Ngoja niwaambie ni Nini kimeiangusha Barcelona ungana nami niwajuze

Ramsy Dalai Lama

Senior Member
Apr 5, 2021
147
540
Barcelona ilikuwa klabu ya kwanza katika mchezo wowote kuingiza $1bn katika mapato ya kila mwaka lakin kwa sasa ina deni karibu $ 1.4bn na hii katika miaka ya karibuni. Barcelona imekuwa katika misimu yote mibaya baada ya usiku wa Berlin mnamo Juni 2015 iliposhinda fainali yake ya nne ya Ligi ya Mabingwa ndani ya miaka 10. Klabu hii ilikuwa imefanikiwa kutawala kwa muda wa miaka 10, shukrani kwa kizazi kimoja cha wanasoka mahiri kutoka katika academy yake ya vijana (La masia). kwa kipindi chote hicho Barca iliweza kumudu kusajili karibu kila mchezaji kwenye soka duniani. Katika mafanikio ya biashara yoyote ile ikija suala la management, basi "kuajiri" ni kitu muhimu kuzingatia na kuwa nacho makini ili kuwa na watu sahihi kwenye management. Lakini Barcelona walipoteza "vita" kwasabab yakutozingatia hili.

Ni nini kilienda vibaya? Mchakato wa Barca wa kununua wachezaji ni mbovu isivyo kawaida. ndani ya management ya timu kila mtu alikua ana sauti ikija suala la usajili wa wachezaji na ukajitokeza upinzani na mvutano wa nani asajiliwe na ikafika wakati wanasajili mchezaji mara nyingi bila kujisumbua kumjulisha kocha mkuu. Aliyesimamia sera mbaya ya usajili ndani ya Barcelona kati ya 2014 na 2020 alikuwa Josep Maria Bartomeu. Mwanachama mwenye urafiki ndani ya management ya barca, na ni mfanya biashara maarufu Spain anayesimamia kampuni ya familia inayotengeneza Passenger Boarding bridge ambayo huchukua abiria kutoka ndani ya kituo na kuingia kwenye ndege. Mnamo Januari 2014, akiwa makamu wa rais wa Barca alishikilia kwa muda kiti cha urais baada ya aliyemaliza muda wake, Sandro Rosell, alipojiuzulu. Bartomeu alichukuliwa kuwa mtunzaji tu wa nafasi ya urais. Hata hivyo, Julai 2015, mwezi mmoja baada ya ushindi huo huko Berlin, wanachama wa klabu wenye shukrani walimpa ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa rais wa Barca.

Baada ya kuwa rais rasmi, tatizo lilikuja kwamba hakuwa mwenye kuijua sana biashara ya soka. Ila kwa bahati tu ni kwamba kwa wakati huo mkurugenzi wake wa michezo, alikua golikipa mashuhuri wa Spain Andoni “Zubi” Zubizarreta, na alikuwa amesajili wachezaji kama Neymar na Luis Suárez, ambaye alishirikiana na Messi kwenye safu ya ushambuliaji ya “MSN”, bora zaidi katika soka. Lakini cha kushangaza Bartomeu alimfukuza Zubi. na haikuishia hapo bali alifukuza wakurugenzi watano wa michezo katika miaka sita. Na huo ndo ulikua mwanzo wa kushuka kwa Barcelona na kuanza taratibu kupoteza Ufalme wake.

Ukiachana na hilo kushuka kwa Barcelona kulianza kwa kumpoteza Neymar. Mbrazil huyo alikuwa winga mwenye uwezo wa hali ya juu ambaye alikimbilia pasi za Messi. Utengenezaji wa magoli (xG) ni kipimo cha upimaji idadi ya mabao ambayo timu inaweza kufunga kulingana na ubora wake wa nafasi. So katika msimu wa 2015/16, Neymar peke yake alichangia 1.2 xG kwa kila mchezo, nyuma kidogo tu ya Messi 1.4. Lakini cha kushangaza Neymar mnamo 2017, alijiunga na Paris Saint-Germain (PSG) kwa ada ya uhamisho ya €220m, ambayo ilikua rekodi ya dunia. Na tangu hapo Barcelona hawakuwahi ku replace nafasi yake.

Mwaka 2017, wakala wa Uhispania Junior Minguella aliipatia bodi ya Barcelona mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappé mwenye umri wa miaka 18. Lakini Minguella hata hakupata majibu kutoka kwa Barca hadi hatimaye ujumbe wa WhatsApp ulipowasili kutoka kwa mjumbe wa bodi, Javier Bordas unaosema: "Si makocha wala Rais anayemtaka Mbappe". Lakini haikuishia hapo Bordas alisema miaka kadhaa baadaye kwamba management ya kiufundi ya Barca pia ilimkataa mchezaji wa Norwegian Erling Braut Haaland, kwa sababu hakuchukuliwa kuwa "mchezaji wa style ya Barca". Leo hii, Mbappé na Haaland ndio vijana wawili wanaotamaniwa zaidi kwenye soka.

Badala yake Barca walimlenga Mfaransa mwingine, Ousmane Dembélé wa Borussia Dortmund. Bartomeu alijitolea kulipa €105m kama ada ya usajili, pamoja na €42m kama performance bonus. Hii iliku zaidi ya gharama ya Mbappé. lakini miezi sita baadaye, Barca ililipa Liverpool €160m kwa creator wa ki Brazil Philippe Coutinho. Ada ya uhamisho ya Neymar ilikuwa imetumiwa yote, na wakaongeza na zaidi. Lakin si Dembélé wala Coutinho waliofanikiwa Barca. huenda ni kutokana na wasiwasi uliopo katika kujiunga na klabu hii.

Barca ilianza kununua wachezaji kwa bei ya juu pengine mara mbili ya bei ambayo timu ilitarajia kupata katika kuuza mchezaji, na kuthibitisha hili, Mapema ya 2019, Barcelona ilianza kumkimbizia kiungo mchanga wa Ajax Amsterdam Frenkie de Jong, shabiki wa Barca tangu utotoni. Alikuwa na wasiwasi kwamba hatajiunga na timu. Lakini Barcelona ililipa Ajax ada ya uhamisho ya €75m. Kulingana na wakala wa kandanda Hasan Cetinkaya, akiishauri klabu hiyo ya Uholanzi, hii ilikuwa karibu mara mbili ya kile Ajax ilitarajia kupata hapo awali. Cetinkaya alisema: “Kulikuwa na shinikizo kubwa kwa wasimamizi wa michezo wa Barcelona ili kufanikisha mpango huo, kwahiyo waalitaka kumsajili kwa gharama yoyote ile.” kwa hiyo Barca ilizoea kulipa kupita kiasi.

Mapema majira ya joto 2019, Neymar alimtumia ujumbe Messi kusema anataka kuondoka PSG. Messi aliona nafasi ya kurekebisha makosa ya Barcelona ya 2017. Alijibu: "Tunakuhitaji kushinda Ligi ya Mabingwa." Alimwita Bartomeu na kumjulisha. Lakini Barca ilimtazama Neymar aliyekuwa na majeraha, mpenda raha, mwenye umri wa miaka 27 na kuamua haitalipa ada ya PSG ya takriban €200m.

Kufikia wakati huu, Barcelona ilikuwa inaishiwa na pesa kwasabab ya matumizi mabaya ya fedha ndani ya club na kwa kiasi fulani kwa sababu ya kufanya manunuzi mabaya pamoja na nyongeza ya mishahara. Kwa Mfano kati ya 2017 na 2021, Messi alipata jumla ya zaidi ya €555m, kulingana na dondoo kutoka kwa mkataba wake wa kurasa 30 uliochapishwa katika gazeti la El Mundo. lakin sio Messi tu bali kila Messi alipopata nyongeza, wachezaji wenzake walitaka waongezewe pia.

Mshahara wa Messi hatimaye uliwafanya Barcelona kushindwa kumnunua mchezaji ambaye Messi alikuwa anamtaka zaidi. Barca ilitumia msimu wa joto wa 2019 zaidi au kidogo kujifanya hadharani kutaka kumsajili Neymar, ili hatimaye iweze kurudi na kumwambia Messi, "Samahani, tulijaribu kila kitu lakini hatukuweza kumpata." kwa hiyo badala yake Barcelona ililipa Atlético Madrid €120m kwa Antoine Griezmann, Mfaransa mwenye umri wa miaka 28 ambaye aliikataa klabu hiyo mwaka mmoja kabla. Ilikuwa ada ya rekodi kwa mwanasoka mwenye umri wa zaidi ya miaka 25. Pia iliwatajirisha wapinzani wa Barcelona Atlético zaidi.

Uwindaji wa Barca wa kumtafuta Neymar haukuweza kumdanganya Messi. Alipoulizwa kama klabu ilifanya kila iwezalo kumpata Mbrazil huyo, alijibu, “Sijui . . . sio kila kitu kiko wazi sana. ” Alipoulizwa kama anaendesha klabu, alikanusha kama kawaida yake: "Ni wazi kwamba sielekezi mambo, mimi ni mchezaji tu, sina maamuzi kwenye team, management ndio yenye maamuzi"

Mfanyakazi wa klabu ambaye amefanya kazi na Messi tangu kwanza mwaka 2004. Aliwahi kusema kwamba. "Messi anajua anaweza kumtoa mtu yeyote Barca. Lakini hapendi uhasama na mtu - yeye ni mtu mzuri. Lakini anajua ana uwezo huo” Wakati Messi aliposhindwa kwenye pambano, mfanyakazi huyo alisema, hatasema chochote zaidi ya kuandika katika notebook yake inayoelezea maisha yake.

Na kushindwa kumnunua Neymar ilikuwa pigo kubwa zaidi kwa Messi ndani ya Barca na iliingia kwenye notebook yake. Hakuweza kumsamehe Bartomeu. Messi hakutaka kuingilia utawala na angependelea wakurugenzi na makocha washughulikie kila kitu - lakini mradi tu wangenunua wachezaji wanaofaa Barcelona.

Kwa jumla, Barcelona walitumia zaidi ya €1bn kwa uhamisho kati ya 2014 na 2019, zaidi ya klabu nyingine yoyote ya soka, lakini kama mlinzi mkongwe Gerard Piqué alikiri, "Kila mwaka tulikuwa wabaya zaidi." Na ukiangalia, kwa mfano Barca ilisajili wachezaji wengine ambao Barca haikupaswa kuwasajili kama; Lucas Digne – €16.5, Thomas Vermaelen – €18m, Andre Gomes – €35m, Martin Braithwaite – €18m, Malcom – €41m, Arda Turan – €34m, mpaka Douglas Santos na Kevin-Prince Boateng hawa wote hawakuweza kufit Barcelona

Kufikia Januari 2020, wakati Barca ilipohitaji mshambuliaji kuchukua nafasi ya Suárez aliyekuwa majeruhi, klabu hiyo ilipunguza bei ya ununuzi. Mkurugenzi wa michezo Eric Abidal aliwasiliana na mawakala wa Cédric Bakambu, fowadi wa Kifaransa na Kongo huko Beijing Guoan. Bakambu alipopigiwa simu ambayo kila mwanasoka anayesafiri ana ndoto yake, aliruka kwenye ndege hadi Hong Kong, kutoka ambapo angeweza kupata ndege hadi Catalonia.

Alikaa macho kwa furaha wakati wa saa nne kwenda Hong Kong. Wakati ndege ilipokuja kutua mara message ilingia kwenye simu yake na ulikua ujumbe kutoka kwa Abidal ukisema: Barca ilikuwa imebadilisha mawazo yake. Badala yake klabu hiyo ilimsajili mchezaji tofauti, ambae ni Mdenmark Martin Braithwaite, kutokea Middlesbrough katika michuano ya Uingereza.

Bado ununuzi wa ajabu wa enzi ya Bartomeu ulikuwa Matheus Fernandes. Mnamo Januari 2020, Barca ilimsajili kiungo wa akiba asiyejulikana mwenye umri wa miaka 21 kutoka klabu ya Brazil Palmeiras. Ada ya uhamisho ilikuwa €7m, pamoja na €3m katika nyongeza. usajili wa Fernandes ulikua usajili wa siri. Barca haikuwahi kumpa official presentation. Na walimpeleka kwa mkopo Valladolid B, ambapo alicheza mechi tatu tu, alirudi Camp Nou na akapewa shati ya "Covid" nambari 19, ambayo hakuna mtu mwingine aliitaka. Msimu uliopita alicheza dakika 17 katika kikosi cha kwanza na hakuna aliyeweza kujua ni kwa nini Barca walimnunua.

Mkurugenzi wa michezo wa Palmeiras, Alexandre Mattos, alieleza baadaye kwamba kwa namna fulani alimshawishi Abidal kuja kuona wachezaji wa akiba wa klabu hiyo wakifanya mazoezi. "Wakati huo, uongozi uliniita kichaa na kusema: 'Unataka kumuuza mchezaji wa akiba wa Palmeiras ambaye tena hachezi sana, kwa Barcelona?'” Lakini cha kushangaza alifanikiwa kumuuza.
Acha tu nicheke kwa kweli halafu mtu anashangaa Messi kugombana na Abidal.

Kufikia majira ya joto 2020, kukosekana kwa fedha ya usajili Barca ilikuwa ikimsumbua Bartomeu na wajumbe wake wa bodi. Chini ya sheria zinazosimamia vilabu vinavyomilikiwa na wanachama wa Uhispania kama vile Barca, wakurugenzi walilazimika kulipa hasara kutoka katika mifuko yao. Bodi ilihitaji kuorodhesha faida haraka kabla ya mwaka wa fedha kuisha tarehe 1 Julai. Na kwa hivyo mpango wa kubadilishana wachezaji ambao ni wa ajabu kuwahi kutokea ukafanyika na wakakubaliana na Juventus, ambayo pia alikuwa na hamu ya kuboresha vitabu vyake vya mapato na matumizi ya mwaka. Juve "ilimuuza" kiungo wa Bosnia Miralem Pjanic kwenda Barca kwa ada ya €60m, wakati Barca ilimuuza kiungo wa kati wa Brazil Arthur Melo kwa Juve kwa €72m. Kiasi ya fedha hizo hakikulipwa kamwe. Zilibuniwa tu kwa madhumuni ya uhasibu. Kilichojalisha ni kwamba ubadilishaji huo ulisaidia kusafisha vitabu vyao. Lilikuwa ni jambo zuri kwa bodi ya Bartomeu, lakini si kwa Barca.

kikosi cha barca chenye wazee kilimpata mchezaji mwingine mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni Pjanic. Baada ya kufikia kuchapwa mabao 8-2 na Bayern Munich kwenye Ligi ya Mabingwa, mzozo wa kifedha wa Barca ulizidi kuwa mbaya. Klabu ilihitaji kuwapunguza wachezaji mwenye umri mkubwa waliolipwa kupita kiasi ambao kulikuwa hawana umuhimu Barca. Suárez, 33, alifahamishwa katika simu ya dakika moja kwamba hahitajiki tena barca. Na mwishoe Alijiunga na Atlético ila Barcelona waliendelea kulipa sehemu ya mshahara wake kutokana mkataba.

Bartomeu anastahili kupongezwa kwa kumsajili Pedri mwenye umri wa miaka 17 kutoka Las Palmas msimu wa joto, kwa ada ya awali ya €5m pekee. Aling'ara kwa Spain katika Mashindano ya Uropa na kucheza fainali ya Olimpiki ya wanaume. Bado, mafanikio hayo hayakuwezi kuzidi mapungufu yote ya Bartomeu. Barcelona ilimaliza msimu uliopita katika nafasi ya tatu katika ligi ya Uhispania, kiwango chake kibaya zaidi tangu 2008. Atlético Madrid ilishinda taji hilo, hasa kutokana na zawadi ya Barca ya Suárez. Raia huyo wa Uruguay alifunga mabao 21 kwenye ligi, na ndiye mshambuliaji ambaye Barcelona walikosa msimu mzima. Baada ya kufunga bao la ushindi, alikaa uwanjani akilia kwa furaha huku akiipigia simu.

Msimu huu unaweza kuwa mbaya zaidi kwa Barca La Liga na michuano yote kama haitachukua hatua mkakati ili kuirudisha timu kwenye ufalme wake. klabu imeweza kutumia takriban €160m au €200m kwa gharama za wachezaji mwaka huu, chini ya theluthi moja ya kiasi cha miaka mitatu iliyopita. Barcelona ilikua tu hailipi mishahara isiyoweza kumudu bali pia ilikua ikitumia gharama kubwa kununua wachezaji ambao waliishia kutoipa mafanikio club. Barcelona inabidi iirudie La Masia kwa ajili ya kutengeza wachezaji Bora na wenye kucheza style ya Barca ya tiki taka ili kurudisha hadhi yake kama timu. Naona Xavi kaingia rasmi Barcelona ni imani yangu atafanikiwa na nitaeleza kwanini baadae kidogo
 
Ninavyoamini kikosi cha vijana cha sasa cha Barcelona baada ya miaka mitatu kitakuja kufanya makubwa sana. Iwapo hawatauzwa 'watoto' hao wa sasa.
 
mkuu uko sahihi sana ila pia kuhusu ugomvi wa messi na abidal ulianza mda sana coz huko nyuma inadaiwa messi alishawahi kumuita abidal mzoga so hawakuwa wakielewana
Lakin pia kwe baadhi ya sajili ambazo imesemekana walizfny tu bila kushirikisha makocha ni kitu cha kawaida sana kwa barca na madrid management zao mara nyingi hufanya sajili zao kwa vile wanavyoona wao inafaa kwa maslahi ya muda mrefu na kibiashara kuliko kuwashirikisha mkocha ambao ni watu wakupita
Pia huu upigaji wa enzi za kina bartomeu hata watangulizi wao nao walikuwa na habari hizihizi sema tu kpnd hiko barcelona ilikuwa kwe moto hivyo madudu yao hayakuwa sana kwe focus ya watu kumbuka hata kwe kumnunua neymar kuna sarakasizilipigwa mpk kupelekea kesi za uhalifu
Pia yaliyotokea barcelona ndio hali halisi ya clubs nyingi zinazomilikiwa na wanachama watu huzitumia sana kwa mslahi yao binafsi hasa wafanya biashara, bartomeu tenda zote zilizokuwa zinahusiana na club ukifuatilia kampuni zinazowin utakuta zinahusiana nae kwa namna moja ama nyingine na sasa anachunguzwa na polisi ya catalonia
 
Ninavyoamini kikosi cha vijana cha sasa cha Barcelona baada ya miaka mitatu kitakuja kufanya makubwa sana. Iwapo hawatauzwa 'watoto' hao wa sasa.
true ila kazi wanayo ni tofauti sana na kikosi cha kina messi kilipoanza
 
true ila kazi wanayo ni tofauti sana na kikosi cha kina messi kilipoanza
Ni timu ninayoifuatilia sana, nimeona namna Xavi alivyoingia na mipango yake, akikaa pale kwa muda mrefu watafanikiwa sana, maana wale watoto atakuwa amewapika vizuri sana. Halafu ndio maana wamewawekea vipenge vya fedha ndefu sana za kununuliwa kama Pedri na Ansu Fati wamewekewa euro bilioni moja kuondoka. Kwa sasa wasifikirie ubingwa wajikite kutengeneza timu. Na huu utaratibu wa timu kumilikiwa na Wanachama unazingua sana.
 
Haya mambo yanazikumba klabu nyingi tu
Kwenye maisha kuna kupanda na kushuka kwenye tasnia mbali mbali
 
Ni timu ninayoifuatilia sana, nimeona namna Xavi alivyoingia na mipango yake, akikaa pale kwa muda mrefu watafanikiwa sana, maana wale watoto atakuwa amewapika vizuri sana. Halafu ndio maana wamewawekea vipenge vya fedha ndefu sana za kununuliwa kama Pedri na Ansu Fati wamewekewa euro bilioni moja kuondoka. Kwa sasa wasifikirie ubingwa wajikite kutengeneza timu. Na huu utaratibu wa timu kumilikiwa na Wanachama unazingua sana.
ni kweli mkuu mi wasiwasi wangu ni idadi kubwa ya wachezaji wadg wanaoingia kwe system kwa wakati mmoja huenda wengine wakashndwa kupata mazingira mazuri ya kudevelop hatimaye wakapotea, nakumbuka xavi alipoingia kwe timu akacheza na waliomzidi badae wakafuata sergio iniesta messi wakati huo wanaingia wanacheza around kina gaucho etoo so ilikuwa nafuu sn kwao kuingia kwe system bila pressure kubwa, villa alikuja badae, alba alikuja badae tofauti na sasa wakati fati pedri gavi nico mingueza araujo wote inabidi waingie sasa halafu wale senior wao waliopo ndo wamechoka(sergio) na pique amekuwa na performance mbovu hatarim so hawa madogo wanabeba mzigo wote by themselves wengine wakiwa ndo mara ya kwanza kucheza senior team wengine msimu wa pili naona xavi ana kazi sana ila akifanikiwa watatisha sana aisee, nawapenda sana nico gavi fati ila pedri na puig hawanivutii kabisa
 
ni kweli mkuu mi wasiwasi wangu ni idadi kubwa ya wachezaji wadg wanaoingia kwe system kwa wakati mmoja huenda wengine wakashndwa kupata mazingira mazuri ya kudevelop hatimaye wakapotea, nakumbuka xavi alipoingia kwe timu akacheza na waliomzidi badae wakafuata sergio iniesta messi wakati huo wanaingia wanacheza around kina gaucho etoo so ilikuwa nafuu sn kwao kuingia kwe system bila pressure kubwa, villa alikuja badae, alba alikuja badae tofauti na sasa wakati fati pedri gavi nico mingueza araujo wote inabidi waingie sasa halafu wale senior wao waliopo ndo wamechoka(sergio) na pique amekuwa na performance mbovu hatarim so hawa madogo wanabeba mzigo wote by themselves wengine wakiwa ndo mara ya kwanza kucheza senior team wengine msimu wa pili naona xavi ana kazi sana ila akifanikiwa watatisha sana aisee, nawapenda sana nico gavi fati ila pedri na puig hawanivutii kabisa
Kwa hali ya sasa pale Barca utampanga nani zaidi ya hawa watoto, hawana choice kabisa. Na usajili mwingine wa kipuuzi ni Dapay, sioni kama anafiti kwa staili ya Barca, kwani angefiti zaidi kule Real Madrid. Ila nina imani sana na watoto hawa watatoboa tu na hata rais Laporta anaonekana anaweza kuifikisha mbali.
 
Kwa hali ya sasa pale Barca utampanga nani zaidi ya hawa watoto, hawana choice kabisa. Na usajili mwingine wa kipuuzi ni Dapay, sioni kama anafiti kwa staili ya Barca, kwani angefiti zaidi kule Real Madrid. Ila nina imani sana na watoto hawa watatoboa tu na hata rais Laporta anaonekana anaweza kuifikisha mbali.
yeah hamna jinsi pia hamna wa kumpanga zaidi ya hawa madg itabidi tu xavi akomae nao, pia kuhusu depay ni usajili mbovu kabisa hafiti utamaduni wa barca wa team play yy anacheza sn yy mwnyw badala ya kuwachezesha na wenzie km wanavyomchezesha yy, pia wanataka kufanya mistake nyngne kumleta sterling ambaye ni km depay tu ndio maana pep hamtaki kule ni heri wamchukue bernldo silva tu, barca haihitaji wanaokimbia tu km Vilnius sterling depay no
 
akifeli Xavi basi, barca utahangaika zaidi, maana naona wameweka matumaini mengi sana kwa Xavi wakati hajawahi kutana na changamoto za ligi 7 bora za ulaya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom