Ngeleja ampa siku tatu Mkurugenzi (DED)wa Halmashauri Sengerema

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,734
Mbunge wa Sengerema William Ngeleja ametoa siku tatu kurejeshewa madawati yaliyotengenezwa kwa fedha za mfuko wa jimbo

Agizo hilo amelitoa kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Visent Bushaija kutokana na madawati hayo kusambazwa shuleni bila kukaguliwa na kuwekewa nembo.

Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi huyo amesema hajagawa madawati yaliyotokana na fedha za mfuko wa jimbo bali anagawa madawati yaliyopo katika karakana.

“Hakuna dawati hata moja lililotoka kwenda shuleni, madawati yanayotoka kwenda shuleni ni yale yanayotokana na wahisani mbalimbali pamoja na fedha za halmashauri pekee,”amesema.

By Daniel Makaka, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz.
 
U have made my day jinsi ulivyoandika mkuu maneno yako hapo juu....

Duh nakufananisha kama mtu anayeandika faster faster ili atoke nduki kukimbia fumanizi,
Ah ah ah Jamii forum thank u Baba
Huyo atakuwa anatumia smartphone mpya
 
sasa naye mbona ana kihere here? anapelekaje "mashuleni" wakati mwenzake hajayatia chata lake? hii siyo poa.ayarudishe yatiwe chata halaf yakabidhiwe mbele ya Tv na magazeti.
 
Huyo Ngereja ndio yule alikula Hela za Escrow? Asitishe watu huyo watanzania tunamdai kodi zetu
 
Anataka siku ya kugawa awepo?

Ajipambanue, "wamebarikiwa wale watoao kwa siri, utoapo kwa mkono wa kuume basi hata mkono wa kushoto usijue" nimenukuu japo sikumbuki ni wapi nilipata kuyasikia maneno hayo
 
Kama taarifa hizi ni za kweli Ngeleja atambue kwamba alipokuwa mbunge na waziri ulikuwa wakati mwafaka wa kuonyesha mfano kwa kuhakikisha shule zote jimboni kwake hakuna mwanafunzi anayeketi chini. Kwa sasa atulie aache watu wafanye kazi ya kuwatumikia wanyonge!
 
Mbunge wa Sengerema William Ngeleja ametoa siku tatu kurejeshewa madawati yaliyotengenezwa kwa fedha za mfuko wa jimbo

Agizo hilo amelitoa kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Visent Bushaija kutokana na madawati hayo kusambazwa shuleni bila kukaguliwa na kuwekewa nembo.

Hata hivyo, Kaimu Mkurugenzi huyo amesema hajagawa madawati yaliyotokana na fedha za mfuko wa jimbo bali anagawa madawati yaliyopo katika karakana.

“Hakuna dawati hata moja lililotoka kwenda shuleni, madawati yanayotoka kwenda shuleni ni yale yanayotokana na wahisani mbalimbali pamoja na fedha za halmashauri pekee,”amesema.

By Daniel Makaka, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz.

Ngeleja nae bwana sijui yukoje???? Mfuko wa jimbo si ni hela ya serikali na madawati yanagawiwa shule za serikali sasa chata ina umuhimu gani hadi tupate hasara ya kuyarudisha na kuyasamza tena???? Hata hivyo msimu wa uchaguzi bado sana muda ukifika watakuwa wamesahau kama mfuko wa jumbo kupitia mbunge ulitoa madawati. Acha hizo X minister.

Kama ni issue ya TV unaweza kufuata ukouko wanakoyagawa ukarushwa kwenye kideo na sisi tutakuyona bila chenga!!!!!!
 
inaonekaan hawa DED, wakee wa wilaya na makati tawala ni wabunge watarajiwa kwenye hayo majimbo waliopo, so tutegemee vita kubwa sanaa.
 
Back
Top Bottom