyama vya siasa ili kukidhi matakwa ya wafadhili. Na baadhi wakatoka TANU nope CCM kuanzisha ama kujiunga na vyama hivyo. Kikubwa hapa ni kwamba hayati Mwalimu ndiye alieshauri jambo hilo na likawa. Vyama KIINI MACHO vikaanzishwa na vimeendelea kuwepo bila malengo yake kufa ama kubadilishwa (VYAMA VIINI MACHO KWA WAFADHILI) na katika mfumo wa vyama hivyo ambavyo vipo kwa ajili ya... Watanzania walio wengi tumeendelea kuimbishwa na kuimba nyimbo ambazo hatuzifahamu na mwisho wa siku tunabaki kulalamika kuwa tumeonewa na wale wahusika tunaowatetea mda huo wako kimya wakila kuku. Tutaendelea kupata machungu na nyoyo kuuma kama tutaendelea kutaraji vyama hivi,

  tutaendelea kusikia machungu na taarifa tusizozipenda ikiwa tutaendela kukumbatia vyama hivi...

  mpaka siku tutakapojua kuwa tunachezeshwa kilua kwenye ngoma ya kimasai! muda utakuwa umekwenda na vizazi vitatuhukumu.

  Ahsanteni sana.
   
 2. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,293
  Trophy Points: 280
  Na katika kuthibitisha hilo: Mara zote chama kimojawapo kikianza kupata nguvu na kubadili uelekeo basi hapo songombingo na mashaka huanzishwa kwa makusudi maalumu ili chama kile kipate sura tofauti miongoni mwa watu, na miongoni mwa mapandikizi huhamia vyama vingine ama hurudi walikotoka wakipeleka maneno tofauti na matamshi yao ya awali. Wote mnajua nini kinatokea katika siasa za vyama vyetu vya upinzani iwe CHM, CUF, NCCR, TLP na hata vile ambavyo havina anuani!
   
Loading...