Ngoma ya daku siku za mwezi wa ramadhani

Ngoma ya daku siku za mwezi wa ramadhani

BRAND

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2013
Posts
296
Reaction score
260
Nani anaikumbuka hii ngoma ya daku iliyokuwa maarufu miaka ya tisini na kurudi nyuma iliyokuwa ikifanyika nyakati za usiku!

Mimi sio muislam lakini kwa hakika ngoma hii ilikuwa burudani tosha sana kwangu ktk kipindi kama hiki cha mwezi wa ramadhani.

Hasa pale wanapotokea watoto wa uswazi wakiwa full yaani na kinyago chao pamoja na nyimbo maridhawa zilizo jaa manjonjo huku kinyago akicheza kwa ustadi, huku wakipita nyumba kwa nyumba kutoa burudani kwa malipo atakayojiskia mwenye nyumba,

Ni ngumu kunielewa kama wewe sio wa miaka ile au hujawahi kabisa kuishi uswazi

Siku hizi naona digital imetawala sana watu hawana muda huo wapo bize na tv pamoja na smartphones tu.
 
Subiri washindilie ubwabwa watakuja
 
4048337.jpg
 
"ukizubaa zubaa utakula wali bila nazi kuchujaaa,
utangoja uchokozi toka ungujaaa,
daku kulaa daku kulaa. ."
 
Siku hizi wakubwa wanapita mchana wiki la mwisho kukusanya hela kwa huku kwetu usiku hatuwasikii. vipo vitoto vikishalewa uji vinapita hata Saa mbili bado ati daku kulaa
 
Back
Top Bottom