Ngeleja tunaitaji vtendo acha story gazetini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ngeleja tunaitaji vtendo acha story gazetini!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jan 8, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  MHnafikiri mpaka sasa ndie waziri unaeongoza kwa kuandikwa kwenye magazeti yakinukuu kauli zako mbali mbali bila vitendo...kwa kukusaidia tu watanzania usione wamekaa kimya si wajinga wanasikia na kuelewa...kama uko serious na kauli zako imefika wakati wa kufanya vitendo...leo hii kila STATION ya mafuta petrol 1450-1600 diesel 1400-1500.....ni nguvu gani zinazo kuinua na kuinuka kwenda kwenye magazeti na kutangaza kila siku watakiona wasiobadilisha ...kama ni urafiki tunakuomba achana nao angalia majukumu yako....tunajua EWURA wanakula na wenye station za mafuta hilo unalijua nhivyo atupendi kwenda mbali hata kama kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake....tunaomba uo urefu wauangalie vizuri wataua....vizazi vyetu.....

  Wazo langu usikurupuke tena kwenye magazeti kama unapita kila kituo dar unaona 1500 na kukaa kimya.....wacha ama waendelee ama walipizwe faini kama mlivyosema ..ama mnalipishana kimya kimya mil 3...uku mnawaa mbia waendelee...waonneeni huruma watanzania....pia nimesoma unasema petrol 1166 mpaka 1271 embu watangazie petrol ngspi diesel ngapi.....ni hayo tu mh


  WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja amewataka wananchi kuondoa wasiwasi juu wafanyabiashara wanaouza mafuta kwa bei ya juu, kwa sababu baada ya siku chache, serikali itaanza kuwashughulikia kikamilifu.


  "Serikali inakusanya takwimu za bei ya mafuta, zikikamilika, kazi ya kuwachukulia hatua itaanza mara moja," alisema Ngeleja alipohojiwa na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.


  Kanuni ya kuwabana wafanyabiashara hao ilitatangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) na utekelezaji wake utaanza baada ya kutangazwa kwenye gazeti la Serikali.


  Ngeleja alisema wafanyabiashara wanaouza mafuta kwa bei ya juu, hawana njia yoyote ya kujitetea kwa sababu kanuni inayotumika kuwabana ilijadiliwa na kukubaliwa katika kikao cha pamoja kati yao na Ewura na watumiaji wa mafuta.


  Ngeleja alisema kitendo cha kuendelea kuuza kwa bei ya juu zaidi ya iliyopangwa ni kuyasaliti makubaliano waliyoafikiana awali wakati wa kupanga kanuni itakayowawezesha kukokotoa bei stahili za mafuta nchini.


  Alisema kwamba, sababu zinazoendelea kutolewa na wafanyabiasha hao juu ya kuwa na hifadhi ya mafuta ya muda mrefu, hazina msingi bali ni tamaa yao ya kutaka kujiongezea faida.


  Waziri Ngeleja aliwasifu baadhi ya wafanyabiashara ambao tayari wameanza kukubaliana na kanuni hiyo.


  Alifahamisha kuwa utekelezaji wa agizo la Ewura ulianza tangu Januari 5, mwaka huu na kwamba, serikali itaendelea kusimamia maamuzi yake.


  Kauli ya Waziri Ngeleja imetolewa siku moja baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu, kusema hawawezi kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaokiuka agizo la mamlaka hiyo hadi agizo hilo itakapotangazwa kwenye Gazeti la Serikali baada ya kupitishwa na Mwanasheria Mkuu.


  Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi jana katika vituo mbalimbali vya mafuta jijini Dar es Salaam umebaini kuwa petroli ilikuwa inauzwa kati ya Sh1,450 hadi 1,600 kwa lita, dizeli ni Sh1,350 hadi 1,450 na mafuta ya taa Sh 750 hadi 1,100.


  Bei hizo ni tofauti na agizo la Ewura lilotaka lita moja ya petroli iuzwe Sh1,166, diseli Sh1,271 na mafuta ya taa Sh 819.
   
Loading...