X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,344
- 14,120
Ni zahiri kuwa madawa ya kulevya ni mabaya na yametuharibia sana ndugu zetu, lakini hakuna asiyejua kuwa mtandao wa madawa ya kulevya haukuanzia tu nchi hii, inaaminika kuwa kila sekunde inapoisha wauzaji wa madawa ya kulevya wanaingiza zaidi ya bilioni. kwa mtazamo huo unapoanzisha vita dhidi ya mtandao huu hatari inatakiwa uwe umejikamilisha katika nyanja zote, nitakuwa mchoyo wa fadhira endapo nitashindwa kumpongeza kijana mwenzangu PAUL MAKONDA kwa ujasiri wake mkubwa wa kuingia katika vita hii kubwa ambayo watu wenye akili sawa sawa walipambana miaka kwa miaka kumkamata mtu mmoja. lakini kwakuwa tumeshazoea kuona kuwa ngoma za watoto siku zote huwa hazikeshi, sitochelewa kusema kuwa harakati hizi za MAKONDA zitazimika kama mwenge unavyozimwaga, na hii yote ni kwakuwa MAKONDA anajijua kuwa yeye bado ni mdogo ki uongozi na kwa makusudi anaamua kupiga ngoma ya kitoto tena akajisahau kuwa anaowapigia ngoma hiyo ni watu wazima waliopevuka kiakili, leo hii ata mtoto mdogo ukimchapa lazima atakuhoji juu ya kile unachomuadhibia na mtoto huyo ataenda mbali sana kudai visibitisho...iweje leo MAKONDA kwa makusudi ameamua kutufanya watanzania hatuna akili eti pasipo kisibitisho, kwa kutumia uenyekiti wa kamati ya ulinzi alionao, pasipo kukaa chini na kujipanga anawashutumu watu kuhusika katika janga hili la madawa ya kulevya. ata kama mimi eddy_mhando Ningekuwa nahusika na hiyo mivitu lazima ningebisha kuwa sihusiki kwa mfumo huo anaoutumia makonda...mimi nadhani makonda amelewa sifa....
JESHI LA POLISI LATOLEWA KAFARA
nalipenda sana jeshi la polisi kwani ndilo haswa lililosababisha hali ya usalama nchini mwetu ikawa salama kama ilivyo, nakumbuka miaka ile enzi za mwalim {JK} polisi walitumika kwenda kuwakamata ndugu zao wanajeshi wa jwtz waliotaka kuipindua nchi, hivyo polisi ni miongoni mwa vyombo vyenye historia ya kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. polisi huwa hawakurupuki lakini nashangazwa sana na tukio hili polisi wanalazimishwa kukurupuka jambo ambalo ata wao wanajua kuwa wanavuruga ushahidi na mwisho wa mchezo hakuna yeyote atakaye kamatwa na visibitisho na mchezo utakuwa umeishia hapo. mimi niwaombe tu polisi wafanye kazi kwa kufuata taratibu walizofundishwa kwenye shule za kipolisi. polisi nyie ni wafanyakazi wa muda mrefu serikalini najua kuna baadhi yenu mlifanya kazi ya upolisi tokea enzi za Nyerere, japo Nyerere aliachia madaraka lakini nyie bado mpo hadi leo nadhani hiyo ni kutokana na weredi wenu wa hali ya juu kiutendaji, hivyo nawasihi sana polisi msithubutu kufuata matakwa ya mtu asie na weredi wa kipolisi atalichafua jeshi lenu na atakuja kusababisha mje kudharirika kama si kuzarauliwa, polisi msifuate wanasiasa wao wamechaguliwa na watapita kuwaacha mkiwa bado mnatuhudumia wananchi, hivyo ni budi yenu polisi kufanya kazi kwa kushirikiana vizuri na wananchi.
eddy_mhando nitakuwa nyuma ya kiongozi yeyote mwenye nia nzuri ya kupambana na biashara hii haramu, nipo teyari kushirikiana na kiongozi yeyote kuhakikisha tunaitokomeza biashara hii hatari ya madawa ya kulevya lakini tu kwa kufuata haki na taratibu za kisheria.