Msafiri Kasian
JF-Expert Member
- Sep 9, 2011
- 2,133
- 659
Kwa taarifa nilizozipata kutoka kwenye website ya Tanzania Commission for Universities (TCU) zinasema;"kwa wale waliomaliza kidato cha sita, Diploma za Elimu Ufundi na ualimu mwaka 2012 wataanza kutuma maombi yao ya udahili kuanzia tarehe 7 Mei 2012 mpaka tarehe 30 Juni 2012. Waombaji wote wanapaswa kutuma maombi yao katika kipindi hiki kwa kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe ya mwisho." Vilevile: "Waombaji wanajulishwa kwamba pamoja na baadhi ya kadi kuwa zimeandikwa Tsh 50,000 malipo ya kadi yataendelea kuwa Tsh. 30,000 tu hata kwa kadi hizo", pia "Waombaji wote wanashauriwa wazitunze kadi zao vizuri baada ya kuzitumia kwa uthibitisho endapo zitahitajika. Waombaji ambao si watanzania watatakiwa kulipa $60 (dola za kimarekani sitini tu) katika matawi ya Benki ya NBC na watapewa namba ya kutumia mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kwa ajili ya udahili." katika taarifa iliyowekwa kwa lugha ya kiingereza katika website hiyo,inasomeka kama ifuatavyo;"NB: Students with less than two principal passes (two Es) at A level and less than 3 credits (C grade) at O level are advised not to attempt to apply or purchase scratch cards as they do not have the minimum requirements for admission to higher education institution degree programme. The system can only process applicants with 2 principals and above and not otherwise as the minimum requirements for admission. It is therefore advised that you read the admission requirements carefully as presented in the admission guidebook to avoid unnecessary inconveniences.Maana yake ni kwamba,kama hauna angalau,"C" tatu O-level na "E" mbili A-level,sytem yao haitakutambua.
SOURCE:www.tcu.go.tz(website ya TCU).
SOURCE:www.tcu.go.tz(website ya TCU).