Ngassa alikataa dili la bilioni 1.6 El Merreikh

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,805
12,672
Baada ya kusoma hili andiko mwanasport nikaona huyu Mchezaji ni mwehu na kuna wengi tu wa aina yake mfano Ajibu.

Nimekopi kama ilivyo kwenye gazeti la Mwanasport

MWAKA 2012 wakati wa Cecafa kule Uganda, niliupeleka ujumbe wa klabu ya El Merreikh ya Sudan ukiongozwa na ofisa habari wao, Idrissa Adelbagi Sheikh, kwenye kambi ya Tanzania Bara kufanya mazungumzo na Mrisho Ngassa.

Mazungumzo hayakwenda vizuri. Jamaa wakaondoka kurudi kwao Khartoum.

Baada ya mashindano wakaja Dar es Salaam na dau kubwa zaidi, dola ,000 na mshahara wa dola 5,000 kwa mwezi kwa Ngassa mwenyewe, na dola 100,000 kwa Azam Fc.

Siku hiyo Tanzania walikuwa wakicheza dhidi ya Somalia, Ngassa akafunga mabao 5 peke yake. Mwenyekiti El Merreikh kule Khartoum akapiga simu kusisitiza kwamba Ngassa lazima apatikane kwa vyovyote.

Jioni tukaonana na Ngassa na jamaa walikuwa na dau la dola 100,000 kwa Ngassa mwenyewe pamoja na mshahara wa dola 4,000 kwa mwezi, na dola 75,000 kwa klabu yake ya Azam FC.

Mazungumzo hayakwenda vizuri. Jamaa wakaondoka kurudi kwao Khartoum.

Baada ya mashindano wakaja Dar es Salaam na dau kubwa zaidi, dola 200,000 na mshahara wa dola 5,000 kwa mwezi kwa Ngassa mwenyewe, na dola 100,000 kwa Azam FC.

Azam FC ikakubali, lakini Ngassa mwenyewe hakupatikana. Tukaanza kumtafuta bila mafanikio.

Jamaa wakadhani Azam FC au mchezaji mwenyewe au wote wawili wanawafanyia uhuni...wakaongeza dau la dola 300,000 na mshahara hadi dola 6,000 kwa Ngassa, na dola 200,000 kwa klabu yake ya Azam FC.

Bado Ngassa hakupatikana. Mwenyekiti akapiga simu na kusema jamaa wasirudi bila Ngassa. Adelbagi akabaki hapa Dar es Salaam akihangaika na viongozi wa Azam FC na mimi kumtafuta Ngassa...bila mafanikio.

Baadaye akaondoka na kusema wameachana na mpango wa Ngassa.

Mimi binafsi nilihangaika sana kwa sababu waliniahidi dola 10,000 endapo mpango ungekamilika.

Kwa hiyo kujificha kwa Ngassa kulinivuruga mno kwa sababu kulinikosesha pesa nyingi sana.

El Merreikh walipoondoka, Ngassa akapatikana. Kumbe alikuwa amefichwa na Yanga kwenye hoteli ya Double Tree Hilton, Msasani Dar Es Salaam.

Lakini El Merreikh hawakukata tamaa. Wakanitumia tena mkataba mwingine wenye kipengele cha kumlipa Ngassa mshahara wake wote ambao wamekubaliana, endapo klabu ingeamua kuvunja mkataba katikati.

Nikamtafuta Ngassa na kuanza kuongea naye kumuelewesha maana ya mshahara wa dola 10,000 na dau la dola 400,000 la kusainia mkataba.

Wakati huo, dola moja ilikuwa sawa na Shilingi 1,800, kwa hiyo dola 10,000 ilikuwa sawa na Sh 18 milioni.

Nikam-wambia hiyo ni bei ya kununua kiwanja kilichopimwa, maeneo ya Mivumoni na Mbweni, ambacho wakati ule kilikuwa Sh. 15 milioni.

Kwa mkataba wake wa miaka 4, ilikuwa na maana kwamba angeweza kununua kiwanja kimoja kila mwezi na baada ya miezi 48, angekuwa na viwanja 48 katika maeneo ya kifahari ambayo baadaye

angeweza kuuza kwa bei mbaya sana.

Nikamuelewesha kuhusu kuwekeza kwa kununua dhamana za serikali. Nikamwambia dola 200,000 za kusainia mkataba, ukinunua dhamana za serikali, kila mwaka unapata mgawo wa 10%... sawa na dola 20,000.

Huo ulikuwa sawa na mshahara wake wa mwaka wa wakati huo akiwa Azam FC.

Tena hapo ilikuwa kabla signing fees haijapanda hadi Dola 300,000 na baadaye Dola 400,000.

Kiufupi, Ngassa katika miaka minne ya kucheza El Merreikh angeingiza mfukoni mwake Sh. 1.6 bilioni, hiyo ikiwa ni pesa ya kusaini mkataba na mishahara yake ya miezi 48. Hapo haujajumlisha na posho nyingine ambazo angepata kutokana na mafanikio ya timu.

Akanijibu, ‘tafuta pesa kwa nguvu zako, usitegemee nguvu zangu’.

Alinijibu hivyo baada ya kumueleza kwamba katika dili lile, mimi nilikuwa na dola elfu 10. Kwa hiyo akadhani nahangaikia maslahi yangu pekee bila yeye kufaidika.

Nikatafuta namba ya baba yake, mzee Khalfan Ngassa, na kumuelewesha haya mambo niliyokuwa namuelewesha mwanaye.

Mzee akasema yeye mwenyewe anasikia kwa watu tu...Mrisho hajawahi kumwambia hata mara moja.

Nikawajibu El Merreikh kwamba Ngassa hapatikani. Ndipo wakaangukia kwa Suleiman Ndikumana wa Burundi, ambaye kwenye ile Cecafa aliifungia Burundi bao moja dhidi ya Tanzania Bara, na kuisaidia timu yake kushinda 1-0.

Leo Ngassa analalamika Yanga hawamjali yeye mzawa...anasahau kwamba alipoteza nafasi yeye mwenyewe.

El Merreikh walikuwa tayari kumlipa pesa zote hizo na kumgharamia kila kitu kule Sudan (yaani hata angeshindwa kutamba angelipwa pesa zote).

Leo angekuwa na dola 400,000 kwenye dhamana ya serikali maana yake angekuwa na uhakika wa dola 60,000 kila mwaka (sawa na Sh. 11 milioni kila mwezi).

Asingekuwa mtu wa kuilalamikia Yanga, badala yake angekuwa mtu wa kuisaidia Yanga kama alivyokuwa akifanya Mwinyi Zahera.

Pole sana Ngassa. Ingekuwa busara ungeamua kusema hadharani namna ambavyo uliivuruga kesho yako wewe mwenyewe ili kizazi kinachoibukia kijifunze kutoka kwako.

ANDIKO NIMEKOPI GAZETI LA MWANASPORT

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bongo kuna wanaume wana gene za kike, wana ile nataka sitaki.

Ukimtongoza/Ukizungumza na msichana kwa nia ya kumtaka kimapenzi na labda hata kumuoa, Atakwambia nina boyfriend, mara hili na lile. Huwa ahawaangalii how serious the issue might be, wao hukataa tu. wanataka umbembelezeeee wee , eti ukifanya hivyo ndio unampenda.

Huyo naye ukiangali story hiyo, ilikuwa ni the same situation.

Sasa mwanaume unafichwaje? kwani ukipatikana ukasikiliza kasha uka kataa au ukatafuta wataalamu wakautizama mkataba wako, na ukaamua kama mwanaume.

Eti mwananume unafichwa kama demu vile, hahaha.
 
Mbona niliwahi kusikia sababu kuu ya Ngasa kukataa/kuogopa kwenda El Mereikh ni hofu aliyokua nayo ya kufanya kipimo fulani cha afya ambacho alikua na hofu nacho kutokana na historia ya "alikopitapita"? Kwamba pamoja na uzuri, ubora na unono wa mkataba lakini ilikua lazima apime na afaulu vipimo vya afya
 
Kukosa exposure kunatugharimu sana. Pia hili neno uzalendo limeturudisha nyuma.

Wakati wa Kenya na Wanigeria wakienda nje walitafuta makazi na kuendeleza kwao, sisi tuliambiwa kuloea nje ni sawa na kuolewa na beberu.
Sky unakumbuka zile slogans za "Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha na tumenyonywa kiasi cha kutosha"? Hawa mabeberu tunawabadilishia majina tu tangia enzi. Tulianza kuwaita Mabwanyeye hadi Makabaila na Mabepari

Halafu kiongozi yoyote akienda nje akionana na diaspora anawaambia "rudini nyumbani mjenge nchi yenu huku mnajenga uchumi wa wenzenu" wakati Waganda, Wakenya na Wanigeria raia wake kwenda nje ni mkakati wa nchi. Hata China ni hivohivo

Kwa suala la Ngassa ni jambo la kusikitisha ingawa kuna habari kwamba aliogopa kupima afya ambalo lilikua ni sharti la lazima kabda y kwenda kucheza Sudan. Nadhani aliogopa historia yake mwenyewe
 
Achana na propaganda hata Kiingereza tuliambiwa ni lugha ya mkoloni. Leo hii hata cha kuombea maji hatukijui
 
Sky unakumbuka zile slogans za "Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha na tumenyonywa kiasi cha kutosha"? Hawa mabeberu tunawabadilishia majina tu tangia enzi. Tulianza kuwaita Mabwanyeye hadi Makabaila na Mabepari

Halafu kiongozi yoyote akienda nje akionana na diaspora anawaambia "rudini nyumbani mjenge nchi yenu huku mnajenga uchumi wa wenzenu" wakati Waganda, Wakenya na Wanigeria raia wake kwenda nje ni mkakati wa nchi. Hata China ni hivohivo

Kwa suala la Ngassa ni jambo la kusikitisha ingawa kuna habari kwamba aliogopa kupima afya ambalo lilikua ni sharti la lazima kabda y kwenda kucheza Sudan. Nadhani aliogopa historia yake mwenyewe
Alikuwa na tatizo gani
 
Back
Top Bottom