Ngoja tuwatetee ma hausi geli

Waterlemon

Senior Member
Sep 2, 2016
137
178
Naona kila ukifunua kurasa za JM siku hizi kelele mno kwa ma hausi geli. Mara oooo, wanavunja ndoa za watu, mara wanakuwa ni marupu rupu ya mabwana mwenye nyumba, mara.... yaani hata hawapewi nafasi hata ya kumeza mate.

Kwani nao hao ma house girl si watu? Naona ma h/g wamevaliwa vibwebwe siku hizi... Waachieni bhana. Mtu hakeshi kwa bahati ya mwenzie... sasa na hao ma house girls hope waitoe wapi kama sio ya kupindua?

Kama limama lenye nyumba limejiachia mpaka kupinduliwa na house girl, basi linastahili hilo na wala pole halipewi.

Na kwa mabwana wenye tamaa za kutaka kutoovyea na kudokoa ma house girls wakati wanapewa vya kutosha na wake zao... wakikabwa na matonge kooni, na wala wasionewe huruma.... wacha mimacho iwatoke kwa kupaaliwa.

Waachieni bhana... ma house girl nao wapo katika profession kama wengine. Mbona siskii masekretari wakishambuliwa na wao hao kiboko katika kujipendekeza na kupapasa papasa ndevu za wakuu wao ili wanyakue manono manono yenye faida kwao!!!

Representing!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom