Ngoma ya escrow kumbe ni standard chartered


Ndio maana nasema kidumu chama cha mapinduzi

Tumekuwa na viwanda vya nguo vingi tu...Sunguratex...mwatex...urafiki

Tumekuwa na kiwanda cha magari Nyumbu na ndio magari yanayotumika zaidi Tanzania

Tumekuwa na Surplus Balance of trade kwa miaka yote ya utawala wa CCM....

Tumewachukulia hatua wezi wote wa Richmond,Deep Green ,Kagoda na Meremeta

Ni chama chetu CCM kimeibua hoja ya Escrow ya IPTL na ndio kinaisukuma ajenda ijadiliwe bungeni

Ni CCM hii uchumi umekuwa kwa double digit tangu kipindi cha kupata uhuru.....

Ni ccm hii chini ya Kikwete tumeingia mikataba mingi na nchi za nje na mikataba hio tumeiweka wazi #Open Government initiative
 
Hata zingekuwa za NMB ndo zichotwe tu kienyeji!!!? maelezo mareeeeefu hamna hoja hapa
JMAil umeandika maneno mengi pasipo hoja za msingi, ulisoma gazeti hukuelewa inawezekana unatumika pia kufagilia hao wahaya wezi.
 
Last edited by a moderator:
Ukweli suala la IPTL/ESCROW ni vita ya Maslahi ya mashirika ya kibepari katika vita ya kuhodhi shughuli za Gasi na Umeme na upande mwengine Ustawi wa Mabanki yao kama Standard Chartered Bank kama financiers wa Mradi wa IPTL.Pia imeingiliwa na kambi za kisiasa za ndani ya CCM kutoka wagombea watarajiwa wa urais kunyumbuana na pia kambi ya upinzani nao kuona huo ni mwanya wa kipekeee kuisulibisha CCM na kui punguzia Points za 2015.
Pia ni eneo lilio ingiliwa na Wajasiramali wetu walokosa vitalu kutokana na kuwa wao ni madalali tu wa hivyo vitalu ambao wamekereka kupewa vitalu bure na sasa nao wanatumia nguvu zao zote kukomoa na kuhakikisha wabaya wao wanaondoka.
Sasa vita inapiganwa na maslahi tafauti na ukweli umekua haujulikani tena kila mtu na jipya , kila siku porojo jipya, ni waatu na maslahi yao kila mmoja na kamba yake.
Pia Hii vita ya gas na mafuta. Makampuni ya kibepari ya gas na mafuta ni ya kimafia yanatumia mbinu chafu na za kutunga ili kuhakikisha hakuna mtu binafsi au makapuni ya nchi za South wanapata tenda za miradi mikubwa ya uzalishaji umeme na gas Tanzania.
Wiki ilopita walidiriki hata kumfachafua Rais wa china ati ndege yake imepakia pembe za Tembo.
Hizi kampuni za kimafia pia wanatumia Rushwa kuwahonga baadhi ya wana siasa wa upinxani kuleta fitina na shutuma dhidi ya kampuni yoyote ile inayo hatarisha maslahi yao .
Tayari madalali wa ma kimafia wapo kazini kuhakikisha IPTL ina sulubiwa na hatimaye isitishwe kuzalisha umeme rahisi na mwisho wa siku wata inunua wao mitambo kama walivofanya katika suala la Richmond na Dowans.
Moja ya mambo ambayo Serikali na CAG TISS pamoja na Takakuru inapaswa kuangalia ni mwenendo wa wana siasa wa upinzani mahusiano yao na makampuni ya kibepari ya kimafia.
Wapo wanao tumiwa kuyumbisha uchumi wa nchi aidha bila ya kujijua au kwa kupewa rushwa hivyo vyombo vyetu viende mbali zaidi kuwa chunguza ikiwezekana maongezi yao yote ya simu na internet na nani wanakutana nao.
Ikumbukwe balozi wa uingereza ndie alie chochea suala kusitishwa misaada kwa vile kuna bank yao ya kimafia ya Standard chartered katika mkataba wa IPTL hivyo wao walitaka hizo fedha walipwe wao. Sio kuwa hazistahili kulipwa bali wangepewa standard chartered kulipa deni.huku ikijua deni hulipwa kwa mujibu wa mkataba.
Hivyo hizi fedha wangepewa benki hii ya kifree mason bas kusingekuwa na wizi wala kusingekuwa na ku stop misaada.
Wako wanaotumikia maslahi ya banki hii kwa kujua au kuhongwa
Wako wanamtumikia mjasirimali mkubwa aidha kwa kutojua au kuhongwa
Wako wanafanya kwa kukosa chenji baada ya kuuomba
Wako walo nyuma ya Mamvi
Tuombe hii ripoti isomwe yaishe. Kwani hio ilo vuja inaonesha mgogoro ulivo anza namna fedha zikawekwa escrow kwa lengo gani na mwisho inaonesha namna taratibu zilizo tumika kuzitoa pesa hizo kw
 

Siku zote hicho ndicho Kafulila anacho pigania, fedha za escrow walipwe SCB-HK. Ila kuna vilaza humu wasiojua kuunga Dots hawalioni, wala hawatokuja kuona hili.
 
misaada imesitishwa,kudos baba mwanaasha division four!
 
nina maana kama taarifa hiyo ni sahihi nasi huku hasa wanasiasa na wapambe wa humu tunarushiana makombora bila kuwa na facts ili kuridhisha mitazamo yetu kisiasa

Said Sabke.

Ni kweli ndugu yangu,wanasiasa walio wengi huwa wanafanya mambo mengi kwa masilahi yao binafsi wala si kwa wananchi kama wanavyosema wakati wa kuomba kura,ni wanasiasa wachache sana ambao hawajitoi ufahamu na wanafanya mambo kwa niaba ya wananchi.
 
hakuna kafara escrow akaunt. Tusiwaingize watu wasio na hatia. Bora lisijadiliwe
 
hakuna kafara escrow akaunt. Tusiwaingize watu wasio na hatia. Bora lisijadiliwe
 
Naam, nilijuwa siku nyingi kuwa kuna siku misaada itasitishwa na ntafurahi sana kama itaendelea kusitishwa.

Ni wakati muafaka tukaanza kujitegemea.

Ala kumbe yale ya awamu ya kwanza yalikuwa mazuri, naelewa tatizo ni kuwa kiongozi wa awamu hiyo hakuwa wa dini yako, angekuwa wa dini yako ungempa misifa kem kem, lakini kwa vile bahati mbaya ni wa dini nyingine huwa kila mara unamponda. UDINI UDINI UDINI utakumaliza sister.
 
Anae tetea wezi nae ni mwizi tu. Kama Anna T kavuta mkwanja nae ni MWIZI tusimung'unye maneno. Kwa nini mkuu ukubali kutumika kama toilet paper kusafisha uchafu wa wengine?
 

Dah! kumbe ni kweli kwamba kuna siku kichaa anaweza kuongea jambo la maana!!! leo umekula nini mpaka umekuwa na positive thinking na nchi yetu?
 
Duh utata, mi nashauri tujadili kwanza bungeni, hela zirudi kisha, tuanze kujua hela ni za nani hasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…