SERGIO
JF-Expert Member
- Dec 13, 2012
- 348
- 145
Ngeleja na mchango mkubwa
katika maendeleo ya umeme
Na MWANDISHI WETU
KWA Tanzania, suala la kukatika kwa umeme limekuwa tatizo sugu kwa miaka nenda rudi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za uchakavu wa mitambo na wakati mwingine uwezo wa mitambo iliyopo kushindwa kukidhi mahitaji ya wateja.
Sababu nyingine ambayo imesababisha kuwepo kwa hali hiyo ni utegemezi mkubwa wa maji katika kuzalisha umeme, tofauti na nchi zilizoendelea ambazo zimekuwa zikitumia nyuklia, gesi na vyanzo vinenevyo.
Kutegemea maji, kwa maana ya mabwawa kama Mtera, Hale, Nyumba ya Mungi, Kihansi na Kidatu, kumesababisha wakati mwingine nchi kuwa katika mgawo mkubwa wa umeme hasa kutokana na kupungua kwa kina cha maji kwenye vyanzo hivyo.
Inapokosekana mvua ya kutosha, mathalan, kina cha maji katika mabwawa mengi hupungua na hivyo kusababisha uzalishaji wa umeme kuwa mdogo, hivyo kuleta matatizo kwa watumiaji.
Matokeo ya kukosekana kwa nishati hiyo ni kuongezeka kwa matumizi ya mafuta ambapo baadhi ya taasisi na watu binafsi hulazimika kutumia majenereta, ambayo pia si rafiki wa mazingira.
Baadhi ya viwanda ambavyo vinahitaji kiwango kikubwa cha umeme, hulazimika kufunga shughuli na kuwapa likizo wafanyakazi wao. Matokeo ya kukosekana kwa nishati hiyo ni kupungua kwa uzalishaji kwenye viwanda na hatimaye kushusha ukuaji wa uchumi wa nchi.
Hata hivyo, kiasi cha umeme kinachozalishwa katika mabwawa na vyanzo vinene hakitoshelezi mahitaji yanayotakiwa. Kiwango cha kawaida kinachotakiwa, kwa mujibu wa Shirika la Umeme Tanzania, ni takriban megawati 1,200 lakini kiasi kinachozalishwa ni kidogo.
Kwa mujibu wa TANESCO, umeme unaozalishwa katika mabawa na kiasi kwenye mabano ni Kidatu (megawati 204), Kihansi (Megawati 180), Mtera (megawati 80), Pangani (megawati 68), Hale (Megawati 21), Nyumba ya Mungu (megawati nane) na Uwemba (megawati 0.82).
Jumla ya kiasi kinachozalishwa katika mabwawa hayo ni megawati 561 tu. Kwa takwimu hizo inadhihirisha kwamba mahitaji ya umeme ni makubwa hivyo uzalishaji kwa njia mbalimbali unapaswa kufanyika.
Kutokana na uhaba wa kiasi kinachohitajika, serikali ililazimika kununua umeme kutoka nchi jirani za Zambia (kwa ajili ya mikoa ya Rukwa na Katavi) na Uganda kwa mkoa wa Kagera. Licha ya kununua umeme kutoka maeneo hayo, pia baadhi ya sehemu zimekuwa zikitumia umeme wa jenereta.
Pia ilianzisha mpango mahsusi wa kuzalisha umeme wa gesi wa megawati 102 katika mitambo ya Ubungo, Dar es Salaam, kwa kutumia mitambo ya Songas.
Zote hizo ni jitihada katika kuhakikisha umeme unapatikana ili kuchochoea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Watanzania kutokana na ukweli kwamba nishati hiyo ni muhimu katika uzalishaji.
Kwa sasa kuna mpango kabambe wa kuhakikisha umeme unawafikia hadi wananchi wa vijijini ili kutimiza mpango wa serikali wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini (MKUKUTA).
Lengo la kufikisha nishati hiyo vijijini ni kutokana na ukweli kwamba unaweza kusaidia uanzishwaji wa viwanda vidogo na vya kati ambavyo vina uwezo wa kumkomboa mwananchi wa kawaida kutoka katika umasikini.
MCHANGO WA NGELEJA
Jitihada za sasa zinazoendelea katika maendeleo ya nishati, kwa kiasi kikubwa zimechangiwa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ambaye wakati wa uongozi wake kati ya mwaka 2008 na 2012, kuna mipango mingi aliyoianzisha.
Ili kuhakikisha Tanzania inafikia maendeleo ya uchumi wa kati, alibuni na kuasisi miradi mingi ya umeme kwa kuwa alitambua fika kwamba nishati hiyo ni nguzo kubwa katika ukuaji wa uchumi katika taifa lolote, lililoendelea na linaloendelea.
Katika kufanya hivyo, Ngeleja ambaye kabla ya kuwa Waziri alikuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, alibuni na kutekeleza miradi mingi ya uzalishaji wa umeme katika maeneo mbalimbali nchini.
Miongoni mwa miradi hiyo ni ya Nyakato (Mwanza) ya kuzalisha megawati 60, Kinyerezi (Dar), Somanga Fungu (Kilwa) na Mchuchuma- Liganga kwa ajili ya uzalishaji wa Megawati 600. Lengo la kuanzishwa kwa miradi hiyo ni kuhakikisha uzalishaji wa umeme unafikia megawati 3,000 ifikapo mwaka 2015/2016.
Miradi mingine katika kutekeleza azma hiyo ni kuunganisha mikoa yote ya Tanzania katika gridi ya Taifa kupitia miradi ya North-West Grid kutoka Shinyanga, Geita, Kigoma, Katavi, Rukwa hadi Mbeya na Makambako hadi Songea pamoja na kuimarisha huduma ya umeme kupitia North-East Grid kutoka Dar es Salaam hadi Kilimanjaro.
Pia katika juhudi hizo, mikakati zaidi ya nchi kuwa na umeme wa kutosha iliendelea ambapo chini ya uongozi wake ulianzishwa utaratibu wa kufunga majenereta mapya ya kuzalisha umeme katika maeneo ambayo hayajaunganishwa kwenye gridi ya taifa.
Miongoni mwa maeneo hayo ni Kigoma- Ujiji, Kasulu, Kibondo (yote mkoani Kigoma), Sumbawanga Mjini, Namtumbo na Somanga Fungu, Ngara na Biharamulo mkoani Kagera na Mpanda mkoani Katavi.
Sambamba na hilo, aliasisi mradi wa bomba kubwa la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Mradi huo uliasisiwa mwaka 2009 na utekelezaji wake kuanza mwaka 2012.
Kuanzishwa kwa bomba hilo ambalo liko katika hatua ya kukamilika, kunaleta matumaini ya Tanzania kupata umeme wa uhakika ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa uzalishaji na nchi kufikia malengo ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Licha ya mradi huo, Ngeleja aliasisi mradi kabambe wa usambazaji wa umeme vijijini ambao kwa sasa umepamba moto nchi nzima. Katika mradi huo ulioanzishwa mwaka 2009 na kusimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA), hivi sasa kumekuwa na mafanikio makubwa kwa sababu hasi mwishoni mwa mwaka 2014, asilimia 36 ya Watanzania waishio vijijini wamenufaika na nishati hiyo.
Umeme huo unaosambazwa vijijini ni wa gharama nafuu kwani wananchi wanaunganishiwa kwa sh. 27,000 tu kwa laini za kawaida.
Ili kuhakikisha pia uzalishaji wa umeme unafanyika kwa ufanisi, Ngeleja alisimamia mapitio ya mpango kamambe wa mifumo ya umeme (Power System Master Plan) wa TANESCO kwa mwaka 2009 hadi 2033.
Sambamba na kusimamia mpango huo, chini ya uongozi wake ulitolewa mpango mahsusi wa ushirikishaji wa sekta binafsi katika uzalishaji wa umeme.
Mpango huo uliendana na Sheria ya Umeme ambayo iliondoa ukiritimba wa TENESCO katika uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme nchini.
Katika miradi ya Mchuchuma, Ngaka na Kiwira, kwa mfano, inadhihirisha wazi kwamba ukiritimba wa TANESCO umeanza kutoweka kwani taasisi binafsi zimeanza uzalishaji wa umeme ambao utaingizwa katika gridi ya taifa na kuwanufaisha Watanzania, hivyo kuchochea maendeleo ya taifa.
Kwa mantiki hiyo, unapozungumzia maendeleo ya nishati ya umeme nchini, ni vigumu kumuondoa Ngeleja kwani mchango wake umeonekana dhahiri.
Kwa maneno mengine, maendeleo makubwa katika sekta ya nishati imechangiwa kwa kiasi kikubwa na kiongozi huyo ambaye alibuni miradi mingi ambayo kwa sasa inatekelezwa sehemu mbalimbali nchini.
Source: Majira