I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,730
- 10,033
Kutokana na taarifa za kuibuka kwa aina mpya mataifa yote yako katika sintofahamu ikiwemo taifa letu la Tanzania. Lakini ukiachana na hayo, kuna raia wengi ambao tayari walikwisha amua na kupata chanjo zote muhimu kwa ajili ya kujikinga. Lakini afikiriavyo Mungu si sawa na afikiriavyo mwanadamu. Sasa unaambiwa kuna wasiwasi chanjo hizo zikawa hazina maana tena kwa aina hii mpya. Kama tunakumbuka, tuliachiwa wosia "Daima kwa kila kitu tukumbuke kumtanguliza mungu." Na wakati huu tumefeli sana hilo tukubali.
Aina mpya ya Virusi vya Corona, B.1.1.529, ambavyo ni tofauti na kina zaidi ya mabadiliko (mutation) 50 kwa ujumla na mabadiliko mengine 30 katika muundo wa protini ambayo ndio shabaha kuu ya chanjo.
Baadhi ya mataifa duniani yamekwishaanza kuchukua tahadhari dhidi ya Kirusi hiki kipya.
Mabadiliko (mutation), inatajwa kuwa mara mbili ya kirusi cha Delta pamoja na uwezekano wa chanjo kushindwa kuhimili kirusi hiki, huku uwezekano wa kutokea kwa maambukizi ni mkubwa kuliko aina zingine za virusi vya corona.