Ngereja akwamisha kesi ya Godbless Lema

joseeY

Senior Member
Nov 4, 2010
108
17
TATIZO la mgawo wa umeme umekwamisha kesi ya kupinga ubunge wa Godbless Lema, baada ya mawakili wa upande wa wadai, Alute Mughwai na Modest Akida, kushindwa kuandaa na kuwasilisha mahakamani na kwa mawakili wa utetezi muhtasari wa hoja zilizo kwenye hati ya madai.

Akiahirisha kesi hiyo juzi, Jaji Aloyce Mujulizi, aliagiza upande wa utetezi kuwasilisha hoja zao kwa muhtasari ili kutoa nafasi kwa usikilizaji wa awali wa shauri hilo lililofunguliwa na wapiga kura watatu; Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo.

Hata hivyo, mawakili Mughwai na Akida wanaowakilisha wadai hao, aliieleza mahakama kuwa badala ya kuandaa na kuwasilisha muhtasari wa hoja zao juzi, walishindwa kufanya hivyo jana kutokana na umeme kukatika ofisini kwao.

“Ina maana waheshimiwa mawakili hamjafanikiwa kupata fedha za kutosha kununua majenereta kwa ajili ya tahadhari na dharura ofisini kwenu?” alihoji Jaji Mujulizi akikatiza maelezo ya Wakili Mughwai.
Akijibu swali hilo, Mughwai alisema anayo jenereta ofisini kwake, lakini kwa bahati mbaya mafuta yaliisha na hata alipohamia ofisini kwa mwenzake, nako ulikuwa umeme umekatika.

Kutokana na hali hiyo, Mughwai aliomba mahakama kuahirisha usikilizaji wa awali hadi siku nyingine, ili kutoa nafasi kwa upande wa utetezi kusoma na kujiandaa vyema kujibu hoja zao, huku pia akibainisha kuwa atakabiliwa na kesi nyingine Mahakama ya Rufaa kati ya Oktoba 7 na 11, mwaka huu.

Kutokana na mawakili wa utetezi, Method Kimomogoro na Timon Vitalis, kutokuwa na pingamizi kuhusu ombi hilo, Jaji Mujuluzi aliahirisha shauri hilo hadi Oktoba 17, mwaka huu itakapokuja kwa usikilizaji wa awali na kumwagiza Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, George Hubert, kuanza mchakato wa kuomba muda wa kusikiliza na kuamua shauri hilo kutokana na kipindi kilichobaki kisheria kuwa kifupi.

Kwa mujibu wa kifungu cha 115, kifungu kidogo cha V ya sheria ya uchaguzi, shauri linatakiwa kusikilizwa na kuamuliwa ndani ya mwaka mmoja tangu kufunguliwa, hivyo kufanya kesi hiyo iliyofunguliwa Novemba mwaka jana kubakiwa na miezi miwili.

Pia, Jaji Mujulizi aliagiza upande wa utetezi upatiwe nakala ya kumbukumbu na mwenendo wa mahakama tangu kuwasilishwa kwa shauri hilo, usikilizaji na uamuzi wa pingamizi zilizowasilishwa na wajibu madai

Lema na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (CAG), huku msajili akiagizwa kutangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo ya mahakama siku, muda na mahali kesi hiyo itakaposikilizwa.

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
TATIZO la mgawo wa umeme umekwamisha kesi ya kupinga ubunge wa Godbless Lema, baada ya mawakili wa upande wa wadai, Alute Mughwai na Modest Akida, kushindwa kuandaa na kuwasilisha mahakamani na kwa mawakili wa utetezi muhtasari wa hoja zilizo kwenye hati ya madai.

Akiahirisha kesi hiyo juzi, Jaji Aloyce Mujulizi, aliagiza upande wa utetezi kuwasilisha hoja zao kwa muhtasari ili kutoa nafasi kwa usikilizaji wa awali wa shauri hilo lililofunguliwa na wapiga kura watatu; Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo.

Hata hivyo, mawakili Mughwai na Akida wanaowakilisha wadai hao, aliieleza mahakama kuwa badala ya kuandaa na kuwasilisha muhtasari wa hoja zao juzi, walishindwa kufanya hivyo jana kutokana na umeme kukatika ofisini kwao.

"Ina maana waheshimiwa mawakili hamjafanikiwa kupata fedha za kutosha kununua majenereta kwa ajili ya tahadhari na dharura ofisini kwenu?" alihoji Jaji Mujulizi akikatiza maelezo ya Wakili Mughwai.
Akijibu swali hilo, Mughwai alisema anayo jenereta ofisini kwake, lakini kwa bahati mbaya mafuta yaliisha na hata alipohamia ofisini kwa mwenzake, nako ulikuwa umeme umekatika.

Kutokana na hali hiyo, Mughwai aliomba mahakama kuahirisha usikilizaji wa awali hadi siku nyingine, ili kutoa nafasi kwa upande wa utetezi kusoma na kujiandaa vyema kujibu hoja zao, huku pia akibainisha kuwa atakabiliwa na kesi nyingine Mahakama ya Rufaa kati ya Oktoba 7 na 11, mwaka huu.

Kutokana na mawakili wa utetezi, Method Kimomogoro na Timon Vitalis, kutokuwa na pingamizi kuhusu ombi hilo, Jaji Mujuluzi aliahirisha shauri hilo hadi Oktoba 17, mwaka huu itakapokuja kwa usikilizaji wa awali na kumwagiza Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, George Hubert, kuanza mchakato wa kuomba muda wa kusikiliza na kuamua shauri hilo kutokana na kipindi kilichobaki kisheria kuwa kifupi.

Kwa mujibu wa kifungu cha 115, kifungu kidogo cha V ya sheria ya uchaguzi, shauri linatakiwa kusikilizwa na kuamuliwa ndani ya mwaka mmoja tangu kufunguliwa, hivyo kufanya kesi hiyo iliyofunguliwa Novemba mwaka jana kubakiwa na miezi miwili.

Pia, Jaji Mujulizi aliagiza upande wa utetezi upatiwe nakala ya kumbukumbu na mwenendo wa mahakama tangu kuwasilishwa kwa shauri hilo, usikilizaji na uamuzi wa pingamizi zilizowasilishwa na wajibu madai

Lema na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (CAG), huku msajili akiagizwa kutangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo ya mahakama siku, muda na mahali kesi hiyo itakaposikilizwa.

mujuluzi huyu si ndiye aliyeongwa ujaji na baba yake ridhwani ambaye ni mwenyekiti wa taifa wa CCM baada ya kumsomeshea mwanae Uingereza. kama ndiye yeye huyu basi mawakili wakirudi wana paswa kumuomba jaji ajitoe kutokana na conflict of interest. je atalinda maslahi ya mtu aliyempa kazi ya ujaji au atazingatia sheria ? tayari kuna conflict hapo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom