Ngoma azichapa kavu na Tambwe

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,258
NGOMA%2BNA%2BTAMBWE.jpg

Wakati Yanga ikiendelea na harakati za kujiandaa na mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo, ghafla kumeibuka mtafaruku baina ya nyota wa timu hiyo, Mrundi, Amissi Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinadai kuwa wachezaji hao walivurugana na kufikia hatua ya kushikana na kudondoshana chini wakipambana walipokuwa kwenye mazoezi ya timu hiyo huko nchini Uturuki walipokwenda kuweka kambi.

Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi na kudai kuwa ingawa sababu ya ugomvi wao haikujulikana tatizo nini lakini walionekana wakirushiana maneno kabla ya baadaye kuvaana wakati programu ya mazoezi ya kocha Hans van Der Pluijm raia wa Uholanzi ikiendelea.

Imeelezwa kuwa wakati ugomvi huo ukiendelea na Tambwe akishikwa kwa ajili ya kutulizwa ndipo Ngoma alipopata upenyo na kumpiga Tambwe usoni na kusababisha kumpasua katika paji lake la uso.

"Baada ya hapo ikawa tafrani lakini Tambwe ikabidi atibiwe kwa ajili ya kumtuliza maumivu, baadaye kocha akazungumza nao kwa ajili ya kuwatuliza na baada ya pale ishu ikapoa, lakini mpaka wanarudi Tambwe na Ngoma hawakuwa kwenye mawasiliano mazuri," kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, baada ya tukio hilo, Ofisa Habari wa Yanga Jerry Muro alipozungumza na Waandishi wa Habari, juzi Makao Makuu ya Yanga, Kariakoo jijini Dar, alifafanua kuhusu ishu hiyo akieleza kuwa ulikuwa ni msuguano wa kawaida ambao hutokea popote pale wachezaji wanapokuwa mazoezini.

"Hapana, haukuwa ugomvi, ilikuwa ni suala la kuingiliana wakati wanafanya mazoezi, hutokea popote na hasa kwa timu yenye ushindani kama Yanga maana Ngoma na Tambwe walikuwa wanacheza timu mbili tofauti kwa hiyo kuingiliana vibaya kwa bahati mbaya wakati mnachuana ni kawaida na hakukutokea ugomvi mkubwa.

"Tambwe na Ngoma wote wapo kikosi cha kwanza kwa hiyo huwezi sema eti walikuwa na bifu kwa kugombania namba ndiyo maana wametibuana, hapana, ni suala la mazoezini tu," alisema Muro.

Championi Jumatatu lilifanya jitihada za kuwatafuta wachezaji hao kulitolea ufafanuzi suala hilo lakini Tambwe hakuwa hewani kwa muda mrefu na hata alipopatikana hakupokea simu ya mkononi hata baada ya kupigiwa zaidi ya mara mbili.

Ngoma naye alipotafutwa mara ya kwanza alionekana kuongea na simu nyingine, alipopigiwa tena simu yake iliita bila ya kupokelewa.

Hata hivyo, Tambwe alipotua kwenye Uwanja wa Ndege akitokea Uturuki usiku wa kuamkia jana alionekana akiwa na bandeji amefunga usoni, hali ambayo inaonyesha ukweli wa suala hilo.
SOURCE: CHAMPIONI
 
Kama waliingiliana mazoezini basi wasameheane tu,au vipi wana yanga wenzangu.
 
si mlimtema nyie kwa madai kuwa ni mnyemeleaji au mviziaji tu lakini mpira hana???!!!!
Actually, he is. Hebu chunguza mechi za kimataifa jinsi anavyozunguka uwanjani bila tija!
 
Sasa mbona ni pachika magoli mzuri tu????
Ndio maana kocha amemtafuta mchezaji mwingine, ameona huwezi kufanya mipango ya magoli kwa kutegemea uviziaji. Mipango ya goli lazima ionekane inavyoenda hatua kwa hatua. Tambwe haziwezi ligi za makundi zenye giants, labda zile za Comoro na Shelisheli
 
Ndio maana kocha amemtafuta mchezaji mwingine, ameona huwezi kufanya mipango ya magoli kwa kutegemea uviziaji. Mipango ya goli lazima ionekane inavyoenda hatua kwa hatua. Tambwe haziwezi ligi za makundi zenye giants, labda zile za Comoro na Shelisheli

Mmmmmmmh nayaheshimu mawazo/maoni yako....ila kwa maoni yangu siamini kuwa kocha amesajili fowadi mwingine kwa kuwa eti Tambwe hayuko kwenye mipango yake...naamini fowadi mwingine anahitajika ili kutoa uwanja mpana zaidi kwa kocha kuhusu formation anayotumia. Mimi naamini (ningekuwa kocha wa Yanga) ningesajili wachezaji wanne: (1) Beki wa kushoto (2) Defensive midfielder -wa kuprotect defenders pale katikati na hard tackler (3) Wing midfielder anayeweza kukaa na mpira na mwenye chenga kama alivyokuwa Ngasa lakini awe na nguvu na mrefu- lengo likiwa ni kuwachanganya defenders wa upinzani na kutoa pasi murua kwa wafungaji na yeye mwenyewe kufunga (4) Forward mwenye nguvu na mzuri kwa control na pia vichwa na mwenye uwezo wa kurudi nyuma kusaidia ulinzi na mwenye pasi nzuri. Forward huyo ningemweka acheze na Ngoma na Tambwe aka MVIZIAJI. formation yangu ingekuwa 4-3-3 au 3-5-2 (katika hao wawili mmoja ni huyo mviziaji Tambwe) au 3.4-1-2 (katika hao wawili mmoja ni MVIZIAJI Tambwe)
 
Back
Top Bottom